Mzigo wa Mjerumani upo tena wakutosha Tz. Ndo maana na serikali wametunga sheria inayoitwa Antiquities Act...aka mambo ya kale. Mininashimo langu karibuni nazoa mzigo. Mnategemea nitatangaza? Najua mtanisema nimejiunga Freemasons. Mamilionea wengi TZ wamepiga huo mzigo asieamini aendelee kutoamini. Tena mi chimbo langu halina muujiza wala nini... walitumia akili kubwa sana ikiwemo kutengeneza chumba ndani ya jabari chini ya aridhi mlimani.
na hadithi alikufundisha nani?Hadithi hizi hazikuanza hivi karibuni! Huko Tukuyu, Mbeya kuna ziwa linaitwa Kibisi ambalo halina sehemu inayooneka kwa macho kama inaingaza maji ziwani humo au kutoa ambalo Wajerumani baada ya kushindwa vita ya pili ya dunia walitupa hazina kubwa ya mali ambayo upatikanaji wake ni mgumu kwani kila anayezamia na kutaka kuitoa anakumbana na mauzauza mengi ikiwemo kutokewa na joka kubwa linalotisha!
Inasemekana kuna wazungu walijaribu kuitoa hazina hiyo wakashindwa baada ya mmoja wao kuzamia huku akiwa amefungwa vifaa maalumu pamoja na minyororo ya kufungia masanduku ya chuma yanayosemekana yapo chini ya ziwa. Mzungu huyo hakurudi juu wala masanduku na kupotelea chini ya ziwa na kuwafanya wenzake kuondoka kwa majonzi makubwa badala ya furaha!
Haya mambo yapo ni kweli kuna mali ziliachwa na Wajerumani mara baada ya kushindwa kwenye vita kuu ya I ya Dunia. Ila hakuna hata mmoja anaye weza kuprove beyond dought kwamba ameona that is why kila mtu anasema aliambiwa.
Ila mimi kwa macho yangu nimeshuhudia shimo juu ya mlima na ni kubwa sana ila alichimba nani sijui na kilichopo napo sijui.
Kwenye ishu ya Uchawi inaweza kuwa hawakutumia uchawi ila kwa akili walizo tumia ikiwemo kuchimba mashimo na kujenga vyumba ndo kunafanya watu waamini kwamba ni uchawi.
Hizi imani za kishirikina,wapo watu wametoa kafara hadi za watu ili kupata mali za kusadikika.Ipo dhana ya kwamba wajerumani wakati wapokuwa wakikurupushwa na waingereza tanganyika baadhi ya mali zao walishindwa kuondoka nazo,hivyo inasadikika mali nyingi walidhihifadhi chini ya ardhi kwa utaratibu maalumu ambao ktk mazingira ya kawaida si rahisi kuzitoa au kuzihamisha.
Inasadikika mali hizo zitakaa hapo zilipo mpk wao wenyewe watakapoamua kuzifuata,pia inasadikika walitumia "runic rituals"ktk kudhihifadha utaratibu unaoendana na utoaji kafara binadamu.
Yapo maeneo mbalimbali ambako inasadikika masanduku haya yalihifadhiwa, baadhi ya maeneo hayo ni Tanga (usambara),Morogoro,Singida,Lindi,Kilimanjaro na nk.
Yeyote mwenye taarifa zaidi aweza kutujuza zaidi juu ya suala hili,kwani maeneo haya yatakapo julikana vema huenda yakawa chanzo kizuri cha utalii kutokana na historia yake kusisimua.
Nawasilisha.
bora uamini kuliko kutoamini kabisa !!!ila tutarudi punde kutoa ushuhuda ila hamkawii kusema oooh flani katoa kafara ,au freemason au muuza unga kama wachangiaji wengine wanavyosema,penye nia pana njia hizi ni mali zetu lazima tuzifukue,ila si kazi rahisi hata kidogo.
mkuu hizi habari kweli ila wale jamaa wameroga sana,unaweza ukafuatilia ukikaribia kufanikiwa unaghairi kumaliizia kazi au mkagombana wenyewe kwa wenyewe ,wamepumbaza sana ila amin tu wazungu wachawi sana.
Mpaka muda huu hapa mkoani kwetu kuna jamaa wanachimba kwa kutumia gleda wakifuatilia mali za kale za Wajerumani.
Leo wiki ya tatu na inasemekana kuna mzigo wa dhahabu wa kg 1000 gleda linaunguruma masaa 24
Huku kwetu kuna mzee mmoja alishachimba hzo mali tangu akiwa kijana hadi sas ana miaka 65 bado hajafanikiwa kufikia masanduku hayo, hata leo jioni alitoka huko kuchimba, nilijaribu kumdadis yule mzee anasema kwamba mali hxo zipo shida ni kwamba zimezindikwa hata waganga wa huku africa hawawzi kuzitoa hadi wajerumani wenyewe.
Ila pamoja kuelewa hvyo mzee wa watu bado tu anakomaa na anasema bado anamatumaini kuwa siku moja Mungu atamsaidia ataxifikia hzo mali, binafsi nafaham maeneo mengi yanayosadikiwa kuwepo kwa mali hzo so mwenye kuhitaji aniPM nimpe ramani. kuna sehemu palikuwa na gereza la wajerumani zamani, Babu yake baba aliwahi kufungwa pale na mjerumani kisa alikuwa na urafiki na mwingereza, kipindi hicho walichimba maandaki makubwa hapo lkn hawakujua matumizi ya maandaki yale, sasa hapo ndo unaambiwa mali zimejaa na zinahitaji nguvu kubwa kuziondoa.