Mali yaahirisha Uchaguzi Mkuu wa Mwakani ili kupata Katiba Mpya kwanza

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Utawala wa kijeshi nchini Mali umetangaza hii leo kuwa utaahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Februari mwakani.

Uchaguzi huo ulilenga kuwarejesha madarakani viongozi wa kiraia katika taifa hilo la Afrika Magharibi linalokumbwa na uasi wa makundi ya kigaidi.

Msemaji wa serikali ya Bamako Abdoulaye Maiga, amewaambia waandishi wa habari kuwa duru mbili za uchaguzi zilipangwa kufanyika Februari 4 na 18, 2024, zitaahirishwa kidogo kutokana na sababu za kiufundi, ambazo zinahusiana na suala la kupitishwa kwa katiba mpya mwaka huu na mapitio ya orodha ya wapiga kura.

Aidha Maiga ameelezea pia mzozo walionao na kampuni ya Ufaransa ya Idemia, ambayo utawala wa kijeshi umesema inahusika na mchakato wa kuhesabu watu.

Tarehe mpya za uchaguzi wa rais nchini Mali zitafahamishwa hapo baadaye.

DW Swahili
 
Wa kwetu wa Jamhuri ya Stupid land sijui wanafeli wapi.

Washaridhika na wakuu wao kupewa ma VX na wa chini kupewa pombe za bure kwenye mabwalo yao wanaona maisha washayapatia.

Jamhuri ya Stupid land haitokaa sawa mpaka kinuke kidogo, watawala wamejibweteka sana.
 
Subiri waweke mambo yao vizuri, wafanye marekebisho ili mkuu wa jeshi agombee urais, ashinde, akae madarakani hadi mwisho wa siku zake au hadi mapinduzi mengine 🤣
 
"The gravest mistake that will never be pardoned is to allow a black man to rule the country something that will set up a foundation to ruin the country for ever." Pieter Bother, the former apartheid South African President.

Today we stand as witnesses to see what is happening in this potentially rich and affluent but impoverished continent where majority of inhabitants struggle to put three meals on the table per day and where almost two thirds of the people live below two dollars a day.
 
Back
Top Bottom