Malezi ya wazazi wa siku hizi na dosari zake!

Kuna vitoto vya mpangaji wetu vilikuja havina adabu ..vinamjibisha mama yao..vinakauli chafu..yani tabia za ovyo ovyo..nikawashikisha adabu mwanzo mama yao alikua anakasirika nikasema kasirika utanishukuru baadae..sasa hivi vimenyooka heshima na adabu..yani hata kusalimia mkubwa kwao ilikua shida siku hizi vikitoka shule hata kama nipo ndani vinagonga mlango shikamoo mamdogo c nawaambia namna hiyo..hadi baba yao anashangaa mabadiliko ya watoto wake
Safii watoto wawe hivyo sio mitoto utadhani imeokotwa balaa tupu hayajui mkubwa wala mdogo.... Hasa watoto wa ukanda wa pwani eeeeeeh hehehehehehhe ni vurugu balaa timbwili wamama Wana matusi si kitoto.... Mtoto nae anakopi kwa mama... Yani katoto kadogo kanatukana matusi mtu mzima huyawezi
 
Hahahahaha mama zetu walijua kutulea jamani..kipindi Niko mtoto nilikua naona ni uonevu but now namshukuru kwa malezi Yale ..naweza ishi popote pasipo kulalama
Kabisa ukiwa unafanywa vile unaona anakuonea

... Kuna tabia maza alikuwa nayo ukimuaga unaenda sehemu ukachelewa kurudi anasubiri saa moja usiku Ile anakufukuza nyumbani na lazima uondoke.... Basi nilikuwa nakaa na dadangu wa ma mkubwa... Alikuwa anatutimua saa moja usiku tunaanza safari ya kwenda kwa Bibi yetu hapo ni mwendo wa lisaa... Njiani napita nalia tu mpaka nafika yaani kama nakaa na mama wa kambo vile kumbe mama mzazi.... Tukifika kwa Bibi tunakaa siku mbili baba anatufuata tunarudi nyumbani
 
Hahahahahahaha safiii ndo dawa yao wenyewe si wanamchekea toto gani lina domo chafu kama choo cha stendi
Hahahahahahaaa choo cha stand haswa.

Na baba ake ndie chanzo cha tabia chafu za kale katoto..mama ake amepigwa marufuku kumuadhibu akosapo..mama ake hana kauli kwa kale katoto

Mburaaaa nikuzae mwenyewe na bado unipande kichwani..haitakuja tokea
 
Safii watoto wawe hivyo sio mitoto utadhani imeokotwa balaa tupu hayajui mkubwa wala mdogo.... Hasa watoto wa ukanda wa pwani eeeeeeh hehehehehehhe ni vurugu balaa timbwili wamama Wana matusi si kitoto.... Mtoto nae anakopi kwa mama... Yani katoto kadogo kanatukana matusi mtu mzima huyawezi
Uwiii tena ukanda wa pwani ndio usiseme ..ukipiga mtoto wake utamwagiwa mvua ya matusi hadi ujute..utaambiwa zaa wako huujui uchungu wake..nakamata nafinya napiga kuzaa hata chura anazaa..siwezi ona mtoto anafanya ujinga nikakaa kimya
 
Kabisa ukiwa unafanywa vile unaona anakuonea

... Kuna tabia maza alikuwa nayo ukimuaga unaenda sehemu ukachelewa kurudi anasubiri saa moja usiku Ile anakufukuza nyumbani na lazima uondoke.... Basi nilikuwa nakaa na dadangu wa ma mkubwa... Alikuwa anatutimua saa moja usiku tunaanza safari ya kwenda kwa Bibi yetu hapo ni mwendo wa lisaa... Njiani napita nalia tu mpaka nafika yaani kama nakaa na mama wa kambo vile kumbe mama mzazi.... Tukifika kwa Bibi tunakaa siku mbili baba anatufuata tunarudi nyumbani
Haahahahaha bimkubwa alikua hatari kufukuzwa tena nyumbani!! ..bimkubwa wangu ilikua ukifanya ivyo anakua kimya kama hakuna kilichotokea..anaacha unaoga unakula unajuaa soo limeisha..unataka kulala sasa pale ndipo mahojiano na kipigo kinapoanza chumbani mtu mbili tu..baba anaambiwa naomba ukae pembeni sitaki kuingiliwa ninapoadhibu mwanangu..utapewa kipigo na ole wako siku inayofuata unune au ususe kula..ole wako
 
Ni kweli mtoto ukimlea vibaya hawezi kukaa na mtu.... Kuna dogo yupo form two ni wa kike anakaa na mamake utadhani mke mwenzie jamani mama mtu nae utakuta anaenda kulalamika kwa WiFi yake " mwanangu hanisikilizi nikimtuma hataki" eeeiiiish sasa unajiuliza yeye mwenyew hamuwezi huyo WiFi atamuweza?
Mimi nilishawaambia kama utaona mwanao namnyanyasa...kaa nae milele mpaka...kaa nae mwenyewe...sitaki toto lisilo na adabu...
 
