MALEZI: Mzazi, Usimpe mtaji mwanao!

Dah!, umeniuzunisha kweli, mawazo haya ya karne izooo kitambo wakati kuna mapori anaenda kufyeka hapate shamba.
Karne hii tayarisha mtoto aweze kujisimamia mwenyewe, mpe mtaji wa pesa au wa aina yoyote,mbinu za kuizalisha na mbinu za kulinda mtaji. Nyie ndo mnasababisha wasomi hawana kazi wanasubili kuajiliwa na vitu wanavyo kichwani
Nikulee nikusomeshe nikupe na mtaji na mke juu!halafu uitwe je ? mwanaume?
 
Alichoongea kina mantik, japo mnakikataa bila hoja za msingi

Mtaji wa kujitafutia mwenyew unakua na uchungu nao sana kuliko na mtaji wa kupewa. Siunajua kesho utapewa tena ata ukikata.
Sio kweli mbona mo kila kitu karithi kwa baba ake na ndio tajiri nambari uno Tanzania hata baba make hakuwahi kuwa tajiri namba moja Tanzania? Pili umeshwahi kukutana na mtoto was kihindi au mwarabu anazunguka na bahasha kutafuta Nazi? Inshu sio mtaji tu mjeengee mazingira mazuri na misingi imara ya biashara atafanya vizuri
 
Nikulee nikusomeshe nikupe na mtaji na mke juu!halafu uitwe je ? mwanaume?
Ni kweli mkuu ndio maana tajiri namba moja Tanzania ni muhindi mo dewji na wahindi na waarabu ndio wanaoongoza kwa pesa Tanzania hii,wakati mtoto wako anatafuta milioni 5 afanye biashara muhindi au mwarabu anapewa milion10 afanye biashara baada ya miaka5 muhindi anakuwa na uzoefu was kutosha kwenye biashara na milioni 100 kwenye kaunti wakati huo mtoto wako ndo kaipata hiyo milion 5 hana uzoefu na hajui afanye biashara gani unadhani mwanao atatusua how?
 
Sasa mzee gani anakupigia hesabu tu then hakusaidii. Kipindi namtegemea shule alikuwa anakuja anaongea sweta limechakaa,viatu inabidi ubadilishe,kitu flani kinafaa kuwa hivi then akiondoka ananiachia hela ya kunyoa tu Kila nikipiga simu anadai ana vikao mara ana kazi siku nyingine anajifanya asikii vizuri hivo anasema ntakupigia kesho. Iyo kesho ni zaidi ya miezi mitatu kimya.Maza angekuwa maskini ningeshakuwa mojawapo ya magaidi maarufu hapa duniani maana nna aina flani ya roho ya kujichukia haiwezi ondoka
 
Sasa wewe utakuwa umemsaidia nini? kama na yeye ataanza moja. Ulitakiwa uwe na investment zako dogo akirudi unampa kitengo unamwangalia uwezo wake, kama yuko vizuri unampandisha taratibu hadi unamwachia biashara. Tatizo la wazazi wengi wao wenyewe wameshindwa kujikwamua. Ni sawa na mzazi alieajiriwa mpaka anastafu hana alichojiajiri alafu anamwambia kijana wake ajiajiri.
 
hii hoja ni nzuri na ina maana pana sana...muhimu mzazi uwe na watoto karibu, waulize wanapenda kufanya nini ukubwani....kama ni biashara kama wewe mzazi.... start to build them na kuhakikisaha masomo yake anafanya vyema.....mtaji ni mbinu na maarifa.....biasha sio lelemama.....so kama una uwezo wa biashara na unaweza kumpa mtaji mpe, mpe na miongozo....tusiwakee watoto mipaka....na tuendelee kuzaaaaa,,,,, elimu si ni bureeeeee
 
Sasa mzee gani anakupigia hesabu tu then hakusaidii. Kipindi namtegemea shule alikuwa anakuja anaongea sweta limechakaa,viatu inabidi ubadilishe,kitu flani kinafaa kuwa hivi then akiondoka ananiachia hela ya kunyoa tu Kila nikipiga simu anadai ana vikao mara ana kazi siku nyingine anajifanya asikii vizuri hivo anasema ntakupigia kesho. Iyo kesho ni zaidi ya miezi mitatu kimya.Maza angekuwa maskini ningeshakuwa mojawapo ya magaidi maarufu hapa duniani maana nna aina flani ya roho ya kujichukia haiwezi ondoka
😂😂😂😂😂..pole hope sahv anakuheshimu
 
Na huu ndiyo ukweli kama mwanao anapokuomba mtaji afanye sijui biashara usimpe.

Muulize tu nikikutafutia msichana utaoa? Atajibu hapana, mke nitatafuta mwenyewe. Basi mwambie na mtaji ajitafutie, aanze biashara yeye anayoiweza, utamuongezea tu. Siyo unamuanzishia mradi huo lazima utakufa tu.

Wazee wengi tunakwama hapa.
Mkuu basi ili ku-balance equation hata mtoto asimpe mzazi wake mtaji inapotokea akaombwa. Maana kuna wazazi wengi tu wanapewa mitaji na watoto wao.

Basi wafundishe na hao watoto endapo wazazi wao watawaomba mitaji wawajibuje katika kuwanyima hiyo mitaji waliyoombwa.
 
Alichoongea kina mantik, japo mnakikataa bila hoja za msingi

Mtaji wa kujitafutia mwenyew unakua na uchungu nao sana kuliko na mtaji wa kupewa. Siunajua kesho utapewa tena ata ukikata.
Sawa lakini sasa kwa nini iwe upande mmoja. Kuna wazee wengi tu wanawezeshwa mitaji na watoto wao. Basi mitaji yote ya kupewa ipigwe stop ili kila mtu (mtoto na/au mzazi) apambane kujitafutia mtaji ili awe na uchungu nao.
 
Ndio maana familia za Kiafrika huwa haziendelei sababu hela zote ziko centralised.

Niliwahi omba mtaji kidogo nikanyimwa iliniuma sana. Nikasaidiwa na mtu baki
 
Yani nyie madingi wa kibongo ni wanoko, Juzi nilisikia zee moja hapa mtaani, linasema kijana wake akimaliza chuo halitaki kumuona nyumbani. Eti aanze kujitegemea huko huko.
Hii ya kujitegemea haina ubaya wowote ikiwa kama utakuwa bado ujapata fedha atakuwa anakusapoti kidogo kidogo ili upambane ikiwapo kukupatia kimtaji kama inawezekana ili uazie kujikwamua.

Hiyo ya kuifukuza mitoto baada ya kumaliza chuo hasa ya kiume ili ikajitegemee hata mimi naweza kufanya. Sasa wewe umesomeshwa kwa mamilioni ya pesa alafu unamaliza chuo unarudi nyumbani kufanya nini? Unasomeshwa ili uje kupambana na ulimwengu ujitegemee siyo kurudi nyumbani kuhemea ugali.

Najua mwanzoni mazingira ya walio wengi yanakuwa sio rafiki kihivyo lakini nenda pambana siyo kujiregeza kwenye sofa na remote unaangali TV.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom