Malisa ampinga kwa fact Polepole kuhusu CCM kuiletea maendeleo Moshi

Malisa ampinga kwa fact Polepole kuhusu CCM kuiletea maendeleo Moshi

malisa bana!Anazungumzia historia
Lazima amekubali maendeleo bila ya amani na utulivu si lolote,Malisa hakutoa Takwimu mangi aliacha shule ngapi na leo zipo ngapi
Kama barabara imejengwa na mangi 1940,lazima ifanyiwe ukarabati au kujengwa upya
miaka ya 80,malisa alikua hajazaliwa,ilikua kwenda moshi lazima ulale njiani kwa ajili ya kuvunja springi au kupasua tairi kwa ubovu wa barabara,malisa hajui kakuta lami watu wanaenda kwa corolla
Mkuu Malisa kaongelea barabara za Moshi, siyo za kutoka mikoa mingine kwenda Moshi. Hizo ulizosema ni kweli miaka ya 80 unatoka Dar saa kumi unaingia Moshi kesho yake saa mbili au tatu asubuhi. Halafu kumbuka kuwa hiyo miaka ambayo barabara zilikuwa mbovu ni serikali ya CCM ndiyo ilikuwa inatawala hadi leo.
 
Na gazeti watu walikuwa nalo kabisa[emoji3]
37274230_2102538933121358_1368044330425516032_n.jpg
 
hiyo mzee utumwa na ukoloni usinge kuwepo... moshi sijuikilimanjaro ingekuwa kama Denmark...
 
Kuhusu maendeleo naamini ni jukumu la serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake na sio swala na kujisifu ama kusifiwa ni jukumu la msingi hilo na ndio lengo kuu. Ni sawa na mzazi awe na watoto watano ila mmoja tu ndio kapata elimu inayostahili, hapo mzazi hawezi kusifiwa kuwa kamsomesha mwanae bali anafaa kulaumiwa kwwa kushindwa kuwapa elimu bora wanawe wanne!
 
hata kibondo kuna lami za kipindi cha utwana na kasulu... nao walikuwa na maendeleo... ukerewe walijenga ghorofa ndio tawala ya kwanza ya africa mashariki kuwa na ghorofa kabla hawajaja wajuaji na kuleta utwana au kuimarisha utwana... pia kulikuwa na viwanda aina ya mwijage... (small and medium industries)
 
kila kona kulikuwa na maendeleo kama ni nyuma 1960....
 
Huyu dogo ameanza kuchanganyikiwa. Moshi ilianza kuendelea zamani za pontio pilato kabla ya ujio wa Dr.Livingstone na Gavana Edward Twining.

Mwaka 1902 barabara zinazounganisha mitaa mbalimbali ya Moshi zilikuwa na lami, enzi hizo CCM haijazaliwa, mama yake TANU wala bibi yake TAA.

Mwaka 1895 Ikulu ya kwanza ya kisasa ya Mangi mkuu wa wachagga ilijengwa eneo la KDC Moshi. Ikulu hiyo hadi sasa ndiyo inayotumika kama Ikulu ndogo ya Rais akija mkoani Kilimanjaro.

Mwaka 1917 dola ya wachagga ilikuwa na mfumo rasmi wa serikali na baraza la mawaziri, ikiwa ni pamoja na ofisi na magari kwa watendaji waandamizi wakiwemo mawaziri. Ofisi za mawaziri ndio zinatumika leo kama ofisi za halmashauri ya wilaya ya Moshi.

Miaka 100 iliyopita Moshi kulikuwa na viwanda mbalimbali kikiwemo kiwanda kikubwa zaidi cha kubangua kahawa eneo la Afrika Mashariki. Mwaka 1940 dola ya wachagga tayari ilikuwa na gazeti lake (Komkya), lililokuwa likisomwa maeneo yote ya wachagga kuanzia Siha hadi Rongai. Gazeti hilo liliandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
-
Kufikia mwaka 1950 karibu kila kata au tarafa ilikuwa na shule ya sekondari, zahanati au kituo cha afya pamoja na kanisa la kisasa, kuanzia Siha mpaka Tarakea. Sio zote lakini nyingi zilikuwa na shule zilizojengwa na wamisionari miaka mingi sana iliyopita.

Wakati chakubanga na babu yake wanatembea kilomita 50 kwenda kuchoma chanjo ya tetekuwanga, wazee wa kichagga walikua wakipata huduma za afya kwenye vituo vya afya vya mission vilivyopo kwenye kata/tarafa zao.

Leo mtu mmoja pengine kwa sababu ya kukosa chanjo ya pepopunda anaropoka kwamba maendeleo ya Moshi yameletwa na CCM? What a shame.!!
-
Kimsingi CCM na serikali yake zimezorotesha maradufu maendeleo ya Moshi kuliko wakati mwingine wowote katika historia. Moshi ya wakati ule (kama dola yenye mamlaka kamili), na Moshi ya leo (kama wilaya) ni vitu viwili tofauti. Moshi ingeachwa kuwa dola huru kama ilivyokuwa zamani, ingekuwa na maendeleo maradufu kuliko leo.

