Malkia wa Sheba (Queen of Sheba) ni nani?

Naskia wakimtaja sana huyu malkia wa sheba kama mwanamke flani amaizingi sana na mtaalamu sana wa mapenzi.

Pia aliwahi kumtembelea mfalme Solomoni baada ya malkia kusikia habari za hekima za mfalme Solomoni.

Inafahamika malkia alizaa mtoto wa kiume aliemuita Menelik na huyu alikuja kuwa mfalme na huu utawala ulianza mwana 1232 hadi ulipofikia kikomo pale mfalme wa mwisho Haile Selassie alipopinduliwa mwaka 1975 na habari za huu ufalme zikafikia kikomo hapo.

Walikuwa wanauita Solomon family/dynasty. Japo kwenye biblia haijawekwa wazi kwamba Solomon alilala na malkia wa sheba(makeda). Embu wenye additional information wajazie please tupate habari iliyonyooka.

Kumbuka pia Solomon alikua anapenda sana wanawake na alilala na zaidi ya wanawake 1000 so uwezekano wa wao ku sex ni mkubwa. Pia tunaona walivyo Wayahudi wengi weusi Ethiopia.

Swali langu ni juzi kuna mwanamke nilimsema vibaya akaanza kunichamba kwa maneno ya kasha kwamba yeye ni malkia wa sheba anajua sana kuteka wanaume.

Sasa najiuliza huyu mwanamke wa usheba vipi? Embu mwenye taarifa atupe kuhusu habari zake za ngono maana yaonekana alikuwa mwanamke mmoja hatari sana.
========

Baadhi ya michango kutoka kwa Wadau
Watu weupe waliingia Misri baada ya mavita yao wenyewe kwa wenyewe. ...kwa kweli mzungu amevuruga historia lakini tunashukuru kwa yote kwani MAULANA MOLA WETU RHABUKA NI MWAMINIFU SANA. ...tuna HEKIMA NA UFAHAMU NA BUSARA
 
Who is the Queen of Sheba? In the Bible we are introduced to an unnamed queen from the land of Sheba who travels to Jerusalem to meet King Solomon (see 1 Kings 10; 2 Chronicles 9). Accompanied by many attendants and camels, the Queen of Sheba brings a large quantity of spices, gold and precious stones with her. She is drawn to Jerusalem because of Solomon’s fame, and she tests the king with hard questions. Solomon is able to answer them all.
Impressed by Solomon’s wisdom —and by the riches of his kingdom—she proclaims, “Your wisdom and prosperity far surpass the report that I had heard” (1 Kings 10:7). The Queen of Sheba gives King Solomon 120 talents of gold, precious stones and the largest quantity of spices ever brought to Jerusalem (1 Kings 10:10). In return King Solomon gives the Queen of Sheba gifts and “every desire that she expressed” (1 Kings 10:13). After receiving these gifts, the queen returns to the land of Sheba with her retinue.
The Biblical account of the Queen of Sheba and King Solomon ends there, but later Jewish, Christian and Islamic sources have elaborated the story—adding details to the famous queen’s visit. In his article “Where Is the Land of Sheba—Arabia or Africa?” published in the September/October 2016 issue of Biblical Archaeology Review, Bar Kribus investigates the location of the land of Sheba and looks at the figure of the Queen of Sheba—both in the Bible and in a text called the Kebra Nagast .

Dated between the 6th–14th centuries C.E., the Kebra Nagast ( The Glory of Kings) is an important text to the Ethiopian Orthodox Church. It names the Queen of Sheba as the beautiful queen Makeda and identifies the land of Sheba as ancient Ethiopia. Kribus thoroughly examines the latter claim in his article “Where Is the Land of Sheba—Arabia or Africa?”
According to the Kebra Nagast , Queen Makeda travels to Jerusalem and has a love affair with King Solomon . Makeda then returns to the land of Sheba—giving birth to a son, Menelik, along the way. Menelik is raised in Ethiopia, but when he turns 22, he travels to Jerusalem to meet his father. King Solomon is delighted with his firstborn son and tries in vain to convince Menelik to remain in Israel and succeed him as king. However, Menelik chooses to return to the land of Sheba. Solomon sends the firstborn sons of Israel’s elders with his son from Israel to Ethiopia, and the Ark of the Covenant travels with them. To this day, many Ethiopians believe that the Ark of the Covenant resides within the Chapel of the Tablet next to the Church of Maryam Tsion in Aksum, Ethiopia.
Is this the final resting place of the Ark of the Covenant? Many Ethiopians believe that the Ark of the Covenant resides within the Chapel of the Tablet next to the Church of Maryam Tsion in Aksum, Ethiopia.
Ethiopians claim the Queen of Sheba as part of their heritage, and through her union with King Solomon, Ethiopians also claimed a connection between their kings and the Davidic monarchy of Israel. Bar Kribus explains: “Their [Ethiopian] kings were seen as direct descendants of the House of David, rulers by divine right.”
With 11 rock-hewn churches, Lalibela, Ethiopia, is understandably a place of pilgrimage for those in the Ethiopian
But is the land of Sheba truly ancient Ethiopia, as purported by the Kebra Nagast ? Archaeological and historical sources document a Kingdom of Saba (Sheba) during Biblical times in modern-day Yemen. Those in ancient Ethiopia were fully aware of the Kingdom of Saba in southern Arabia—and sometimes even appropriated aspects of their culture.
The Queen of Sheba and King Solomon: Another depiction of the Queen of Sheba is seen in Giovanni Demin’s 19th-century painting
Solomon and the Queen of Sheba, which shows the meeting of the Queen of Sheba and King Solomon.
Where is the land of Sheba? Is it in Africa or Arabia? Bar Kribus wades through history, archaeology, tradition and legend as he pieces together the story of the Queen of Sheba and investigates the land of Sheba. Who has the rightful claim to the Queen of Sheba?
 
