Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
MWENYEKITI wa Kamati ya Waamuzi, Nassor Hamduni, amewaambia wanachama na mashabiki wa Simba kuwa wamesikia kilio chao dhidi ya mwamuzi Ramadhani Kayoko na jambo hilo litakwenda kufanyiwa kazi na Kamati na Nidhamu na anaweza kuadhibiwa iwapo itathibitika kuwa alikuwa na mapungufu kwenye uamuzi wake.
Ijumaa iliyopita baada ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Azam FC kumalizika, mashabiki wa 'Wekundu wa Msimbazi' hao walifanya maandamano ndani ya uwanja wa CCM Kirumba, wakimshutumu mwamuzi huyo kwa kutochezesha mechi hiyo kwa haki, wakidai aliwanyima haki kwenye baadhi ya matukio na kuwafanya kutoka sare ya bao 1-1.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Hamduni aliwaomba radhi mashabiki na wadau wote waliokwazwa kwa njia moja ama nyingine kutokana na ufanyaji kazi wa waamuzi katika mechi za hivi karibuni ambazo zimeonekana kuwa na malalamiko mengi.
"Tumeyasikia, tunaheshimu kauli za mashabiki kwa sababu hao ndio wadau wetu wa soka na waswahili wanasema ndiyo wanaotuweka mjini, tumesikia na naomba kuwaeleza.
"Suala la kukataa mwamuzi si la mashabiki, viongozi au kamati yetu waamuzi, bali lipo kwenye kamati maalum ambayo inachunguza mwenendo wa waamuzi, na kama Kayoko ataonekana ana matatizo kwenye mechi aliyochezesha atachukuliwa hatua na si yeye tu, yeyote yule ambaye itabainika amevurunda, tunaomba mashabiki watulie wasubiri Kamati ya Nidhamu ambayo imeshajua hayo, watachukua hatua na sisi Kamati ya Waamuzi ikitufikia tutaridhika na maamuzi watakayochukua," alisema.