Malumbano ya Spika Sitta na Mzee Mrema

Ok basi, siku za mwanzo za uhai wake kama hutaki kuamini kuwa siku za uhai wake zinahesabika!!! Mrema anajipendekeza ili apate kiinua mgongo cha Unaibu Uwaziri Mkuu wake, cheo ambacho hakipo kwenye katiba, hana jipya!!!

sasa dont you think hicho kiinua mgongo ni haki yake............he doesnt have to do that to get it????
 
Kwani mtu kufikishwa mahakamani ndio nini?

Wewe unafikiri kwamba chama ambacho kinatumia nguvu kubwa ya pato la nchi kujinunulia madaraka wataachia utawala kirahisi. Kama unafikiri kikwekt anapiga vita ufisadi nakupa pole. Mwambie kagoda ni ya nani uone alivyo na kigugumizi. Muulize meremeta ni nini asipokupa jibu kwamba ni usalama wa taifa. mwambie atekeleze azimio la bunge la kumwajibisha Hosea kama atazubutu. Maana anajua hosea alikewepo kwenye ile kamati ya kuchunguza EPA na anafahamu A to Z. Anahofia akitengua uteuzi wake atamwaga siri ya kagoda. Hata hao wote walioshitakiwa ukiangalia jinsi kesi zao zilivyo-draftiwa unagundua kuwa hawana kesi ni usanii juu ya usanii. Sasa mrema amenunuliwa kwa mkopo kuwawafinyia vurugu watu wanaoonekana kuwa na akili ndani ya ccm. Analia kwamba ccm inagawanywa kana kwamba ikigawanyika upinzani utakosa nguvu.
 
Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party Mh Augustine Mrema leo ametangaza fedha alizonazo kwenye account yake ya benki. Mrema amesema ana shilling miilion 37 kwenye hiyo akaunti ambazo zimemzidi za Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Pinda ambaye hivi karibuni alitangaza kwamba ana shilling million 25 kwenye account yake.

Mrema amehoji kama ana fedha zaidi ya Waziri Mkuu Pinda iweje Sitta aseme hana uwezo wa kifedha. Kama yeye kafulia Waziri mkuu ni vipi......

Habari zaidi nikizipata...............................
deadly wisdomly
 
  • “Kauli zako zimeniathiri, kwa sababu nimeshajitangaza kugombea ubunge wa jimbo la Vunjo.

MWENYEKITI wa Chama chaTanzania Labour (TLP) amemtaka Spika wa Bunge, Samuel Sitta, amlipe fidia ya Sh bilioni moja ndani ya wiki moja kuanzia juzi, vinginevyo atamfungulia kesi ya madai Mahakama Kuu kwa kile anachodai kwamba amedhalilishwa.

Mrema amempa Sitta taarifa ya kusudio la kumfungulia kesi ya madai mahakamani endapo hatatimiza masharti ya kumfidia na kumwomba radhi.

Katika barua aliyoiandika juzi, Mrema amempa Sitta siku saba hadi Jumatatu ijayo, kutimiza masharti yake kabla ya kumfikisha mahakamani.

“Naomba kukufahamisha, kwamba ninakusudia kukufungulia kesi ya madai Mahakama Kuu ya Tanzania kutokana na wewe Mheshimiwa Sitta kunitukana, kunikashifu, kunivunjia heshima na kunidhalilisha kupitia magazetini,” inasema sehemu ya barua ya Mrema kwa Spika Sitta.

Barua hiyo inaendelea: “Vinginevyo, uniombe radhi kupitia magazeti yale yale na kwa uzito ule ule katika kipindi cha siku saba tangu utakapopokea barua hii; unilipe fidia ya Sh bilioni moja.”

Akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Pili, Mrema alikuwa na kawaida ya kutoa siku saba kwa wahusika kutekeleza maagizo yake kabla hajachukua hatua.

Alinukuu gazeti la Mwananchi la Machi 5 mwaka huu, ambalo lilimkariri Sitta akimwita Mrema mhuni na aliyepitwa na wakati, aliyefilisika kisiasa na kifedha na kwamba sasa anatafuta njia ya kujinasua kutoka hali hiyo.

