Malisa GJ: Umuhimu wa Katiba Mpya

Hata vyama vingi wengi walikataa lkn yakafanyika mabadiliko,msitumie ujinga wa wtz wengi kuendelea kutawala
Wanaodai katiba kwa nguvu sio wananchi ila ni CHADEMA idadi yao haifikii hata robo ya watanzania wote

Na hao CHADEMA wanadai hiyo katiba kwa tamaa yao ya madaraka wanahisi labda litakua daraja la wao kuingia madarakani na ndio maana wakuzungumzia katiba mpya wanalenga katika tume ya uchaguzi

In short ndio CHADEMA inakufa maana mtapoteza hi miaka 4 yote kudai katiba na hiyo katiba haitapatikana

R.I.P CHADEMA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kujidanganya ww,mataifa mengi ya ulaya magharibi yalipata maendeleo makubwa baada ya mabadiliko ya kisiasa sambamba na katiba bora.
Hiv kwann chama chakavu mnaiogopa katiba mpya????yaan bdo mnataka hii mbeleko iliyopo ktk hii katiba chakavu?????
Mkuu umewahi kuisikia katiba ya uk au kujua ilivo?? Jiulize ndo utatajua kuwa mifumo ipo tofauti Sana...

Mkuu ninajidanganya vp???
 
Kwanza, mkuu wananchi kutokuelewa katiba yao ni uthibitisho tosha kwamba maendeleo ya kijamii katika nchi yetu ni mabaya sana mkuu. Kutokuelewa katiba yao maana yake hiyo jamii ina tongotongo kubwa sana katika macho yao.

Pili, kutokujua katiba yao inasemaje siyo hoja kubwa sana kwani huo ni uzembe wao. Sasa suala la uzembe wao wa kutokufuatilia mambo mbalimbali kwa manufaa yao yasikwamishe mchakato wa katiba mpya.

Tatu, mkuu katiba mpya tunayoitaka ni ambayo itaakisi maisha halisi ya Watanzania na yenye kuleta tija katika jamii na siyo ya copy & paste.

NB: suala la wananchi kutokujua katiba yao ya sasa ni uzembe mkubwa sana na siyo sababu ya msingi ya kutuzuia kuwa na katiba mpya.
Mambo 2 makuu,

mwenye jukum la kufanya katiba ieleweke ni Nan?? Tufanye ok.. ni uzembe wa mwananchi. Je aachwe hvyo au aelimishwe?? Je ktk uzembe wake ameathirika kwa namna ipi kwa kutokuwepo matakwa ya Sasa ya katiba??

Pili hyo katiba itachunjwaje? Ikiwa hakuna kura ya maoni kwa watu wote wakiwa huru Kama wanataka mabadiliko ya katiba au la?? Je sis tulio andika ni % ngp ya wale wanaohitaji katiba?? Kwa utafiti upi?? Walao tungejua kuwa wtz wangp wamehojiwa ktk makund yapi ambao wamesema wanataka au hawaitaki..

Walugulu wanasema NO RESEARCH NO RIGHT TO SAY(kama ntakuwa nmepatia).. tusiende na mihemko tuuuuuuuu.. nakubaliana nawe ila utafiti huru kabisa ufanyike...
 
Kabla uongo wake wa list feki ya Lissu kulipwa mafao yake na bunge haujakauka vizuri leo malisa ameamua kuhara uongo mwingine!

Haya ngoja tuone mauzo ya cocaine yatqkavyokuwa mitaani baada ya punda kuachiwa huru na mahakama.
Mkuu hoja ya katiba Mpya wewe unaiunga mkono?
 
Tunahitaji kuwa na katiba bora kabisa kwa Africa & Dunia kwa sasa ili kumuenzi yule mwendamahoka
 
Mkuu umejibu kwa hisia za kisiasa au kwa matink?? Kwa hyo Sasa hv tunaviongoz wabovu??
Umejibiwa kwa manyik. Sema hautaki kusikia ukweli.

