Nimeshtuka sana leo asubuhi, baada ya kusikia taarifa katika kituo cha RFA kipindi cha MATUKIO -michezo kuwa
Jamal Malinzi Rais wa TFF atatoa pesa zake mfukoni kufidia malipo ya kukatisha mkataba wa Kocha wa timu ya taifa ndugu Poulsen.
Hapa ndo naanza kuona harufu ya ufisadi hapa na kwa sababuJamal Malinzi yuko humu basi ntamuomba aje kutoa ufafanuzi wa yafuatayo.
- Ukiwa kama Rais wa TFF, Je shirikisho lina mgogoro wa kifedha kiasi kwamba haliwezi kabisa kulipa fidia hiyo?
- Je huoni kwamba unatujemgea wasiwasi kua unajenga mazingira ya kujilipa hapo baadaye, tena zaidi kwa njia zisizo halali?
- Je hii sio njia ya kuwa intimidate viongozi wengine ili waogope kuhoji baadhi ya matumizi yako ya pesa kwa kuwa tu umeanza na visingizio vya kutumia pesa zako Binafsi.
- Je huoni kuwa hii ni conflict of interest?? Kwa nini utumie Pesa yako tena bila kuutangazia uma ni kiasi gani wakati shirikisho lina uwezo wa kulipa pia
- kama kweli una nia hiyo thabiti, kwa nini msiwatangazie wana michezo kiasi halisi unachojitolea wewe mfukoni mwako... na kiasi anachodai Poulsen
Ndugu
Jamal Malinzi, kwa watu wanaofanya "critical thinking" hii ni njia mojawapo inayotumiwa ni viongozi kujenga mazingira ya UFISADI hapo baadaye.
Tunakumbuka miaka ta tisini "CCM" iishindwa kuwalipa watumishi wake mikoani kwa takribani miezi sita, mpaka ROSTAM AZIZ alipojitolea pesa zake mfukoni na kuipa CCM ili iwalipe watumishi (nilikua pia CCM wakati huo so najua hili) lakini wote tunajua jinsi gani alijilipa hizo pesa na zaidi. mifano ya namna hii ni mingi sana.
Tupe hoja zako, unajipambanuaje katika hili??la sivyo ni kujenga mazingira ya ufisadi tuuu.