Mrema anadai kwamba kauli hizo, akiwa Mwenyekiti wa Taifa wa TLP, zimesababisha wanachama wapatao 500,000 nchini wakose imani naye. Na pia kauli hizo anadai zimemvunjia heshima aliyojijengea kutokana na utumishi wake wa zaidi ya miaka 30 akiwa Ofisa Usalama wa Taifa, Mbunge, Waziri na Naibu Waziri Mkuu.

Alisisitiza: “Kauli zako zimeniathiri, kwa sababu nimeshajitangaza kugombea ubunge wa jimbo la Vunjo.

Hivyo kauli zako zinaweza kutumiwa na wapinzani wangu dhidi yangu.” Akizungumza na gazeti hili, Mrema alisema anaendelea na mchakato wa kuandaa mwanasheria atakayesimamia shauri lake.

Alisema Mahakama pekee ndiyo itakayotoa tafsiri halali kama Sitta alimdhalilisha au la. Gazeti hili lilimtafuta Spika Sitta kwa simu kwa lengo la kumuuliza kama amepokea taarifa ya Mrema, lakini simu yake haikupatikana.

Mazingira ya kutofautiana kati ya Spika Sitta na Mrema yamekuwa yakidhihirika kupitia vyombo vya habari.

Mrema aliitisha mkutano wa waandishi wa habari hivi karibuni na kudai kwamba Sitta ni mchochezi, mjenga makundi na mtu anayehatarisha amani na usalama wa nchi, kauli ambayo inadaiwa pia Spika aliijibu kupitia Mwananchi.
 
Huyu naye na 'siku saba' zake ovyooo. Sh bil1 ? anatafuta ela ya kanga na kofia huko jimboni?
 
Mrema naona sasa anaisha kabisaaaa...anaelekea kufulia kisiasa asijeshangaa hata huko vunjo akakosa ubunge...
 
Alianza mwenyewe kumchokoza sasa amerushiwa makombora anaanza kuhaha!
 
Mzee wa Kiraracha hapa akaniacha. Anataka fidia ya bil 1 kwa sababu 'ameatirika' kisa ameisha tangaza kugombea Ubunge.

Ina maana hiyo ndo faida kamili au nusu yake anayotatarajia kupata endapo 'ataukwaa ubunge?'

Kweli huyu mzee kaishiwa.....
 
Bwana A L Mrema ana haki kabisa kumburuza mahakamani Mheshimiwa S Sitta kama anaona amekashifiwa.Ikumbukwe Bwana Mrema si mtu wa kwanza kukimbilia mahakamani kwa kukashifiwa wako kina Mheshimiwa Rostam Azziz,Reginald Mengi,Yusuph Manji na wengineo kibao kinachonishangaza wote hawakuitwa machizi,wameathirika au punguani kwa kwenda mahakamani kutafuta haki.

Mheshimiwa S Sitta anaweza kujikuta katika matatizo ambayo kwa hakika angeweza kuyakwepa,kutoa kauli kwamba fulani kafilisika kisiasa nadhani si kosa lakini unapokwenda mbali zaidi kusema fulani kaishiwa hana fedha kwa maoni yangu nadhani hiyo ni kashfa unless aweze kuithibitishia mahakama bila shaka yoyote.
 
Hii kali.
Huyu jamaa ni mjanja sana kama hamjui.
Watu wengi walishamsahau kabisaaa.
Kaanza taratibu kumpigia debe Jk. Hii iliwafanya watu wamkumbuke kidogo.
Amegeukia kwa sitta sasa hivi kageukia kwa sitta, kila
gazet. sasa ni Mrema, Mrema..
Kweli akili ni nywele.....................
 
Huyu jamaa anatumiwa 'kumchafua' Sita, mmesahau kazi zake mara hii? hamjiulizi kwa nini wakati huu Mrema anamwandama sana Sitta na sio mwingine? ana nguvu gani za kisheria kudai fidia kabla hata kesi haijaenda mahakamani? mahakama si ndo inatoa haki?
 
Wote ni wanasiasa (Mrema na Sita) na hiyoo ndo gharama ya uanasiasa.. Kauli zao ndo mitaji yao kupanda na kushukaa..
 
Back
Top Bottom