Katika utawala wowote kunakuwepo na viongozi wabovu. Kama ulivyofahamishwa, Katiba Mpya itawapunguza na watakapoonekana itakuwa rahisi zaidi kuwashughulikia hata kama watakuwa wanalindwa na baadhi ya watu.

Amandla...
 
Hakuna umuhimu wa katiba mpya full stop tujenge nchi, hatuwezi kuridhisha wachache tukaacha maslahi ya wengi.
 
Aseme ukweli kwamba KATIBA MPYA ni takwa la WANASIASA sio WANANCHI
 
Muda wangu wa kuchangia nimeutumia kujibu maswali matano yanayoulizwa na wengi huko mtaani kuhusu Katiba (5 common questions).

1. Kwanini mchakato huu umeandaliwa na BAVICHA? Mnapigania Katiba ya nchi au ya Chadema?

#Jibu: Mchakato wowote wa katiba ni wa kisheria na kisiasa. Katiba ni jambo linalogusa watu wote, hivyo kila kundi lina haki ya kujadili. Vijana wa chama cha zamani, badala ya kuwaonea gere BAVICHA, nanyi mnaweza kuandaa kongamano lenu. Muhimu kila mtu apate nafasi ya kuamua muastakabali wa taifa letu.

2. Katiba mpya sio kipaumbele cha Rais, kwanini msiachane nayo?

#Jibu: Katiba sio mali ya Rais ni mali ya wananchi. Hivyo kama wananchi wanataka katiba mpya, Rais hawezi kuzuia kwa namna yoyote. Kama wananchi wakisema Katiba mpya ni kipaumbele chao, Rais atake asitake atalazimishwa (kwa sauti ya kimbunga Jobo).

3. Je, Katiba mpya ina umuhimu wowote?

#Jibu: Ndio. Itatuwezesha kupata tume huru ya uchaguzi, ambayo mchezaji wa timu pinzani hataweza kujigeuza refa kama ilivyo sasa. Itaimarisha uchumi kwa sababu wawekezaji wote wakubwa duniani hupenda kuinvest mitaji yao mahali penye stability ya kisiasa. Pamoja na faida nyingine nyingi (ambazo zimetajwa na wazungunzaji wengine) katiba mpya itamfunga "breki" Rais asiteue majambazi kama Sabaya na kuwapa ofisi za umma.

4. Kwanini tusifanye marekebisho kidogo ya Katiba iliyopo badala ya kudai mpya?

#Jibu: Katiba iliyopo imeshafanyiwa marekebisho mengi sana. Kati ya mwaka 1980 hadi 1995 ikifanyiwa marekebisho mara 13. Kama ni nguo basi imechakaa na ina viraka vingi sana. Kwahiyo badala ya kutafuta mahali pengine pa kuweka kiraka, ni bora tununue nguo mpya.

5. Kwanini Mchakato wa Katiba usisubiri kwanza ili tujenge uchumi kama alivyosema mama Samia?

#Jibu: Wakati akiongea na waandishi wa habari, Mama Samia alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, uchumi wa nchi uliporomoka kutoka 7.2% hadi 4.8%. Kumbuka kipindi hicho mchakato wa katiba ulikua umesimamishwa. Kama kuzuia Katiba mpya kunasaidia kujenga uchumi, basi ilitakiwa kipindi cha mwendazake uchumi uimarike kuliko wakati mwingine wowote, lakini haikua hivyo.

