Malecela: CCM Arusha imewakosea maaskofu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malecela: CCM Arusha imewakosea maaskofu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 10, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,895
  Likes Received: 416,603
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Mwananchi la leo linatuhabarisha ya kuwa mkongwe wa siasa nchini ametofautiana na akina Makamba na vigogo wengineo ndani ya CCM kwa kubainisha ya kuwa CCM Arusha ndiyo imewakosea maaskofu na hivyo wanapaswa kuwaomba msamaha na ya kuwa uchaguzi wa Umeya haukuzingatia misingi ya haki na hivyo ni batili.......

  Malecela: CCM imekosa adabu kwa maaskofu

  Sunday, 09 January 2011 21:03

  Boniface Meena na Fredy Azzah

  WAZIRI Mkuu wa zamani, John Malecela, amesema kuwa CCM imewakosea adabu maaskofu hivyo inapaswa kukutana nao na kuwaomba radhi.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Malecela alisema kitendo cha kuwashambulia maaskofu hao kilichofanywa na CCM mkoani Arusha ikiwa ni pamoja na kuwataka wavue majoho na kuingia kwenye siasa, ni utovu wa nidhamu.

  Kauli ya Malecela ambaye pia ni kada wa CCM, imekuja siku mbili baada ya chama hicho mkoani Arusha kuwataka maaskofu mkoani humo, kuvua majoho na kutangaza kuingia kwenye siasa, badala ya kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.

  Januari 7 mwaka huu, maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha, walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba "hawatampa ushirikiano".

  Walitoa tamko hilo wakati wakilaani hatua ya polisi mkoani Arusha kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano ya amani ya Chadema na hivyo kusababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi wengine zaidi ya 20.

  Akisoma tamko la umoja wa viongozi wa dini ya Kikristo mkoani Arusha, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu alisema Jeshi la Polisi ndilo lilikuwa chanzo cha vurugu hizo.

  "Sisi kama viongozi wa dini hatuwezi kushirikiana na mtu ambaye hakushinda kihalali, kuna mtu alipiga kura si diwani wa Arusha, Chadema hawakushirikishwa na pia taratibu na kanuni za uchaguzi huo zilikiukwa," alisema askofu huyo.

  Lakini, Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa kitendo cha maaskofu hao kusema hawamtambui Meya wa CCM, Gaudence Lyimo, kimewashtua.

  "Tunawaheshimu sana viongozi wa dini...Ila wanapoingilia masuala ya siasa ni bora wavue majoho tukutane viwanja vya siasa kama alivyofanya mwenzao Dk Slaa," alisema Chatanda.

  Katibu huyo ambaye ndiye chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa mbunge wa viti maalumu kupitia Mkoa wa Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa.

  Chatanda ambaye katika mkutano huo alikuwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa, Onesmo Ole Nangole, alisema kazi ya maaskofu ni kuelekeza njia za imani za kwenda mbinguni na sio siasa.

  "Waje kwenye siasa wagombee udiwani...ili wachague meya. Tulitegemea kabla ya tamko lao wangetuita sote na tukae na tutoe maelezo yetu na hapo ukweli wangeupta, lakini kusema uchaguzi haikuwa halali sio kweli," alilalamika Chatanda.

  Wakati katibu huyo wa mkoa wa CCM akieleza hayo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba alienda mbali zaidi na kuwataka maaskofu hao waende mahakamani au wawashauri Chadema kufanya hivyo kwa lengo la kupinga matokeo ya umeya.

  Makamba alisisitiza kuwa msimamo wa CCM ni kwamba chama hicho ndicho kilichoshinda katika uchaguzi huo wa umeya Arusha.

  Alisema hakuna njia ya kubadili matokeo hayo zaidi ya kufungua kesi mahakamani.

  Lakini jana Malecela alisema CCM inatakiwa kutumia busara kushughulikia mgogoro wa umeya mkoani Arusha badala ya jazba na utovu wa nidhamu.

  Alisema kauli ya katibu huyo wa CCM dhidi ya maaskofu inakera na ili kuweka mambo sawa, ni bora chama hicho tawala kiwaombe radhi viongozi hao wa dini.

  "Ni wazi kwamba alichokisema Chatanda hakiwezi kuwa kauli ya chama. Hayo ni maneno yake na ni utovu wa nidhamu. Nasikitika sana kauli ni ya kwake na si ya chama hivyo aombe radhi," alisema Malecela ambaye alibainisha kuwa chama cha siasa hakina uwezo wa kuwataka maaskofu wavue majoho.

