Kinkunti El Perdedo
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 5,537
- 13,847
Uchumi wa kati watanzania watalipa tu
Kuna vingine naona, anapewa lawama zisizo za lazima... Unajua kuna muda ukiwa mkubwa on top, mambo yanakuwa mengi hadi kiasi cha kushindwa kuyaona mengine... Lawama zinatakiwa ziende kwa wale wasaidizi ambao walikaa chini na kufanya mahesabu yao.. kisha kumpelekea hiyo sheria na kumuamisha... Yeye si wa kulaumiwa kwa kila jamboRahis wa wanyonge mungu anamuona
jitahidini kusoma post na kuielewa kabla hamjatoa matapishi yenu. Mbona post iko clear? Mnakwama wapi vijana wa praise and worship?Mikopo ni swala nyeti.shameful.
Chief kinacho matter hapo ni isssue ya kufuta neno loan, bali kiitwe Ruzuku.Basi serkali isitishe kutoa mikopo kila mtoto ajilipie kuepusha kelele
Akili zako zina Shida wewe. Huelewi kitu gani hapo? Akili zako unajua watu wanampinga JPM? Pimbi weweBasi serkali isitishe kutoa mikopo kila mtoto ajilipie kuepusha kelele

Kuishi kwa matumaini ambayo huna hakika kama yatakuja.Sitegemei hii bodi itakuwepo miaka yote, Kuna serikali itakuja madarakani itafanya marekebisho, na hata fao la kujtoa tungoje Magufuli aondoke Kuna serikali ya kiongozi mwenye huruma tutapata ataondoa haya mateso yanayotengenezwa na binadamu maana haya si majanga ya asili.
Uelewe kuwa si kila anayetoa maoni ni mhusika wa Hilo Jambo, Mimi si mkopaji huko bodi ya mikopo ila naona malalamiko mengi na Wala siishi kwa matumaini Mimi NI mstaafu.Kuishi kwa matumaini ambayo huna hakika kama yatakuja.
Hapo kwenye kuchapwa viboko kwa kulilia mayai kwenye kifungua kinywa "umechapia".Wengi waliosoma nje ya nchi kwa kulipiwa na bodi ya mikopo (HESLB) wanadaiwa fedha nyingi kulinganisha na waliosoma nchini. Nimeona jamaa ana mshahara 900K but anadaiwa 47M. Kwa mwezi atakatwa 143K, kwa mwaka 1.7M. Under "ceteris paribus" mwamba atahitji miaka 28 kumaliza deni lake. Lakini ukiongeza "rention fee" atahitaji miaka 35 kumaliza deni.
Assume ana mika 30 kwa sasa. Jumlisha 35 ya kulipa deni atakua na miaka 65. Umri wa kustaafu ni miaka 60. Maana yake atastaafu bila kumaliza kulipa deni. Ikitokea hivyo Bodi itaenda kukomba kiinua mgongo chake kumalizia deni (kama sheria inavyosema). Sasa jiulize je huku ni kumsaidia mtanzania au kumkomoa?
Kunapaswa kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu mikopo ya elimu ya juu. Wazazi wanaoweza kusomesha watoto wao kwa kuwalipia ni vizuri wafanye hivyo, badala ya kuwaingiza kwenye mikopo hii inayoumiza. Pili, wazazi wasio na uwezo serikali iwape watoto wao ruzuku (bursary) si mikopo (loan)
Awamu ya kwanza na ya pili serikali iliwapa ruzuku wanafunzi wote wa elimu ya juu. Awamu zilizofuata zikaondoa ruzuku na kuleta mikopo. Nyerere na Mwinyi waliweza nini ambacho kimewashinda waliofuata?
Wakati wa Nyerere na Mwinyi wanafunzi wa vyuo vikuu walikula bure, kusoma bure, na kulala bure. Na bado walipewa pesa ya kujikimu. Kuna kipindi nchi ilipita kwenye hali ngumu kiuchumi Nyerere akapunguza bajeti ya mayai kwenye breakfast ya wanafunzi wa UDSM. Wakafanya mgomo. Akawaita Ikulu na kuwatia bakora
Wakati ule mwanafunzi hana pressure ya ada, kula wala kulala. Anapewa pesa ya stationeries, field na research. Asubuhi anapewa breakfast yenye mapochopocho kibao (maziwa, mkate, mandazi, pancacke, chees, jam, mayai, juice, sambusa, sosage etc). Halafu wanapunguziwa mayai wanaamua kugoma. Nyerere akawatia bakora. Akawaambia msijifanye nyie ni muhimu kuliko watanzania wengine.
Sasa wale waliosomeshwa kwa ruzuku na kupata fursa zote hizo, ndio wameleta kitanzi kinaitwa mikopo ya elimu ya juu. Kitanzi hiki kimewatesa sana watoto wengi wa maskini. Hivi Nyerere nae angeweka mikopo hawa viongozi wa leo wangesoma? Nashauri MIKOPO ifutwe wanafunzi wapewe RUZUKU kama zamani. Rasilimali tulizonazo kama taifa zinatosha.!
Malisa GJ