Chloe 92
JF-Expert Member
- Aug 7, 2018
- 568
- 816
Kuna sehem nilienda ile nafika tu mtoto wa miaka 7 ananiuliza "unaondoka lini" mama ake kasikia akacheka tu, mda wa kula ile nachukua chakula akaropoka " wewee unamaliza chakula " na mama ake kimya nilijiskia vibaya nikanyamaza nikamaliza kilichonipeleka nkasepa zangu.Nilijiuliza mtoto anawezaje ongea vile kwa mgeni na mzazi umenyamaza tu.Hom tuliwahi kuishi na watu baki tu ila hakuna aliyewahi kuinua mdomo kumwambia mtu kuwa Ondoka hapa sio kwenu wala kukataa kutumwa na wale tuliokuwa tunaishi nao.
Niliwahi kuambiwa na mtoto wa baba mdogo kuwa ung'ang'ania na wewe upewe, kwani hapa kwenu, si uende kwenu. Nilikwenda kwao xmas moja hivi nikiwa mdogo, roho iliniuma mno siku hiyo, mama mtu alisikia vizuri yale maneno ila akakausha tu