Ama kwa hakika CDM na BAVICHA ni "think tank" kwa maana ya kujali mustakabali mwema wa nchi hii. Kwa maana hiyo, CCM na UVCCM yake kumejaa "empty cases" wengi mno, hata mambo muhimu yaihusuyo nchi yao hawajali kabisa, zaidi ya chama chao kichakavu na matumbo yao wenyewe.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
  1. Katiba mpya ni takwa la kijamii, na linapata msukumo mkubwa na wanasiasa kwani katiba ni mchakato wa kisiasa.
  2. Katiba imeanza kudaiwa toka 1992 mfumo wa vyama vingi uliporejea hapa nchini. Huenda wakati huo hukuwa umezaliwa. 2010-2015 kulifanyika msukumo mkubwa wa kupata katiba mpya, hatimaye ilitungwa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya, na tume ya Jaji Warioba ilizunguka nchi nzima, kukusanya maoni ya wananchi. Hatimaye kukawa na katiba pendekezwa ambayo ilikuwa inasubiri kupigiwa kura japo rasimu ya Warioba ilichezewa. Miaka mitano iliyopita nchi hii ilikuwa mikononi mwa rais muovu, aliyekuwa hataki katiba ya kumzuia kwenye uovu wake. Ila kwenye ilani ya ccm mchakato wa katiba pendekezwa ulikuwepo,lakini rais mwenye kiburi cha madaraka aliigomea. Tunashukuru Mungu kwa kutuondolea yule mtu muovu bila damu kumwagika.
  3. Katiba mpya italeta maendeleo maana itatoa viongozi wenye uhalali wa umma, na wataweza kuwajibishwa iwapo watakosea. nchi za Kenya, Afrika kusini na Ghana ni mifano halisi wa nchi zenye katiba bora, na zinaaminika hata na wawekezaji, kwani zinajali utawala wa sheria, na sio utashi wa rais aliye madarakani.
  4. Tume ya uchaguzi ni sehemu tu ya mapungufu ya hiyo katiba, lakini kuna madaraka makubwa ya urais ambayo yanatumika vibaya, na kwa maslahi binafsi ya rais na genge lake. Udhaifu huo umedhibitika wazi wakati wa JK, na rais muovu aliyefariki hivi karibuni.
  5. Bila utawala wa sheria ni ngumu muwekazaji makini kuwekeza, mfano hali ni wakati wa Magufuli wawekezaji wengi waliondoka. Kama hakuna wawekezaji ni ngumu uchumi kukua. Pia ni rahisi nchi kuingia machafuko ni, kwani hakuna haki. Kama katiba mpya haisaidii mtu wa kijijini, hayo maVX ya serikalini yanawasaidia nini hao wananchi?
 
Wewe ni product makini sana,,kama 60% ya vijana wangalifaham hivi basi,tungefika mbali sana kama taifa ,,,keep on educating
 
Ukiona umejibu swali, badala ya kufunga mianya ya maswali, inakuwa umefungua mianya ya maswali zaidi, maana yake jibu ulilojibu ni zuri lakini sio sahihi.

Majibu ya kaka yetu kipenzi Malisa ni mazuri ila yana mapengo kibao.

Namshauri apunguze hisia afanye tafiti aje na objective answers.
Swali la ngapi majibu yake yana mianya doon
 
Kimsing nakuelewa walao Sasa Kama ndvyo umhim wa katiba mpya uanzie wapi?? Wakati katba ile ambayo mchakato wake ulikwama na hakuna sabba ya kwa nn ulikwama nlikuwa nafanya kazi maeneo tofaut ya kijijn.. baadhi ya watu nliokutana nao hawakuwa na uelewa walao hata wa neno katiba wengine waliniuliza hv hulo bunge la katiba maana yake Nini??

Kwa hyo kunakazi Kwanza ya kuielimisha jamii ya Sasa katiba maana yake Nini.. mapungufu yaliyopo kwenye katiba ya Sasa na kwa nn tutake katiba nyingine..
Na je tunaiunda Kama copy&pest ya ambayo haikufikia muafaka au tunaitaka tuunde ya kwetu??

Mkuu hatuundi katiba kwa kuangalia wengine wameundaje ya kwao ila jambo la Msingi tujue hasa mahitaji ya jamii yetu ni yapi..