Halafu kama kweli CCM inaleta maendeleo, mbona kuna mikoa haijawahi kuchagua upinzani na bado haina maendeleo? Kwanini maendeleo hayo CCM isipeleke kwenye ngome zake? Next time mwambieni kabla hajabwatuka ajifunze historia kdg.!!!!!!!!!

Source instagram:Malisa_gj
Kuna wakati na nashindwa kuelewa, hivi cheo cha UENEZIi CCM kina nini? Cheo hicho kinabadili sana binadamu, tangu enzi za Mhe. Mapuri, Nape, Mwigulu na sasa Polepole! Kuna wakati unajiuliza " mbona huyu alikuwa mzima jana, amekuwaje? Na ghafula anapoondolewa kwenye nafasi hii, unapata mshangao mwingine, mbona mtu huyu alikuwa mgonjwa mahututi jana, ameponywa na nini? Wanaccm tusaidieni.
 
Conspiracy theories zipo nyingi sana za kuwarudisha nyuma kimaendeleo, kila awamu ilikuwa na mkakati wake. Awamu ya kwanza ilivunja nguvu ya chama cha ushirika KNCU, awamu ya pili ikakazia hapo, awamu ya tatu ikawavunjia biashara zao Shekilango na Sam Nujoma road na kauli mbiu ikawa kila anayetaka kuneemeka lazima ajiunge na CCM(Sumaye), awamu ya nne ikaanza kuwapunguza kujiunga na vyuo vikuu na ajira serikalini, awamu ya tano ndio usiseme kabisa.. vunja kimara yote mpaka mbezi bila fidia, ondoa kwenye teuzi zote, kataa pendekezo lolote la kuifanya Moshi jiji, kadiria kodi kubwa kwa wafanyabiashara na mengineyo mengi yaliyo chini ya carpet yakitekelezwa kimya kimya. Lakini kwa msaada wa Muumba watavuka, kwani huwa hawaachi kutoa zaka zao (fungu la kumi) kama walivyoagizwa.
huu ndo ukweli
 
Mkuu Malisa kaongelea barabara za Moshi, siyo za kutoka mikoa mingine kwenda Moshi. Hizo ulizosema ni kweli miaka ya 80 unatoka Dar saa kumi unaingia Moshi kesho yake saa mbili au tatu asubuhi. Halafu kumbuka kuwa hiyo miaka ambayo barabara zilikuwa mbovu ni serikali ya CCM ndiyo ilikuwa inatawala hadi leo.
maendeleo yanaletwa na barabara,kama barabra za kuelekea moshi zingeendelea kuwa mbovu,tusingekua na moshi hii ya leo,halafu mnajitoa ufahamu tokea uhuru moshi ipo chini ya serikali ya chama hiki hili haikwepeki hiyo
 
malisa bana!Anazungumzia historia
Lazima amekubali maendeleo bila ya amani na utulivu si lolote,Malisa hakutoa Takwimu mangi aliacha shule ngapi na leo zipo ngapi
Kama barabara imejengwa na mangi 1940,lazima ifanyiwe ukarabati au kujengwa upya
miaka ya 80,malisa alikua hajazaliwa,ilikua kwenda moshi lazima ulale njiani kwa ajili ya kuvunja springi au kupasua tairi kwa ubovu wa barabara,malisa hajui kakuta lami watu wanaenda kwa corolla
Wewe ndio ulete hizo takwimu sasa sio porojo kama Bosi wako Chakubanga.
 
Wameendelea wapi?
Labda katika wizi. Jamaa katika wizi wapo vizuri sana. Kesi ya Billionaire Msuya, ndio yale yale yanayotokea katika sectors nyingi apa Tanzania, jamaa wapigaji sana
Msuya aliiba nini wewe Kiraka?
 
Malisa, maendeleo ya moshi ni kweli yalikuwa zaidi ya milia mingine, NA yaliketwa sio kwa juhudi ya mangi na wachaga pekee yao, bali yaliketwa NA mkoloni na makanisa, ambayo walikuwa wakifanya mambo kwa maslahi yao. Waingereza na makanisa walichagua makabila kadha hapa nchini ili kuyatumia ili waweze kuendelea kututawala kupitia hayo makabila, walimaji wakubwa wa kahawa walikuwa wazungu, wakisaidiwa kuliendeleza zao hilo NA wachaga , wameru na WaArusha katika mikoa ya Kili NA Arusha.

Ukweli ni kuwa mangi na viongozi wengi wakichaga walikuwa vibaraka wa wakolini . Ilifikia wakati hata Mangi alitaka muingereza alitenge JImbo la Moshi NA kuwa nchi tofauti NA Iweze kujiendesha chini ya himaya ya Uingereza NA Malkia.

Maendeleo ya Moshi happened kipendeleo kwenye mgongo wa Tanganyika
Kwa hiyo Wakoloni walikuwa Moshi pekee,vipi na hiyo kahawa mbona ipo Kagera,Mbinga,Kigoma na sehemu zingine huko napo maendekeo yao yapoje?
 
Back
Top Bottom