"Malaya hao"..!

“Sitaki kabisa kukuona na wale wanawake. Utakuwaje na urafiki na Malaya wale. Sasa hivi watakuuza kirahisi kabisa. Ukitaka kuifanya ndoa yetu ianze vurugu, endelea kuwa na urafiki nao. Wanawake kibao hapa mjini wamekuwa Malaya na kuvunja ndoa zao kwa sababu ya kuwa na marafiki wasio na mpango.”

Je wewe unakubaliana na dhana hii, kuwa mwanamke aliyeolewa kuwa na urafiki na wanawake wasio waaminifu au wanaoitwa Malaya, basi naye atashawishiwa hadi awe Malaya?

Haswaaa yawezekana %80.
 
Huo usemi una ukweli kabisa... show me your friends I will tell you who you are.

Kwa kifupi mke wa mtu hapaswi kuwa mtu wa mashoga wawe watulivu au mapepe. Muda wa kuangalia famila atapata wapi na wakupiga soga atapata wapi???? Ndoa nyingi zinazodumu ni za wanawake wasio na muda mchafu na ushoga wa aina yeyote; maana kuna ushauri mwingi wa kubomoa unatoka kwa mashoga; mfano tatizo dogo la ndani unaweza share nao wakakupa ushauri wa ku seek for a divorce!

UNAUJUA USEMI HUU??? nionyeshe rafiki zako nitakueleza tabia zako
 
Baba shkamoo!
Mada inasemaje tena Baba yangu?! Mimi nasema kuwa inategemea na ukaribu au frequency ya kukutana na hao marafiki!!! Ila baba huyo anayegombezwa hivyo ni mke au mtoto? Mke hagombezwi unaongea nae

Katika wanangu wooooote, wewe pekee ndio umerithi kipaji changu.................... hata hivyo nashukuru umesoma hii maneno kinyumenyume na ndio maana ni wewe pekee umeelewa vizuri..............LOL kwa nini wanaume wanakuwa huru kujichagulia marafiki na si wanawake!?
 
Mtambuzi tatizo si kukubali kuuzwa hapa nachoweza kusema ni kuwa kuna uwezekano wa 99% huyo wife naye ni malaya. Haiwezekani awe na marafiki malaya afu yeye ni innocent; kipi kimemvutia kwa hao mashoga zake. Ukute yeye ndo kiongozi wa kundi la hao malaya.

Hivi kweli mtu mzima ambaye ameolewa na anajua majukumu yake kama mke, ile kuwa na urafiki na wanawake wenye tabia hizo zinazoitwa za umalaya akubali tu kuuzwa na kuwa malaya! hivi hili linawezekana kweli?
 
Huo usemi una ukweli kabisa... show me your friends I will tell you who you are.

Kwa kifupi mke wa mtu hapaswi kuwa mtu wa mashoga wawe watulivu au mapepe. Muda wa kuangalia famila atapata wapi na wakupiga soga atapata wapi???? Ndoa nyingi zinazodumu ni za wanawake wasio na muda mchafu na ushoga wa aina yeyote; maana kuna ushauri mwingi wa kubomoa unatoka kwa mashoga; mfano tatizo dogo la ndani unaweza share nao wakakupa ushauri wa ku seek for a divorce!

Kwa hiyo kwa kuwa marafiki zangu ni akina Bujibuji, Washwasha, Rejao, Ndyoko, Asprin na Klorokwin, basi na tabia zangu utakuwa unazijua?
 
Mbona tabia za watu humu nshazijua siku nyingi tokana na mitandao waliyo subscribe. lol.

Kwa hiyo kwa kuwa marafiki zangu ni akina Bujibuji, Washwasha, Rejao, Ndyoko, Asprin na Klorokwin, basi na tabia zangu utakuwa unazijua?
 
Mtambuzi tatizo si kukubali kuuzwa hapa nachoweza kusema ni kuwa kuna uwezekano wa 99% huyo wife naye ni malaya. Haiwezekani awe na marafiki malaya afu yeye ni innocent; kipi kimemvutia kwa hao mashoga zake. Ukute yeye ndo kiongozi wa kundi la hao malaya.

Kwa hiyo kama mke wa mtu ni msusi, halafu wateja zake hapo mtaani ndiyo hao wanaoitwa malaya, ndiyo awanunie...............!?
 
Kwanza ushawahi sikia kuwa wafanyakazi wa saloon wengi utulivu zero??? But kuna ninao wajua unaenda kusuka mpaka unamaliza hajaongea kitu; na bado ana wateja wa kumwaga. Huna haja ya kuwa na kundi la mshoga ndio uwe msusi wa kukimbiliwa. Watu watakuja kwa sababu ya kazi yako na si mdomo. In most cases wasusi wenye midomo (ambao ni wengi) wana end up kugombana na wateja wao. Mi nimekuja kusuka unaanza kuniuliza story za mume wangu au familia yangu inahuu.

Kwa hiyo kama mke wa mtu ni msusi, halafu wateja zake hapo mtaani ndiyo hao wanaoitwa malaya, ndiyo awanunie...............!?
 
