Mali za Kapteni Komba kupigwa mnada na CRDB

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
Benki ya CRDB iko njiani kufilisi mali za mheshimiwa Kapteni John Komba kutokana na kushindwa kulipa deni . Ikiwepo shule zake kupigwa mnana.

Jumla ya deni lote ni shilingi bilioni moja za kitanzania.

===================================


Chanzo;Raia Mwema
 
Benki ya crdb inatarajia kupiga mnada mali za John Komba anayedaiwa zaidi ya tsh 1 bilioni ndani ya siku 7.Source magazeti ya leo.Wakubwa wa ccm wanaifaidi hii nchi kwa kila sekta wananyonya tuu
 
Front page lead story Rais Mwema...bila shaka atakuwa tayari msituni akijiandaa kuja kupambana na 'wadeni' wake.

Watamtambua kwa kumdai mwanajeshi yule ohoooo.

Akishindwa hivyo bila shaka atawatungia nyimbo...wataimbiwa kwaya na kusahau kudai deni.
 
Benki ya crdb inatarajia kupiga mnada mali za John Komba anayedaiwa zaidi ya tsh 1 bilioni ndani ya siku 7.Source magazeti ya leo.Wakubwa wa ccm wanaifaidi hii nchi kwa kila sekta wananyonya tuu

Bado sakata la picha za uchafu kwenye mtandao yamekuja mengine tena. Kweli dunia tambala bovu
 
ni leo kwenye vyombo vya habari tumeskia kwamba mali za mmbunge Kapteni John Komba zitapigwa mnada kwa kudaiwa na benk ya crdb zaidi ya billion moja fedha ambazo ameshindwa kurudisha. Swali langu ni je kwa nini mtu ukope zaidi ya uwezo wako wa kurejesha? Jamani hili liwe fundisho kwetu sisi. Ni kweli saa nyingine tunakuwa na tamaa ya kukopa na kuanzisha biashara ili kufanikiwa haraka. Ila kaa ukijua kuwa biashara hata siku moja haitabiriki
 
Ndugu huyo kama ni kufaidi kafaidi kihalali, maana amekopa. Na kama alikopa basi anatakiwa kulipa, kama alishindwa kulipa basi taratibu za kupiga minada na kufilisi zinafuata.
Benki ya crdb inatarajia
kupiga mnada mali za John Komba anayedaiwa zaidi ya tsh 1 bilioni ndani
ya siku 7.Source magazeti ya leo.Wakubwa wa ccm wanaifaidi hii nchi kwa
kila sekta wananyonya tuu
 
Mbunge wa Mbinga Bwn.Komba ameendelea kupatwa na majanga baada ya kuelezwa kuwa mali zake kupigwa mnada kulipa deni la mabilioni ktk benki CRDB.Deni hili ni deni la msingi pamoja na riba.
 
mkuu si wote wanaokopa wamekopa kupita uwezo wao wa kulipa,

mambo ya mikopo ndugu yangu yana misukosuko mingi sana katika matumizi yake,

kuna watu wanakopa halafu wakija sokoni kufanya tranaction, unakuta thamani ya pesa imeshuka, hivyo ukienda kubadili pesa huko nje, unatoa pesa nyiingi kununua vitu vichache sana! kumbuka benko haina habari na hilo kabisa!

Mpaka sasa kumbuka hatuoni juhudi za mkuu wa nchi kupandisha thamani ya pesa japo kasoma economics, bado mambo ni mazito sana katika nyanja za uchumi ndani ya nchi yetu ndugu!

Hapo wewe umemjua komba tu, kuna mamia ya raia wamechanganyikiwa kwa kufanyiwa hivi na mambenki!
 
Komba alifanya fitna ili band ya vijana jazz ife ili apate tenda zote za ccm...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…