MALUMBANO YA HOJA ITV: Maulid Kambaya unaingilia mazungumnzo ya wageni

Gushleviv

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
3,473
5,274
Jamani nimekuwa mtazamaji sana wa hiki kipindi lakini kuna kitu kimoja kinanikera sana haswa tabia za waendeshaji(Watangazaji) wa kipindi hiki. Mfano kuna huyu Mtangazaji Maulid Kambaya anapenda sana kuingilia mazungumzo ya wageni kwa kuwakatisha na kujifanya anajua zaidi, kitu ambacho sidhani kama ni utaratibu.

Natoa angalizo kwa uongozi wa ITV jaribuni kuwafunza hawa vijana wenu taratibu na weledi wa kazi. haileti maana mnamualika mtaalamu aje kuzungumzia jambo alafu mtangazaji anamuingilia na kumkatisha mtaalamu na kuanza kuelezea hilo jambo.

Hawa vijana hii tabia ya ujuaji haitawafikisha popote ndio maana wenzao kina Iddi Ligongo, Kikeke na wengineo wamefika mbali sababu ya umakini katika kazi.

Naomba kuwasilisha.
 
ivi iddi ligongo yu wapi yule braza?

hii mada ya bandari naona wote hawana taarifa sahihi wanazunguka zunguka tu si huyu mama wala hawa wachangiaji
 
I'm wordless!

Nchini hatuna watangazaji wanaofuata "Skills za usomaji wa habari,ulizwaji wa maswali na uendeshaji wa vipindi".Hii kazi ni ya kitaalamu na tumeiharibu baada ya kuifanya "Hobby" kitu ambacho si sahihi.

Na-miss sana baadhi ya vichwa vya R.T.D Miaka ilee.Kuanzia kina Ahmed Kipozi,David Wakati (DG),Nassoro Nsekeli,Hega,Hillary,Aloycea Maneno nk.Pia Salim Kikeke naye anajaribu kufanya vizuri.

Wakisimamia vipindi na kutangaza utadhani upepo unapita.

ITV imejaa siasa na kujuana.Period.
 
ivi iddi ligongo yu wapi yule braza?

hii mada ya bandari naona wote hawana taarifa sahihi wanazunguka zunguka tu si huyu mama wala hawa wachangiaji
Yupo VOA (Voice of America) anakula Kipupwe...
 
I'm wordless!

Nchini hatuna watangazaji wanaofuata "Skills za usomaji wa habari,ulizwaji wa maswali na uendeshaji wa vipindi".Hii kazi ni ya kitaalamu na tumeiharibu baada ya kuifanya "Hobby" kitu ambacho si sahihi.

Na-miss sana baadhi ya vichwa vya R.T.D Miaka ilee.Kuanzia kina Ahmed Kipozi,David Wakati (DG),Nassoro Nsekeli,Hega,Hillary,Aloycea Maneno nk.Pia Salim Kikeke naye anajaribu kufanya vizuri.

Wakisimamia vipindi na kutangaza utadhani upepo unapita.

ITV imejaa siasa na kujuana.Period.

Mkuu hivyo vichwa umevitaja acha tu...ukiwasikiliza unatamani wasimalize alafu wamejawa na weledi!
 
Back
Top Bottom