Malipo ya waamuzi katika ligi kubwa za ulaya

Wakina ramadhan kayoko wanakunjaa MKWANJAA kokotee Cha msingi upande dau kubwa kuliko mwenzako akupee matokeo..

Ukisema ategemee malipo ya TFF atachelewa Sana kupataa maendeleo....
Kwa kweli
 
Tanzania mimi hupenda kumwa refarii moja anaitwa Tatu; ni binti mdogo lakini yuko sharp sana. Sijui yeye analipwaje lakini hunikosha sana anapokuwa anachezesha mpira ingawa mara chache chache amekuwa anafanya makosa madogomdogo.
Tatu Malogo??
 
Rama kayoko naskia ni Muajiriwa tasisi moja hiv ya serikali.
Urefa ni kama mazoezi tu na kupata pesa ya maji kupoza koo.
 
Haya leo tuangazie namna gani marefarii katika ligibza wenzetu wanavyolipwa. Sijajua kwa huku kwetu wanalipwaje lakini kwa wenzetu malipo yao ni kila mechi.

Katika ligi kuu ya Uingereza, mwamuzi hulipwa Euro 1300 ambayo ukiibadilisha kwa pesa ya madafu ni sawa na Shilingi Milioni 3,302,550 kwa mechi moja tu.

Kule ligi kuu ya Ureno, mwamuzi analamba Euro 1500 kwa mechi moja ambayo ni sawa na Tshs. Milioni 3,811,197.

Kwa upande wa Ligue 1 ambayo ni ligi kuu ya Ufaransa, mwamuzi huwa anakunja Euro 2900 kwa mechi moja tu ambayo ukiileta kwa pesa zetu ni sawa na Milioni 7,368,178.

Ligi Kuu ya Italia maarufu kama Serie A nayo hawapo nyuma, refarii hulipwa Euro 3400 ambazo ni sawa na Tshs. Milioni 8,637,996 kwa mechi moja tu.

Kule Bundesliga, kwa mechi moja tu, mwamuzi huchukua Euro 3600 ambazo ni sawa na Tshs. milioni 9,145,439.

Tukimalizia na Laliga, mwamuzi huwa analamba Euro 4200 kwa mchezo mmoja tu ambazo ni sawa na Tshs. Milioni 10, 669,777.

Kwa kuhitimisha, EPL ligi pendwa waamuzi wake wanalipwa kiduchu kulinganisha na ligi za nchi nyingine, lakini pia waamuzi wa ligi za wenzetu wana kazi za ziada.

Natamani nifahamu waamuzi wetu akina Kayoko wao wanakunja shilingi ngapi kwa mechi moja.
Mechi za ligi kuu ni laki4..
Mechi za championship laki 2.5
Mechi za first league laki 1.5..

Lensmen wao ni 75% ya refa wa Kati..pia Kuna viposho mechi ikiwa imejaza uwanja ,,ndio maana unaona wenye connection wanasafiri na Simba ,Yanga kila siku example kayoko,Sasii,,Jonesia,Arajiga,kambuzi,mwinyichui ,Mwinyimkuu,mdoe na yule dada mnyaturu
 
Natamani nifahamu waamuzi wetu akina Kayoko wao wanakunja shilingi ngapi kwa mechi moja.

Wakina Kayoko wanakunja ngumi

Niliwahi kusikia jamaa mmoja akisema kuwa wanalipwa kiasi kisichozidi laki 3. Malipo ya mchezo, gharama za accomodation usafiri humohumo.
 
Back
Top Bottom