Mama anafaa atambue kwamba kumnyonyesha mtoto ni jambo lenye kumpatia faida nyingi mtoto

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,646
3,936
233. Na wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada. Hailazimishwi nafsi ila kwa iliwezalo.

Asidhuriwe mzazi wa kike kwa ajili ya mwanawe, na wala mzazi wa kiume kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi (wa baba) mfano wa hivyo.

Watakapotaka kumwachisha kunyonya kwa maridhiano baina yao wawili na mashauriano basi hapana dhambi juu ya wawili hao.

Na mtakapotaka kutafuta wa kuwayonyesha watoto wenu, basi si dhambi kwenu ikiwa mtalipa mlichoahidi kwa mujibu wa shariy’ah.

Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika Allaah kwa myatendayo ni Mwenye kuona.



Mafunzo:

Faida Za Kunyonyesha:

Mama anafaa atambue kwamba kumnyonyesha mtoto ni jambo lenye kumpatia faida nyingi mtoto pamoja na mama yake, kwani ni jambo la asili Alilojaaliya Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa) kwa rahma Yake kubwa na Hikma Yake na bila shaka faida zake hakuna anayezipinga kwani hata madaktari wametambua faida nyingi baada ya utafiti. Baadhi ya hizo faida ni:
Bbc swahili ndio inatoa makala ya kuonyesha faida hii leo hii
 
Back
Top Bottom