Malezi ya wazazi wa siku hizi na dosari zake!

Hahahahahaha hongera kwa maza ako

Nakumbuka bi mkubwa ilikuwa akipika kitu sikipendi nikisusa tu kosaaa nachezea kipigo nakalishwa kwenye sahani na lazima Nile,,,,, ila Nampa pongezi sababu mpaka sasa hakuna mwenye jeuri ya kuinua bakuli lake kumjibu bi mkubwa akiongea na tena tukimvuruga kama tupo karibu nae vibao tunachapwa
Hiyo ya kususa nilishawahi fanya hivyo,Maza alinipa kipigo cha hatari na Mzee alivyorudi akapewa taarifa na yeye akanipa kisago heavy na usiku nikambiwa si umesusa sasa hakuna kula kalale,we tokea siku iyo sijawahi jaribu fanya huo ujinga tena
 
Wataendelea kuharibika Kama wanaume wataendelea kuwa deadbeat dads.
 
Hiyo ya kususa nilishawahi fanya hivyo,Maza alinipa kipigo cha hatari na Mzee alivyorudi akapewa taarifa na yeye akanipa kisago heavy na usiku nikambiwa si umesusa sasa hakuna kula kalale,we tokea siku iyo sijawahi jaribu fanya huo ujinga tena
Umenikumbusha home tulikuwa tunakaa na mtoto wa ma mkubwa... Kipindi ye yupo la saba mimi la tano.. Basi baba akatununulia mabegi ya shule, mie bwana nikaanza kulia langu baya sista yule wamempendelea lake zuri, Maza akaniangaliaaa kisha akakausha tu, wakapika mchana wakala na jioni nikanyimwa tena chakula.. Hiyo siku nilikula kikeki kimoja tu usiku, toka siku hiyo tukinunuliwa vitu silalamiki... Yaani ni unakomeshwa
 
Kwenye hili tunakosea sana na ndomana dunia ya sasa imejaa binadamu wenye less emotion,watoto wenyewe wanalelewa na mahousegirl unategemea nini
 
Mi huwa sina mazoea na mtoto yoyote. Ukileta ujinga nakuchapa na Mama yako hanifanyi kitu
 
na wale watoto ambao mama padre na mama ndo muelimishaji wa biblia lakini watoto wao kutwa wamo magetoni inakuwaje. ni mtoto mwenewe ajielewe tu
 
kuna siku nilikuwa nasikiliza mafundisho ya mchungaji Mitimingi. somo lilihusu malezi alisema nanukuu "misuli ya nidhamu inatoka kwa baba"

waefeso 6:4
 
Kabisa ukiwa unafanywa vile unaona anakuonea

... Kuna tabia maza alikuwa nayo ukimuaga unaenda sehemu ukachelewa kurudi anasubiri saa moja usiku Ile anakufukuza nyumbani na lazima uondoke.... Basi nilikuwa nakaa na dadangu wa ma mkubwa... Alikuwa anatutimua saa moja usiku tunaanza safari ya kwenda kwa Bibi yetu hapo ni mwendo wa lisaa... Njiani napita nalia tu mpaka nafika yaani kama nakaa na mama wa kambo vile kumbe mama mzazi.... Tukifika kwa Bibi tunakaa siku mbili baba anatufuata tunarudi nyumbani
ni balaa, huyo alikua kama mjeshi aisee. Ila kuna wakati mzazi usipokua kama mjeshi basi watoto ni lazima wakusumbue na waharibike aisee.
 
nakumbuka kuna mama mmoja alinipa mtoto wake nimpakate yeye akawa amesimama mbele yetu mtoto akaanza kumshika kalio mi nikamtoa mkono wake haraka kakaniangalia kwa hasira akarudisha mkono pale huku anapapasa kabisa yule mama akageuka akamuangalia mtoto wake halafu akageuka mbele huku mtoto akiendelea kuchezea tako la mama yake mmama wa pembeni yangu ndo akaanza kujibizana na yule mmama ikawa gumzo kwenye gari watu wote kimya kusikiliza ugomvi
Mi nikamuweka mtoto kwenye siti niliyokaa nikashuka tu kituo kilichofuata
Duh, ni hatari sana hii
 
Back
Top Bottom