  Kwa mujibu wa Malecela, viongozi wa dini wako tangu enzi za kale na wamekuwa wakiikosoa Serikali tangu wakati huo na haiajawahi kutokea kiongozi wa chama akawarukia kwa maneno makali kiasi hicho.

  Malecela alisema hiyo sio kauli ya CCM, lakini kwa kuwa imetolewa na mwanachama wake, chama hakina budi kukutana na viongozi hao wa dini na kuwaomba radhi.

  Kauli iliyotolewa ni ya kutokuwa na adabu kwa watu kama maaskofu," alisema Malecela.
   
 2. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  mkongwe amechoka na siasa za uonevu,au ni baada ya kutoswa na ccm ndio anaona mabaya ya ccm
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni msema kweli, msiunganishe na history, kasema kweli period
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  hata kama huko nyuma aliwahi kuwa kero, lakini kwa hili yuko sahihi, big up malecela, ukienda kamati kuu waambie kweupe; hakuna udini hapa, tunachogombea ni mauaji yaliyokuwa yanaweza kuepukika
   
 5. m

  mapambano JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I don't agree with mzee Malecela, then I do not under estimate the power of faith when one is trying to be objective.

  The truth is more people are losing hopes/faith with JK government and becoming impatient as time goes. However, I think such a bold political statement should have not come from any religious leaders, full stop!! The ramifications of religious leaders ( whether Christian, Islam, Hindu, etc) taking a stand in a political platform could be more devastating to our beloved nation.

  NOW ITS THE TIME TO STOP RELIGIOUS LEADERS TO MAKE POLITICAL STATEMENTS BEFORE ITS TOO LATE OR WE ARE BOUND TO START KILLING EACH OTHER !!!!
   
 6. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  if we will maintain our faithfulness in our nation and our relatives, and if we will consider their presence towards our nation cakes, all dis will be story.
  But our greed, selfishness and miscarring will make situation be more worse.
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  In truth, politeness is artificial good humor; it covers the natural want of it, and ends by rendering habitual a substitute nearly equivalent to the real virtue.
   
 8. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  BID UP Malecela! MVI sasa zinaweza kusema ukweli-si ujina wa akina makamba
   
 9. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  The Arusha mayorial elections were a sham and it takes a lunatic to say otherwise. The simplest of the solutions is to have it annulled and let people participate in a free and fair process. If this was done, the bleck spot that has now stuck on our white cloth would not be there. Unfortunately we have always loved to learn the hardway. Lives of innocent people have been lost and others have been maimed. Where will this GREED TAKE US?
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  I meant the BLACK SPORT not bleck! Sorry
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Infact BLACK SPOT
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kama anamaanisha anachosema aondoke huko
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,300
  Likes Received: 22,102
  Trophy Points: 280
  Babu kachoshwa na dhuluma za ccm
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,794
  Trophy Points: 280
  mtu mzima wewe amenena jamani naamini yuko sahihi.
   
 15. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tusiangalie historia tuangalie usahihi wa yale anayoyasema na tushukuru zaidi kama wazee wetu hawa wanasimamia haki.Kitendo walichofanya CCM arusha ni uvunjifu wa haki na amani pia,kwa ufupi ni uhuni wa kupitiliza katika siasa na ni hatarishi kuiingiza nchi katika machafuko.
   
 16. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Huyo Mary Chatanda, Katibu wa CCM (M) ni mKristo kweli ama anaiga majina ya kiKristo. Atawaambiaje viongozi wa dini wavue majoho?
   
 17. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  good one malecela
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,895
  Likes Received: 416,603
  Trophy Points: 280
  Malecela: CCM imekosa adabu kwa maaskofu
  Sunday, 09 January 2011 21:03

  Boniface Meena na Fredy Azzah
  WAZIRI Mkuu wa zamani, John Malecela, amesema kuwa CCM imewakosea adabu maaskofu hivyo inapaswa kukutana nao na kuwaomba radhi.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Malecela alisema kitendo cha kuwashambulia maaskofu hao kilichofanywa na CCM mkoani Arusha ikiwa ni pamoja na kuwataka wavue majoho na kuingia kwenye siasa, ni utovu wa nidhamu.