Umesema vyema MAENDELEO si kuangalia tu binafsi ila ya ujumla.. na hapo ndpo tunapokuja na vipaumbele... Ni vyema tujiridhishe Kama kwel jamii ya Sasa kwa takwim halisi tunahitaji katiba??

Halafu hii mifano ya eti watu wa kijijini hata hawaelewi katiba nini, kwani hao watu wa kijijini wanajua nini sana mpaka wasubiriwe waelewe? Hao watu wa vijijini wanajua kwanini viongozi wanatembelea maVX? Kuna popote mmejadiliana na watu wa huko vijijini ni magari gani yanawafaa viongozi? Je hao watu wa vijijini wanajua VX moja linaweza kuchimba visima sio chini ya sita wapate maji, huku wanaotembea na hizo VX wanamaji mpaka chooni, tena safi ya kuflash vinyesi? acheni kujifichia kwenye watu wasio na uelewa wa mambo.
 
Ninayo maswal machache,

1) Hitajia la katiba mpya nilakisiasa, au la kijamii? Ukijibu njoo na majibu vivid

2) Kwanini katiba mpya uwe Sasa? Kwa Nini haikuwa miaka5 iliyopita? Nini kimepelekea kuidai sasa?

3) Eleza hoja yenye mashiko katiba mpya itasaidiaje kuleta maendeleo ya Tanzania na watanzania? Eleza japo kwa mifano hai ni nchi zipi kwa kuwa na katiba(nzuri) zinamaendeleo kwa sababu ya katiba?

4) Unakubali au kukanusha juu ya ukwel kuwa katiba iliyopo inapangufu katika tume ya uchaguzi na si katiba yote? Ukanushaji au ukubali uwe na majib yaliyo na vielelezo hai.

5) Tuambie kwa faida au kwa hasara Nini kitatokea kama tusipokuwa na katiba nyingine kwa miaka 10 ijayo? Mwananchi alieko kule nyakahoze au mugumu Serengeti au kule songwe kijijini ataathirika vipi?

Nasubri majibu

Mr bonny
Haa haa :oops::oops::oops::oops:haa,

Ama kweli wewe ni "ignorant" wa mwisho...

Eti hivi "katiba inawezaje kutusaidia kutuletea maendeleo...!!"

Labda wewe bado ni mwanafunzi tena darasa la tatu maana ungekuwa hata kidato cha 1 au cha 2 ungekuwa unajua maana na umuhimu wa katiba kiuchumi, kisiasa na kijamii...

Rudi shuleni ukafundishwe upya...
 
Ndiyo maana tunapendekeza kwamba katiba itupe mamlaka sisi wananchi ya kuwaadibisha wanasiasa(Wabunge) ambao hawatendi wanachokiongea.
Umekosea...

Usiseme "....kuwaadabisha wanasiasa (wabunge) ambao hawatendi wanachokiongea..."

KATIBA yoyote hutoa muongozo (guidelines) kwa viongozi au taasisi za umma/serikali kutekeleza wajibu au majukumu ya siku kwa siku kwa umma (watu) sawasawa na katiba inavyotaka wafanye...

Ukisema "katiba ikupe uwezo/mamlaka ya kuwaadabisha viongozi au wanasiasa wasiotenda wasemayo", maana yake unataka turudi kwenye " Umagufulism" aliyekuwa hajali wala kufuata mwongozo wa katiba ilivyokuwa inamtaka afanye na badala yake akawa anataka watu watendee kazi mawazo na hisia zake na ndiyo maana mambo yakaharibika na yeye kujikuta anakufa kifo kibaya maana alikuwa "threat" kwa ustawi Wa jamii yote....!!

KATIBA BORA itapelekea viongozi na taasisi za umma kutekeleza wajibu vyema na kuleta ustawi bora na mpana kwa jamii yote...

