Malisa na Mikopo ya Elimu ya Juu

Malisa na Mikopo ya Elimu ya Juu

Kabisa Mkuu miaka hii ukipata bahati ya kwenda kusoma nje au kufanya kazi nje hakikisha kuja bongo ni kutembea tu na huko uliko fanya juu chini upate makaratasi ili uishi kihalali.

!
!
Baki Huko Huko Tu Fanya Mambo Yako. Bongo Nyoso Alikuwa Hajui? Ndio Atajua Sasa
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Wengi waliosoma nje ya nchi kwa kulipiwa na bodi ya mikopo (HESLB) wanadaiwa fedha nyingi kulinganisha na waliosoma nchini. Nimeona jamaa ana mshahara 900K but anadaiwa 47M. Kwa mwezi atakatwa 143K, kwa mwaka 1.7M. Under "ceteris paribus" mwamba atahitji miaka 28 kumaliza deni lake. Lakini ukiongeza "rention fee" atahitaji miaka 35 kumaliza deni.

Assume ana mika 30 kwa sasa. Jumlisha 35 ya kulipa deni atakua na miaka 65. Umri wa kustaafu ni miaka 60. Maana yake atastaafu bila kumaliza kulipa deni. Ikitokea hivyo Bodi itaenda kukomba kiinua mgongo chake kumalizia deni (kama sheria inavyosema). Sasa jiulize je huku ni kumsaidia mtanzania au kumkomoa?

Kunapaswa kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu mikopo ya elimu ya juu. Wazazi wanaoweza kusomesha watoto wao kwa kuwalipia ni vizuri wafanye hivyo, badala ya kuwaingiza kwenye mikopo hii inayoumiza. Pili, wazazi wasio na uwezo serikali iwape watoto wao ruzuku (bursary) si mikopo (loan)

Awamu ya kwanza na ya pili serikali iliwapa ruzuku wanafunzi wote wa elimu ya juu. Awamu zilizofuata zikaondoa ruzuku na kuleta mikopo. Nyerere na Mwinyi waliweza nini ambacho kimewashinda waliofuata?

Wakati wa Nyerere na Mwinyi wanafunzi wa vyuo vikuu walikula bure, kusoma bure, na kulala bure. Na bado walipewa pesa ya kujikimu. Kuna kipindi nchi ilipita kwenye hali ngumu kiuchumi Nyerere akapunguza bajeti ya mayai kwenye breakfast ya wanafunzi wa UDSM. Wakafanya mgomo. Akawaita Ikulu na kuwatia bakora

Wakati ule mwanafunzi hana pressure ya ada, kula wala kulala. Anapewa pesa ya stationeries, field na research. Asubuhi anapewa breakfast yenye mapochopocho kibao (maziwa, mkate, mandazi, pancacke, chees, jam, mayai, juice, sambusa, sosage etc). Halafu wanapunguziwa mayai wanaamua kugoma. Nyerere akawatia bakora. Akawaambia msijifanye nyie ni muhimu kuliko watanzania wengine.

Sasa wale waliosomeshwa kwa ruzuku na kupata fursa zote hizo, ndio wameleta kitanzi kinaitwa mikopo ya elimu ya juu. Kitanzi hiki kimewatesa sana watoto wengi wa maskini. Hivi Nyerere nae angeweka mikopo hawa viongozi wa leo wangesoma? Nashauri MIKOPO ifutwe wanafunzi wapewe RUZUKU kama zamani. Rasilimali tulizonazo kama taifa zinatosha.!

Malisa GJ
Sumaye alikomalia sana sheria ikapita bungeni, makamanda hawahawa kina malisa wakamchukua aongoze mabadiliko na kina eddo
 
Ni heri mzazi anayeweza kumsomesha mtoto bila loan za heslb afanye hivyo.
 
Wakati mnaomba mikopo,mlipewa karatasi zenye maelezo ya jinsi mikopo hiyo itakavyolipwa, hakuna aliehoji au kukata. Baada ya hapo mkawa mnafurahia boom na kusoma bure.
👉Sasahivi kwenye ulipaji mnaaza kurukaruka. Kwanini mlisaini🤔?Lipeni hizo pesa ili na wengine wanufaike. ☹️
 
Walipe tu hakuna namna maana walipo vyuoni wanataka mikopo wasilete siasa uchwara kwenye mikopo
Watu wengi wenye mawazo kama yako mara nyingi wakizeeka wanageuka kuwa washirikina
 
Wakati mnaomba mikopo,mlipewa karatasi zenye maelezo ya jinsi mikopo hiyo itakavyolipwa, hakuna aliehoji au kukata. Baada ya hapo mkawa mnafurahia boom na kusoma bure.
👉Sasahivi kwenye ulipaji mnaaza kurukaruka. Kwanini mlisaini🤔?Lipeni hizo pesa ili na wengine wanufaike. ☹️
Amini usiamini watu wengi wenye mawazo na fikra kama za kwako wakizeeka wanageuka kuwa washirikina
 
Nilipokuwa nafuta ujinga katika elimu ya juu, kuna wakati nilijikuta najikunyata pale ambapo wanafunzi wenzangu walipokuwa wanatangaziwa kwenda kusaini "bumu". Kuna wakati ilinibidi nijichanganye na marafiki zangu ili na mimi nionekane wa maana, yaani mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu, kulikuwepo kama kaunyanyapaa kiaina hivi "huna mkopo"?