wengi wanajifananisha hawajui historia yake au pengine jina lake pia queen of sheba. alikuwa mzuri lakini si kma cleopatra.

Cleopatra hakuwah kuwa mzuri wa sura hat kidogo , ila alikua na akili nyingi sana ; Spiritually n intellectually na alikua ana ushawishi mkubwa na haiba ya kipekee, mcheshi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nachojiuliza juu ya hii historia ni hiki.

Nabii Suleiman na Malkia huyo walizaa mtoto ni mweusi kabisa na ndiye huyu Menelik wa kwanza. Malkia alikuwa ni wa Yemen na kipindi hiko wanakaa waarabu, maana yake ni mwarabu. Sasa Mwarabu na Mtu mweupe(wengi wanavyoamini Nabii Suleiman ni mweupe) watatoaje mtoto mweusi?
 
Hadith ya Malkia wa sheba imesimuliwa kwenye vitabu Vya dini mbalimbali kama vile Wayahudi, Wakristo na hata Waislamu. Biblia imemsimulia kuwa alikuwa ni Malkia wa kutoka Mashariki Ufalme wa Aksum (axum) huko Ethiopia. Na pia kuna wanahistoria wanaosema kuwa pengine ilikuwa ni kutoka ufalme wa Saba huko Yemen au toka katika hizo Falme mbili zote kwa maana ya kuwa pengine alitawala sehemu zote mbili. Kwa nini wanasema hivyo? Ni kwa sababu alipeleka Zawadi na moja wapo ikiwa ni viungo au kwa lugha ya kigeni spices. Na ina ya spices hizo inasemekana inapatikana tu kwenye maeneo hayo mawili. Na katika hili kila nchi imekuwa ikidai ni wa kwao. Na ukichukulia kuwa nchi hizi zimetenganishwa na kilomita 25 tu za maji inawezekana zote zikawa sahihi.


Katika hadithi hii ya malkia wa sheba. Anaonekana ni malkia ambaye aliamua kutafuta hekima /elimu au ukweli kuhusiana na alichokuwa akisikia kuhusu mfalme Solomon wa Israel. Mfalme huyu alisifika kila sehemu kuwa alikuwa ni mwenye hekima sana(bahati mbaya hatujapata tena dunia hii viongozi wa namna hii) hivyo alifunga safari akitumia ngamia mpaka yerusalem kuonana na Mfalme Solomon au Selemani. Lengo lilikuwa ni kupima hekima za mfalme na pia kusikia maneno yake ya hekima,mafumbo na misemo mbalimbali. Akamletea viungo(spices) manemane,dhahabu na vito vya thaman kubwa sana. kama zawadi

Mfalme seleman alikuwa amesikia habari za Malkia Sheba na Ufalme wake mkuu. Na alisikia kuwa alikuwa na umbo la kushangaza. Kuwa mguu wake wa kushoto ulikuwa umechanika kule chini kama wa mbuzi na pia ulikuwa na vinyweleo vingi sana. Akiwa na shauku ya kutaka kujua kama hizo hadith zilikuwa za kweli au fiksi tu za walimwengu miaka hiyo.(usidhani umbea umeanza sasa au kupakaziana toka miaka ya nyuma mambo haya yalikuwepo) Mfalme seleman naye kwa kujawa na shauku na umbea wa kutaka kujua kama jambo hilo ni la kweli au vipi akaagiza siku hiyo mle ndani kusafishwe na chini pang’ae kama kioo.(nadhani nao walikuwa na tiles zao za miaka ile) inasemekana alipokanyaga pale chini malkia wa sheba mfalme selemani aliona mguu wa malkia ulio chini kama wa mbuzi ukigeuka na kuwa wa kawaida mbele ya macho yake.akashangaa sana.

