Mama aliyepewa fedha kwenye mkutano wa Rais Magufuli, Morogoro aelezea kiasi alichopewa na alichozifanyia

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Mama aliyetoa kero kwa Rais Magufuli kuhusu wafanyabiashara kunyanyaswa na Manispaa ya Morogoro amezungumza na Mwananchi

Amemshukuru Rais Magufuli na kusema kiasi cha fedha alichopewa kilifikia 1,025,000 (milioni moja na elfu ishirini na tano)

Amesema fedha hizo alitumia kulipa kodi ya nyumba ambayo ilikuwa tayari imeisha na kulipa ada kwa watoto na kumhamisha mjukuu shule

wakati fulani tafiti ya taasisi ya twaweza iliwahi kuonyesha ccm inapendwa zaidi na watu wa vijijini hususani wale waliokosa fursa ya kuendelea na masomo ya sekondari na vyuo vikuu.

ni ngumu sana kumtawala mtu mwenye knowledge yake hata kama ni ndogo.
 
Hiyo ndio misaada isiyokuwa na malengo, amepewa samaki badala ya nyavu naye akashindwa kugeuza samaki kuwa nyavu, tumsubiri ziara nyingine ya mkulu. .
 
wakati fulani tafiti ya taasisi ya twaweza iliwahi kuonyesha ccm inapendwa zaidi na watu wa vijijini hususani wale waliokosa fursa ya kuendelea na masomo ya sekondari na vyuo vikuu.

ni ngumu sana kumtawala mtu mwenye knowledge yake hata kama ni ndogo.
Ajabu ni kuwa vyama vya upinzani vinavyojinasibu kuwa na "wasomi" ndivyo vinavyoongoza kwa kukosa demokrasia , mfano mzuri ukiwa Chadema yenye katiba isiyo na kipengele cha ukomo kwa nafasi ya mwenyekiti katika kukiongoza chama.

"wasomi" hao feki wapo, wamekiona hicho kifungu na wamekaa kimya.
 
Back
Top Bottom