  Kauli ya Malecela ambaye pia ni kada wa CCM, imekuja siku mbili baada ya chama hicho mkoani Arusha kuwataka maaskofu mkoani humo, kuvua majoho na kutangaza kuingia kwenye siasa, badala ya kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.

  Januari 7 mwaka huu, maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha, walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba "hawatampa ushirikiano".

  Walitoa tamko hilo wakati wakilaani hatua ya polisi mkoani Arusha kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano ya amani ya Chadema na hivyo kusababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi wengine zaidi ya 20.

  Akisoma tamko la umoja wa viongozi wa dini ya Kikristo mkoani Arusha, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu alisema Jeshi la Polisi ndilo lilikuwa chanzo cha vurugu hizo.

  "Sisi kama viongozi wa dini hatuwezi kushirikiana na mtu ambaye hakushinda kihalali, kuna mtu alipiga kura si diwani wa Arusha, Chadema hawakushirikishwa na pia taratibu na kanuni za uchaguzi huo zilikiukwa," alisema askofu huyo.

  Lakini, Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa kitendo cha maaskofu hao kusema hawamtambui Meya wa CCM, Gaudence Lyimo, kimewashtua.

  "Tunawaheshimu sana viongozi wa dini...Ila wanapoingilia masuala ya siasa ni bora wavue majoho tukutane viwanja vya siasa kama alivyofanya mwenzao Dk Slaa," alisema Chatanda.

  Katibu huyo ambaye ndiye chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa mbunge wa viti maalumu kupitia Mkoa wa Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa.

  Chatanda ambaye katika mkutano huo alikuwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa, Onesmo Ole Nangole, alisema kazi ya maaskofu ni kuelekeza njia za imani za kwenda mbinguni na sio siasa.

  "Waje kwenye siasa wagombee udiwani...ili wachague meya. Tulitegemea kabla ya tamko lao wangetuita sote na tukae na tutoe maelezo yetu na hapo ukweli wangeupta, lakini kusema uchaguzi haikuwa halali sio kweli," alilalamika Chatanda.

  Wakati katibu huyo wa mkoa wa CCM akieleza hayo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba alienda mbali zaidi na kuwataka maaskofu hao waende mahakamani au wawashauri Chadema kufanya hivyo kwa lengo la kupinga matokeo ya umeya.

  Makamba alisisitiza kuwa msimamo wa CCM ni kwamba chama hicho ndicho kilichoshinda katika uchaguzi huo wa umeya Arusha.

  Alisema hakuna njia ya kubadili matokeo hayo zaidi ya kufungua kesi mahakamani.

  Lakini jana Malecela alisema CCM inatakiwa kutumia busara kushughulikia mgogoro wa umeya mkoani Arusha badala ya jazba na utovu wa nidhamu.

  Alisema kauli ya katibu huyo wa CCM dhidi ya maaskofu inakera na ili kuweka mambo sawa, ni bora chama hicho tawala kiwaombe radhi viongozi hao wa dini.

  "Ni wazi kwamba alichokisema Chatanda hakiwezi kuwa kauli ya chama. Hayo ni maneno yake na ni utovu wa nidhamu. Nasikitika sana kauli ni ya kwake na si ya chama hivyo aombe radhi," alisema Malecela ambaye alibainisha kuwa chama cha siasa hakina uwezo wa kuwataka maaskofu wavue majoho.

  Kwa mujibu wa Malecela, viongozi wa dini wako tangu enzi za kale na wamekuwa wakiikosoa Serikali tangu wakati huo na haiajawahi kutokea kiongozi wa chama akawarukia kwa maneno makali kiasi hicho.

  Malecela alisema hiyo sio kauli ya CCM, lakini kwa kuwa imetolewa na mwanachama wake, chama hakina budi kukutana na viongozi hao wa dini na kuwaomba radhi.

  Kauli iliyotolewa ni ya kutokuwa na adabu kwa watu kama maaskofu," alisema Malecela.
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,866
  Trophy Points: 280
  Malecela mzee wangu, hatimae sasa unatuonyesha busara zako bila kujali kama wale wa Chama Twawala watachukia au kununa. Hivyo ndivyo ulivyokuwa unapaswa uwe.
   
 20. Nchi Kavu

  Nchi Kavu JF-Expert Member

  #20
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 3,519
  Likes Received: 1,041
  Trophy Points: 280
  Ukubwa dawa. Mzee umenena. Hiyo ndio faida ya kutaka kuwapa wanawake 50/50.
   
Loading...