Malkia wa sheba akawa akimuuliza mfalme maswali mengi mengi sana na mafumbo ili kumpima hekima yake. Akamjibu kiasi cha kumridhisha kabisa na malkia akafurahia sana na baadaye akamfundisha kuhusiana na Mungu wake yeye Mfalme Seleman (Yahweh) na Malkia wa Sheba akawa muumini wake. Na hivi ndivyo Waethiopia wanaamini Jinsi ambavyo Ukristo uliingia nchini mwao yaani kupitia Malkia wa Sheba.

Malkia alikubali kuwa Mgeni wa Mfalme Seleman.na hapo alikuwa hajaolewa. Akamwonya mfalme seleman asimguse.(najua unaelewa maana ya asimguse). Na mfalme seleman akamwambia kama ni hivyo naye asichukue kitu chochote toka kwake. (toka zaman wanaume walikuwa hawatoi tu zawadi hivi hivi) na hapa mfalme alikuwa amemtega kiujanja kumbuka alikuwa na hekima sana. basi malkia akapewa chakula chnye spices nyingi sana(mfano ukila pilau matokeo yake unakunywa sana maji) Ulipofika usiku Malkia akasikia Kiu. Akachukua Glass ya Maji akanywa. Mfalme akamfuata na kumwambia amevunja makubaliano kuwa hakupaswa kuchukua kitu chochote toka kwake kwa kuwa yeye alisema asiguswe. Hivyo kwa kuahidi kuwa singechukua kitu chochote na mwishowe kunywa maji ya mle ndani amevunja ahadi na mfalme naye atavunja ya kwake ya kutokumgusa.

Basi hapo wakalala wote yaani wakafanya mapenzi na kumbuka mfalme alikuwa amemsubiria kwa hamu sana. Akamnanii….. na siku aliporudi nyumban kwake Malkia wa sheba alikuja kugundua ana ujauzito akamzaa Menelik na kumkuza yeye mwenyewe. Siku moja menelik akaamua kutembelea Israel kwenda kuonana na baba yake. Aliporudi alikuja na sanduku la agano lililokuwa limebeba amri kumi za Mungu alizotoa kwa Wayahudi. Hadith za kale zinasema kuwa sanduku liliendelea kuwa Ethiopia toka kipindi hicho na Waethiopia wana mwona Menelik kama ni Ufalme uliotukuka uliojipanua mpaka karne ya 20. Hii ndiyo hadithi ya Malkia wa sheba.
MENELIK ALIKUJA NA SANDUKU LA AGANO LILILOKUWA NA AMRI KUMI ZA MUNGU ALIZOTOA KWA WAYAHUDI
hizi amri kumi kwa mujibu wa biblia zilishuka kwa musa alipokuwa jangawani akielekea kanani na musa alikuja baadae sana baada ya selemani ,hadithi za biblia zinajichanganya sana
 
wengi wanajifananisha hawajui historia yake au pengine jina lake pia queen of sheba. alikuwa mzuri lakini si kma cleopatra.
ebu tupe tufauti unayoijua ya uzuri wao kati ya huyo sheba na cleopatra
 
Musa alikuja baada ya suleiman teh teh kasome tena Biblia mkuu
MENELIK ALIKUJA NA SANDUKU LA AGANO LILILOKUWA NA AMRI KUMI ZA MUNGU ALIZOTOA KWA WAYAHUDI
hizi amri kumi kwa mujibu wa biblia zilishuka kwa musa alipokuwa jangawani akielekea kanani na musa alikuja baadae sana baada ya selemani ,hadithi za biblia zinajichanganya sana
 
ndio musa alikuja baada ya suleiman ,ina maana hujui hilo? kama huji ficha ujinga wako endelea kusoma coments za watu ujifunze.
musa ni wajuzi tu ,baada ya musa ndio akaja yesu
 
ndio musa alikuja baada ya suleiman ,ina maana hujui hilo? kama huji ficha ujinga wako endelea kusoma coments za watu ujifunze.
musa ni wajuzi tu ,baada ya musa ndio akaja yesu
 