Maisha ya chuo yaliendelea mpaka tukamaliza japo sikufanikiwa kumaliza Ada yote lakini namshukuru sana mkuu wa chuo alinielewa na baada ya miezi minane hivi ya kuhitimu chuo nilifanikiwa kulipa deni lote nikapewa cheti changu.

Nataka kusema nini hapa, wale waliopata mkopo wa elimu ya juu hawaoni kama mkopo ulikuwa na unafuu katika elimu yao bali lilikuwa bomu linalo walipukia sasa. Nashauri mamlaka husika zirekebishe sheria hii ili kuleta unafuu wa mkopo unaolipika bila kuweka ongezeka lolote. Kama mwanachuo alikopeshwa 6m.alipe 6m. Mkopo wa elimu siyo biashara.

Nawatakia kheri ya mwaka mpya 2021.
Asante mkuu
 
Wanafunzi wakinyimwa/kucheleweshewa mikopo Nyuzi za kuilaumu GOT ni za kutosha!lipeni tuu haya madeni Waungwana,mapovu hayasaidii...ule ulikuwa ni mkopo.
Amini usiamini wstu wenye mawazo kama yako mara nyingi wakizeeka hugeuka kuwa washirikina
 
Mi nachoona hapa sio kila mtu aende chuo. Elimu ya secondary na primary inatosha sana kusurvive maisha ya Tz maana kitakwimu. 99% ya watz wanaish kusurvive.
 
Roho mbaya...hakuna anayekataa kulipa...rudi nyuma fuatilia kwa nini watu wanalalamika na bichwa lako kubwa
Kama ulijua kuwa hautakuwa na uwezo wa kulipa hilo deni ungekomea tu sekondari, maana hata hiyo elimu ya chuo naona bado haijakusaidia.Wenzako wanajadili hoja we unaendekeza mipasho kama shoga☹️.
 
Hv unajua mpaka kuwa sheria inaanzia wap
Kuna vingine naona, anapewa lawama zisizo za lazima... Unajua kuna muda ukiwa mkubwa on top, mambo yanakuwa mengi hadi kiasi cha kushindwa kuyaona mengine... Lawama zinatakiwa ziende kwa wale wasaidizi ambao walikaa chini na kufanya mahesabu yao.. kisha kumpelekea hiyo sheria na kumuamisha... Yeye si wa kulaumiwa kwa kila jambo
 
Nilipokuwa nafuta ujinga katika elimu ya juu, kuna wakati nilijikuta najikunyata pale ambapo wanafunzi wenzangu walipokuwa wanatangaziwa kwenda kusaini "bumu". Kuna wakati ilinibidi nijichanganye na marafiki zangu ili na mimi nionekane wa maana, yaani mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu, kulikuwepo kama kaunyanyapaa kiaina hivi "huna mkopo"?

Maisha ya chuo yaliendelea mpaka tukamaliza japo sikufanikiwa kumaliza Ada yote lakini namshukuru sana mkuu wa chuo alinielewa na baada ya miezi minane hivi ya kuhitimu chuo nilifanikiwa kulipa deni lote nikapewa cheti changu.

Nataka kusema nini hapa, wale waliopata mkopo wa elimu ya juu hawaoni kama mkopo ulikuwa na unafuu katika elimu yao bali lilikuwa bomu linalo walipukia sasa. Nashauri mamlaka husika zirekebishe sheria hii ili kuleta unafuu wa mkopo unaolipika bila kuweka ongezeka lolote. Kama mwanachuo alikopeshwa 6m.alipe 6m. Mkopo wa elimu siyo biashara.

Nawatakia kheri ya mwaka mpya 2021.
Tatizo ni pale serikali inapojitoa kuendesha shughuli za bodi kwa kuwalipa mishahara wafanyakazi wake na kugharimia vitendea kazi vya bodi. Hivi sasa bodi inatumia marejesho ya mikopo kulipa mishahara ya wafanyakazi wake na kugharimia vitendea kazi vya bodi na pia kutoa gawio serikalini kama vile wanafanya biashara.

Utaratibu huu ni janga kubwa na litaendelea kuwaumiza wakopaji. Ili kuwaokoa wakopaji serikali haina budi kutenga bajeti ya kuendesha shughuli za bodi na kudhibiti mishahara ya wafanyakazi wake ambayo ni mikubwa mno. Kwani kadri mishahara inavyoongezeka ndivyo wakopaji wananyominywa zaidi!
 
Back
Top Bottom