Malecela: Magufuli hatarini

Malecela: Magufuli hatarini

Maadui zake Ni hao hao anaocheka nao na kula nao anaowaita wenzake kwani wanaona kama amewageuka, watu hao hawapendi sifa alizopata ,Kasi ya kazi yake na mafanikio aliyopata kwa muda mfupi.
adhari za wabaya wake tayari tumeanza kuziona kwa baadhi ya watu walioshindwa kazi uongozi uliopita kurudi tena kazini ili wampunguze spidi.
tulitaka mabadiliko ya kweli ILA yalishindikana kutokana na mfumo mbovu WA nchi lakini gafla tumepata angalau ahueni kupata mtu aliye ndani ya mfumo mbovu mwenye filosofia ya mabadiliko ya kweli ,ikitokea akazimwa tutarudi kwenye machungu yale yale kilichobaki tumuombee ulinzi wa Mungu.
 
Namuunga mkomno Mzee Malechela kwani Mh. Rais ana maadui japo wachache lakini wenye jeuri ya pesa!!! Aongezewe ulinzi.

Tuungane wote kumuombea ulinzi wa MUNGU Mh. RAIS WETU MPENDWA
 
habari ya zamani magufuri amepunguza ulinzi kwa sababu ya kupunguza gharama, ameamua kulindwa na Mungu
 
Waziri mkuu mstaafu, bwana John Malecela, amesema ana hofu ya Raisi Magufuli kuhujumiwa na ameitaka serikali imuongezee ulinzi na kwamba isidharau.Mzee Malecela pia amekwenda mbali zaidi kwa kukumbuka jinsi Mwalimu Nyerere alivyotaka kupinduliwa.

Chanzo:JamboLeo

Bora na wakubwa nao sasa waseme,wengine tumebaki tu yetu macho na masikio.
Huwezi wafahamu maadui wa JPM Ila yy anawafahamu tutakachoshuhudia ni actions na Matukio.
 
Hawezi kuwa mshauri wa kitaifa tena baada ya Mtera kumuona hana la maana bora kibajaji. Atuambie hiyo hatari no ipi kwanza na nani anamshuku kufanya hayo. Sio wamelala na mkewe aliyepigwa chini ubunge kama yeye wakiamka ndoto zao wanazitoa hadharani zijadiliwe.
unajua bhana huu uongozi wa kusubiri upangiwe na nec -ccm ni noma sana ! kwa kauli hii ya malecela mkewe akapewa cheo bila hata kuangalia uwezo wake .
 
Nani amuongezee ulinzi ilihali yeye ndie serikali.si ajiongezee ulinzi.japo mi naamini watanzania tupo pamoja nae.
upo sahii nakuunga mkono yeye ndo kashika dola yote hadi ya ulinzi...lakini wadau kama malecela wanahitajika ili kutoa maoni yao na kufanyiwa kazi.. unaweza ukawa umeshika dola lkn ukawa hujui maadui wako kumbe watu wa nje tunawaona maadui wako...kikubwa tumuunge mkono ameonesha mwanzo mzuri..........
 
Na ole wao wathubutu kumdhuru raisi wetu Magufuli japo kwa lolote tu,
Nadhani ndio watajua kwamba Watanzania walikua wanampenda na kumhitaji au lah.
Kuna wakati itafika Tanzania haitatawalika,vita huku na huko uchochezi wa kidini na umwagaji damu,itakuwa heri Somalia na wakati huo wazungu watachekelea sana huku wakiongeza kasi ya kuiba kila kilichopo na hatimaye vizazi vijavyo vitakuwa hoi bin bin....
 
Haaa haaaa sidhani kama kauli ya Malecela inasimama hadi leo.
 
mhh huyu mama naye ni jipu katumbuliwa kajipu haka magufuli kakawah kabla hakajaiva
 
Mungu aliye mlinda shadrack; Meshack na Abedinego anamlinda na Magufuli hata Leo.
 
Ukiwa mjumbe wa nyumba kumi uliye madarakani na ukitoa kauli kama hiyo wala hakutakuwa na Athali zozote, but ukiwa na cheo kuanzia udiwani (labda) na ukitoa kauli hiyo, mrejesho utaupata tu (sababu unaijua)

Sasa John Malecela kwa title yake unategemea nini kutokana na kauli yake?
-:Hata akisema natoa kauli kama Mtanzania wa kawaida -hautasadiki pia!.
Hawezi kuwa mshauri wa kitaifa tena baada ya Mtera kumuona hana la maana bora kibajaji. Atuambie hiyo hatari no ipi kwanza na nani anamshuku kufanya hayo. Sio wamelala na mkewe aliyepigwa chini ubunge kama yeye wakiamka ndoto zao wanazitoa hadharani zijadiliwe.
 
Nani amuongezee ulinzi ilihali yeye ndie serikali.si ajiongezee ulinzi.japo mi naamini watanzania tupo pamoja nae.
Kuna washauri kuhusu Ulinzi kwani hujawahi msikia walinishauri one two three??? Ndio hao tunaowaambia kwa kifupi TISS!
 
Kuna wakati itafika Tanzania haitatawalika,vita huku na huko uchochezi wa kidini na umwagaji damu,itakuwa heri Somalia na wakati huo wazungu watachekelea sana huku wakiongeza kasi ya kuiba kila kilichopo na hatimaye vizazi vijavyo vitakuwa hoi bin bin....

Hayo uliyotabiri nayafuta kwa JINA LA YESU Kristo hayatatokea kamwe katika nchi hii kwa DAMU ya YESU KRISTO.

Nchi itabaki kuwa ya amani na utulivu na ole wake atakayeleta machafuko hatadumu ingawaje kuna tatizo kubwa sana la kukosekana kwa HAKI na kuminya DEMOKRASIA. Serikali isimamie haki na kuheshimu demokrasia ili amani yetu iwe na maana
 
Back
Top Bottom