Suleiman alisex naye akampata mtoto wa kwanza alieitwa menelik ambao ndio ufalme ulianzia hapo wa kisolomon ukafikia kikomo pale haile selassie alipipinduliwa mwaka 1975. acha ubishi kwenye biblia haijawekwa wazi ila kunasehemu niliona baada ya menelik kuwa mkubwa alienda kumtembelea baba yake (solomon) na huko alipewa zawadi pia solomon alituma watumish kwa ajili ya kuiangalia hiyo familia, kumbuka alitaka amfanye awe meneli awe mfalme wa israel lakini ilishindikana
hapana ufalme haukuanzia hapo. kama ufalme ulianzia hapo wakati anaenda kumtembelea sulemani alikuwa nani huoni unaondoka kwenye point mkuu
 
1000 ivi na kitu ndio huyu mtoto wa malkia wa sheba alianza ufalme then later ukaitwa solomon dynast (menelik ndio mtoto wa kiume wa huyu malkia) ukomo wa huu ufalme wa solomon uliisha pale haile selesie alipopinduliwa mwaka 1975.
habari ya menelik ni ya juzi sana malkia wa sheba alikuwa mtawala wa ethiopia na sio kwamba huyo mtoto alianzisha ufalme hapana isipokuwa aliukuta na yeye akapata nafasi kuuendeleza. kiufupi huyo mtoto ndo alileta uchafuzi kwenye historia ya ethiopia
 
Jedediah ndiye mfalme Suleimani, linamaanisha MPENDWA WA MUNGU. Hili ndiyo jina halisi la mfalme Suleimani na alipewa na nabii Nathani mara baada tu ya kuzaliwa. Kwa maelezo zaidi soma 2 Samuel 12:25.
Haya turudi kwenye mada yetu, baada ya Malkia Mekeda kwenda kwa Mfalme Jedediah alimjaribu lakini akakuta Suleimani ana utajiri mkubwa wa kuisha na akili kumkichwa. Sasa wanahistoria wa Kiyahudi wanasema kwamba Mekeda akaambiwa na Suleimani alale kwenye kasri yake lakini akamuambia mfalme Suleimani kama ukitaka nilale Sharti usiniguse. Suleimani akamwambia sawa lakini na wewe usiguse kitu chochote cha ndani ndani ya nyumba yangu bila ruhusa yangu.

Suleimani alikuwa na mpango wake kichwani, akawaagiza watumwa wake waweke pilipili na viungo vingi kwenye chakula.
Makeda alivyokula usiku kiu kali ikamshika, basi akataka maji Suleimani akamjibu akasema tulikubaliana hutagusa chochote bila ridhaa yangu. Basi Makeda akazidiwa ujanja ndiyo maana akasema Suleimani ni Mfalme mwenye akili sana kuliko alivyowahi kusikia.

Aliondoka Yerusalem na mimba, akajifungua mtoto wake wa kiume akamuita jina MENELEKI 1 maana yake "SON OF THE WISE". Menelik alivyokuwa mkubwa alienda kuapishwa Yerusalem. Na mwanahistoria wa Kirumi Flavius Josephus anakuambia alikuwa Mfalme wa Ethiopia na Egypt, hapo alipewa jina la babu yake DAUDI. Sasa alivyorudi Ethiopia Mfalme Suleimani alituma kundi la Wasomi wa Kiyahudi zaidi ya 1000 na moja wapo walikuwa kuhani AZALIA na ZADOKI ambao kwenye biblia wapo. Hawa walitumwa kwa dhumuni la kumsaidia atawale ufalme wake vizuri.

Wayahudi wa Ethiopia wale wuesi wanaitwa Falahasha na siyo wote ni uzao wa Mfalme Suleimani. Wengine ni wayahudi kutoka kabila la dani ambalo walipotea baada ya kuvamiwa na Ashuru na Wakaldayo kutoka Babeli. Wayahudi weusi wako wengi sana na hichi watu wengi wanakipinga lakini ndiyo ukweli wenyewe. Lakini Wayahudi walianza kuoana na weusi tangu wako Misri na ushahidi mkubwa ni Abrahamu baba wa Wayahudi alizaa na kijakazi wake Hajira ambaye ndiyo mama wa Waarabu. Hajira alikuwa ni mtu wa Misri na Misri ilikuwa inatawaliwa na watu weusi kabla ya Waarabu. Sehemu ya Pili Nabii Musa alimuoa Zipora mtu wa Ethiopia. Ethiopia ilikuwa inatawaliwa na watu weusi hivyo kuwepo na Wayahudi weusi ni kitu cha kawaida sana.
biblical israelite ni weusi
 
m
ndio musa alikuja baada ya suleiman ,ina maana hujui hilo? kama huji ficha ujinga wako endelea kusoma coments za watu ujifunze.
musa ni wajuzi tu ,baada ya musa ndio akaja yesu
musa ni kabla wewe kweli hujui kitu kama musa alikuja baada ya sulemani nani aliwatoa wana wa israeli misri?
 
Back
Top Bottom