Malaysian Model

Malaysian Model

Adili

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2007
Posts
3,138
Reaction score
1,122
Hii imetokea tanzanet........

Hivi miaka ilee kulikuwa na ufazili mkubwa sana ktk civil service sector review, na bale bazungu balitupa model zao za performance based system, yakafanyika ma logic model strategic planning planning kila kona, madokumenti luluki yakatengenezwa na moja ya sehemu ambayo nakumbuka ilileta sana mang'ana ilikuwa kupunguza idadi ya watumishi wa kada za chini kama wapiga deki, waleta vitumbua, wabeba barua na madereva. Tikaambiwa wakuu wote wa vitengo/idara wenye magari lazima wajiendeshe wenyewe na madereva watabaki wachache kwa safari ndefu au kwa ajili ya kazi maalum. Office mgt secretaries wakawezeshwa ili kufanya kazi zao vizuri- wakuu wa idara pia wakaambiwa lazima kujifunza kutaipu wenyewe- vimemo vidogo vidogo na taarifa muhimu za siri - makompyuta yakamwagwa na semina zikaendeshwa ila waingereza waligoma kutoa posho !!
Wapo waliofurahia kujiendesha wenyewe, na wapo waliokataa katakata kwani kwanza waliogopa kama wakipata pancha itakuwaje, na wengine ukubwa wa vitambi ulikuwa shida. Wengine, waliona ni kama kujishusha hadhi maana bosi lazima aendeshwe na wengine, waliona itaharibu uspuni wao, na kuwapunguzia soko ktk harakati za kufukuzia small hausi..

Sasa usiniulize haya maazimio na madudu yote ya PBS, malojiko fremuweki yenye makolamu ya indiketa, minzi ofu velifikesheni na juu yakiwa yamerembwa na smati autikamu yaliishia wapi, na ukienda kuchungulia maofisi sasa utakuta watumishi zaidi ya mara mbili ya waliokuwemo zamani !! Na ktk kuonyesha tumepiga hatua zaidi, sasa hivi kuna bajeti kabisa waheshimiwa idodomya wanapitisha fungu la vitafunwa !! Hao hao wakuu wana receipted na non-receipted alawanzi kila mwezi, na chapati, chuzi, ndizi na mpaka kuku laivu wanauzwa maofisini (sijui kama kuna wachinjaji pia RM ebu saidia kudeki hili..) n.k

Sasa leo hii eti timeanza mfumo mpya na wakuu wote hawa wamejichimbia mzakwe kujifua, na hili litaimbwa weee wakati mikukuta na mikurabita bado inachechemea, sijui kuna MDGs, na MCCs, na kilimo pwanza...??

Siajabu hata madudu ya malaysia ni moja ya masharti...si unajua tena umasikini ni expensive...!!

CAG, kila mwaka anatoa ripoti weee but where.....sasa leo tunasikia trilioni ngapi vile zimepotea hewani, na eti kumbe nyingine walikopeshana kienyeji hadi tukururu... ??? Sitashangaa nyingine wakisema walikopesha polisi ktk posho za wale warusha mabomu na virungu kuzibiti wafuasi wa kile chama cha wakibosho wa mweka sungu 🙂

NB: Hivi watu wasio wasio ukumbi huu wanasomaje jumbe zetu humu ??? Kuna njemba imenipigia leo ikishangaa vipi napinga kuku kuchinjwa, na ikadai labda niende bongo na gari lenye zizi la kuku nyuma yake, maana foleni zilivyo ndefu ana uhakika by the taimu nafika homu bila kuwa na banda huko kokoliko atakuwa amekufa !!!
Now I know kwa nini watu wanasema wanakwenda londoni kutafuta nondo, ngoja na mimi niwatafute wagunya wangu kule uswazi kujua kama kuna dili za makreti buy none, get one free !!

Mjumbe hauawi......
 
Hauwezi kuwa na Malaysian model bila kuchukua hatua za kuwawezesha Wamalaysia kwanza. Malaysia kuna makabila matatu makubwa. Wamalay, Wahindi na Wachina. Alichofanya Mahathir ni kuchukua hatua kuwawezesha Wamalay, ambao walizidiwa uwezo kielimu na kibiashara na Wachina na Wahindi ( wakuja) ili nao wafaidike na keki ya taifa. Leo sisi tunawahamisha wananchi ili kumpa ardhi mzungu au mwarabu. Hiyo si Malaysian model hata kidogo.
 
Back
Top Bottom