Hii mada tam sana matoto hayasikii mi kuna mmoja niliwah mkataza kitu akanijibu unanikataza kwani lazima af yuko na vitoto vyenzake nika kaa kimya maana niliudhika sana aisee wazazi wa kike wanaharibu sana watoto
Jumapili iliyopita nilihudhuria kwenye msiba wa ndugu wa rafiki yangu, Miongoni mwa waombolezaji alikua dada mmoja mwenye miaka kama 26-30, alikuwa na mwanae wa kama miaka minne hivi

Sijui ilikuaje lakini mara yule dogo akaanza kulia na kisha kumvurumishia ngumi na mateke mama yake. Mama mtu akabakia kusema tu " Brian stooop banaa". Mpaka mama mmoja alipokuja akamwambia hiyo ni aibu mwanao hata kama ni mdogo unamuachia akupige hivyo hebu ingieni kule chumbani mkabembelezane

Watoto wote wadogo sio ajabu kuwa na utundu lakini utundu mwingine nahisi kama ni wa kukosa adabu na unaendekezwa na wazazi hasa wakike.

Nimewahi kushuhudia mtoto wa chini ya miaka mitano akiipasua simu ya mama yake kwa makusudi kwa kuibamiza chini na mama mtu anasema "mmmh leo sijui kakasirika nini huyu!" halafu akaanza kumbembeleza!

Kuna mtoto wa shangazi yangu aliwahi kumtupia usoni mfuko wa chips mama yake baada ya kugundua alicholetewa sio alichomuagiza wakati anaenda kazini!

Hapo kwenye msiba baada ya tukio la huyo mama na mtoto watu walisema mengi sana kuhusu dosari za kimalezi za wazazi wa kike wa siku hizi. Kuna mzee mmoja akawa anasema dunia inavokwenda huko baadae hayo mapenzi ya mama na mwana yanaweza kufikia hatua ya aibu zaidi hata mama "kumuonjesha" mwanae atakapo balehe

Sina hakika kama haya mambo ya kudekeza watoto kiasi hiki yalikuwepo zamani ila nahisi mengine ni kuwapotosha watoto kwa kuwapa malezi yasiyofaa.
 
Kuna vitoto vya mpangaji wetu vilikuja havina adabu ..vinamjibisha mama yao..vinakauli chafu..yani tabia za ovyo ovyo..nikawashikisha adabu mwanzo mama yao alikua anakasirika nikasema kasirika utanishukuru baadae..sasa hivi vimenyooka heshima na adabu..yani hata kusalimia mkubwa kwao ilikua shida siku hizi vikitoka shule hata kama nipo ndani vinagonga mlango shikamoo mamdogo c nawaambia namna hiyo..hadi baba yao anashangaa mabadiliko ya watoto wake
Alafu kuna kuku mmoja anasema malezi ni ya baba pia...
 
Uwiii tena ukanda wa pwani ndio usiseme ..ukipiga mtoto wake utamwagiwa mvua ya matusi hadi ujute..utaambiwa zaa wako huujui uchungu wake..nakamata nafinya napiga kuzaa hata chura anazaa..siwezi ona mtoto anafanya ujinga nikakaa kimya
Watoto wa siku hizi kama linadekezwa na wazazi wake usiliguse wewe rekebisha mwanao...ili anaposifiwa mwanao mbele yao wapate funzo...

Usije ukapata kesi bure...mimi nimekoma kwakwel...
 
Haahahahaha bimkubwa alikua hatari kufukuzwa tena nyumbani!! ..bimkubwa wangu ilikua ukifanya ivyo anakua kimya kama hakuna kilichotokea..anaacha unaoga unakula unajuaa soo limeisha..unataka kulala sasa pale ndipo mahojiano na kipigo kinapoanza chumbani mtu mbili tu..baba anaambiwa naomba ukae pembeni sitaki kuingiliwa ninapoadhibu mwanangu..utapewa kipigo na ole wako siku inayofuata unune au ususe kula..ole wako
Hahahaahhahaahahahah aiseeee heshima kwao wamama wakuda wote
 
Uwiii tena ukanda wa pwani ndio usiseme ..ukipiga mtoto wake utamwagiwa mvua ya matusi hadi ujute..utaambiwa zaa wako huujui uchungu wake..nakamata nafinya napiga kuzaa hata chura anazaa..siwezi ona mtoto anafanya ujinga nikakaa kimya
Hahahaha mie vitoto vya pwani naviheshimu mnooo tena ukute mama zao ni wale washinda baharini wale weeeeeeeeee
 
Hahahahahahaaa choo cha stand haswa.

Na baba ake ndie chanzo cha tabia chafu za kale katoto..mama ake amepigwa marufuku kumuadhibu akosapo..mama ake hana kauli kwa kale katoto

Mburaaaa nikuzae mwenyewe na bado unipande kichwani..haitakuja tokea
Eeeh huyo baba ana matatizo
 
Back
Top Bottom