Malenga mgeni..

Ugeni si kitu chema, Mpoto ndoalosema,
Pema usijapo pema,JF hakika ni pema,
Mimi mwingi wa hekima,nina mengi ya kusema,
Mstakabali ndo jina langu,nipokeeni wenzangu.

usimfuate mpoto, upotoke kama foto,
miguu kama ufito, ewe malenga mtoto,
mizani gongo la mboto, na vina kwako ni ndoto,
hekima kitu adhimu, tutakupa tukipenda!

Wewe hunayo hekima, kisa umejiunga nasi
jitofautishe na kima, uyamenye mananasi,
vitani sikae nyuma, kwenye milio ya risasi
hekima kitu adhimu, tutakupa tukipenda.

Piga ngoma na kucheza, hii uliona wapi,
kiwete hawi mcheza, yeye bingwa wa pipi
mtini acha jikweza, tavuliwa mpaka chopi,
hekima kitu adhimu, tutakupa tukipenda,

kama kweli wewe ndiye, tusimulie kwa vina
ukiwa na kiseyeye, jei efu iko pina,
hatuchezagi uyeye, sijaribu kuguguna,
hekima hujipi wewe, jipambanue tukujue,

msikilize na Paw, vigezo uzingatie,
kama sheria ya faw, Invisible aipitie,
kama umezoea waw, ban Fang sikupitie
kweli wewe mgeni, kambayo guuni sitoe.
 
Last edited by a moderator:
Hii ni tenzi,
Leo 'menienzi,
Tembo la Mkwezi,
Hii ni tenzi.

Mgeni wa tunzi?
Mgeni muhanzi?
Usije na Kiangazi,
Hii ni tennzi.

Hapa si Chamanzi,
Ukweli vazi,
Wajibu si tambazi,
Hii ni tenzi.

Kanuni si kazi,
Kuzivunja simanzi,
Jiepushe na ubazazi,
Hii ni tenzi.

Hakika sijitie kitanzi,
Uwe muwazi,
mhogo si kiazi
Hii ni tenzi.

Hii ni tenzi
Hii tenzi,
Hii si tezi
Hii ni tenzi

 
Karibu malenga mgeni, ukiweza wewe tiririririririririka, usiogopeshwe na vina vya jogi wala mizani ya Paw. Ukipatwa na maumivu mwone Painkila. Hapa ban kupenda, na tena utatamanishwa, mizingu gonga repoti utajibiwa na fang na si ffu
 
Mgeni Isaacbest hakika ujuvi, nia na utashu vimekuleta,
Nikuhabarishe kuwa ujio wako wa pekee na ni heri kukuleta,
Invisible, Fang, Paw jukwaa la utambulisho umewaleta?
Hakika picha yajiri Isaac Newton jina lae pako ni sawia limegota.

Paw, isaacbest na jogi wanisamehe,
kwani mimi mashairi nachakachaua… lol

Karibu saana jf Isaac. Pamoja Saaana.
 
Back
Top Bottom