KATIBA MBOVU husababisha kilio na huzuni kwa kila raia kwa sababu katiba hiyo inakuwa inawapa viongozi wa umma kukiuka na kuvunja haki za kiraia kama ilivyokuwa wakati wa uongozi wa Mwendazake John Pombe Magufuli...
 
Mkuu walao kiduchu umejib... Tatzo kubwa tu lipo kwenye maelezo na mifano.. hzo nchi zote ulizozitaja ukiwemo na Ghana... Maendeleo yal hayatokani na katiba.. ila inatokana na historia ya eneo...

Mfano...mapungufu yaliyopo yanaweza yasiwe takwa la kijamii ila la kisiasa.. ni mhim ukatambua kuwa jamii yote ya kinzania inaustarab wake.. kwa hyo haiwez ikawa ni sawa na wanasiasa...

Wanasiasa huwa wananuni ya kuongea one agenst 2... Wanachosema sicho wanachokitenda...
"Wanasiasa hawapendi SIASA ila wanapenda MADARAKA"Profesa Emeritus Isa Shivji
 
Muda wangu wa kuchangia nimeutumia kujibu maswali matano yanayoulizwa na wengi huko mtaani kuhusu Katiba (5 common questions).

1. Kwanini mchakato huu umeandaliwa na BAVICHA? Mnapigania Katiba ya nchi au ya Chadema?

#Jibu: Mchakato wowote wa katiba ni wa kisheria na kisiasa. Katiba ni jambo linalogusa watu wote, hivyo kila kundi lina haki ya kujadili. Vijana wa chama cha zamani, badala ya kuwaonea gere BAVICHA, nanyi mnaweza kuandaa kongamano lenu. Muhimu kila mtu apate nafasi ya kuamua muastakabali wa taifa letu.

2. Katiba mpya sio kipaumbele cha Rais, kwanini msiachane nayo?

#Jibu: Katiba sio mali ya Rais ni mali ya wananchi. Hivyo kama wananchi wanataka katiba mpya, Rais hawezi kuzuia kwa namna yoyote. Kama wananchi wakisema Katiba mpya ni kipaumbele chao, Rais atake asitake atalazimishwa (kwa sauti ya kimbunga Jobo).

3. Je, Katiba mpya ina umuhimu wowote?

#Jibu: Ndio. Itatuwezesha kupata tume huru ya uchaguzi, ambayo mchezaji wa timu pinzani hataweza kujigeuza refa kama ilivyo sasa. Itaimarisha uchumi kwa sababu wawekezaji wote wakubwa duniani hupenda kuinvest mitaji yao mahali penye stability ya kisiasa. Pamoja na faida nyingine nyingi (ambazo zimetajwa na wazungunzaji wengine) katiba mpya itamfunga "breki" Rais asiteue majambazi kama Sabaya na kuwapa ofisi za umma.

4. Kwanini tusifanye marekebisho kidogo ya Katiba iliyopo badala ya kudai mpya?

#Jibu: Katiba iliyopo imeshafanyiwa marekebisho mengi sana. Kati ya mwaka 1980 hadi 1995 ikifanyiwa marekebisho mara 13. Kama ni nguo basi imechakaa na ina viraka vingi sana. Kwahiyo badala ya kutafuta mahali pengine pa kuweka kiraka, ni bora tununue nguo mpya.

5. Kwanini Mchakato wa Katiba usisubiri kwanza ili tujenge uchumi kama alivyosema mama Samia?

#Jibu: Wakati akiongea na waandishi wa habari, Mama Samia alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, uchumi wa nchi uliporomoka kutoka 7.2% hadi 4.8%. Kumbuka kipindi hicho mchakato wa katiba ulikua umesimamishwa. Kama kuzuia Katiba mpya kunasaidia kujenga uchumi, basi ilitakiwa kipindi cha mwendazake uchumi uimarike kuliko wakati mwingine wowote, lakini haikua hivyo.

Mama anaupiga mwingi mnoo
 
Back
Top Bottom