Mawazo ya wengi yameonesha kuwa ukiwa na marafiki wa aina fulani, nawe utakuwa umeangukia au kuna hatari ya kuangukia kundini mwao. Uwezekano upo, sikatai, lakini sio lazima. Yote inategemea mtu (he/she) yuko makini kiasi gani. Huwezi kuwa mlevi, cameroon, asherati... eti kwa sababu tu marafiki zako wako hivyo. Kama uko makini, umakini wako unaweza kuutumia kuwashauri wawache na sio wewe kuangukia humo.

Nasema haya kwa sababu ninao marafiki wa aina nyingi. Ninapopata nafasi na kuona kuna mwelekeo wa kuwashauri (hasa kwa yale yanayohusu tabia), hutoa mchango wangu. Kwa wasiotaka ushauri, hainipelekei kuwanyanyapaa. Kwa mfano, unaye rafiki wa miaka mingi, siku moja unagundua kuwa ni cameroon au malaya/kicheche (kwanza hizi sifa sipendi kuzitumia katika mazungumzo yangu kwa kumwonesha kidole mtu), unamtenga ili asije kukuambukiza tabia zake?

Zaidi ya yote, kwa nini tunakuwa na "prejudices" hizi zaidi kwa wanawake? Hata katika malezi yetu, msichana anawekewa mipaka kadhaa kuliko mvulana. Mvulana akiwa na tabia za ucheche, huyo tunamwita kidume, msichana akizungumza tu na mvulana, huyo anaelekea kubaya.
 
"Sitaki kabisa kukuona na wale wanawake. Utakuwaje na urafiki na Malaya wale. Sasa hivi watakuuza kirahisi kabisa. Ukitaka kuifanya ndoa yetu ianze vurugu, endelea kuwa na urafiki nao. Wanawake kibao hapa mjini wamekuwa Malaya na kuvunja ndoa zao kwa sababu ya kuwa na marafiki wasio na mpango."

Je wewe unakubaliana na dhana hii, kuwa mwanamke aliyeolewa kuwa na urafiki na wanawake wasio waaminifu au wanaoitwa Malaya, basi naye atashawishiwa hadi awe Malaya?

Wapo watu ambao ni rahisi sana kuvutwa na kushawishiwa na marafiki. Ukiwa na mke au mume wa hivyo ujue umeula wa chuya.

Sasa uwe na mke ambaye hana misimamo ya kimaadili na ambaye ni bendera fuata upepo halafu awe na marafiki chakaramu chakaramu...hapo sitashangaa kabisa kama naye akianza kuwa kama wao.

Kupata mtu ambaye si bendera fuata upepo, ambaye anafanya maamuzi yake mwenyewe bila shinikizo la marafiki ni tunu.
 
Aisee, wewe Fe Lady na baadhi ya wengine mmewaza nje ya box, ukilinganisha wachangiaji wengi waliochangia hii mada............ Ahsante kwa kunisaidia kujibu hili swali, nilidhani ni mimi peke yangu mwenye mtazamo tofauti.............!
 
Wapo watu ambao ni rahisi sana kuvutwa na kushawishiwa na marafiki. Ukiwa na mke au mume wa hivyo ujue umeula wa chuya.

Sasa uwe na mke ambaye hana misimamo ya kimaadili na ambaye ni bendera fuata upepo halafu awe na marafiki chakaramu chakaramu...hapo sitashangaa kabisa kama naye akianza kuwa kama wao.

Kupata mtu ambaye si bendera fuata upepo, ambaye anafanya maamuzi yake mwenyewe bila shinikizo la marafiki ni tunu.

Nimekosa kitufe cha LIKE................. Ahsante mkuu..........
 
Ukweli unabaki pale pale; mfano ukiwa kama mzazi makini; watoto wako wawe wa kike au wa kiume hutapenda waongozane na watoto walio na tabia usizo zipenda. Kwa nini utegemee maajabu ya Mungu na kuishi kwa hope kuwa mwanao si bendera badala ya kumuepusha na vishawishi???? What if ni bendera???

Hii si kwa wanawake tu hata wanaume wanafuata upepo vile vile including kuwa na vimada kwa kuwa washkaji wao wote wanavyo. Lazima mtu uchague marafiki. Otherwise ndio hayo ya mkuu wetu wa kaya.

Na kumbuka kuwa ufikiri wetu unaathiriwa kwa kiasi kikubwa na stereotyping. Ukiwa na mke anayezungukwa na malaya jua wazi watu watakuwa wanamwita mkeo malaya; hawana muda wa sijuhi kuchunguza ooh malaya ni rafiki zake tu yeye ni tofauti; stereotyping ina save muda wa kufanya research kama hizo; rafiki zako malaya na wewe malaya simple!

Mawazo ya wengi yameonesha kuwa ukiwa na marafiki wa aina fulani, nawe utakuwa umeangukia au kuna hatari ya kuangukia kundini mwao. Uwezekano upo, sikatai, lakini sio lazima. Yote inategemea mtu (he/she) yuko makini kiasi gani. Huwezi kuwa mlevi, cameroon, asherati... eti kwa sababu tu marafiki zako wako hivyo. Kama uko makini, umakini wako unaweza kuutumia kuwashauri wawache na sio wewe kuangukia humo.

Nasema haya kwa sababu ninao marafiki wa aina nyingi. Ninapopata nafasi na kuona kuna mwelekeo wa kuwashauri (hasa kwa yale yanayohusu tabia), hutoa mchango wangu. Kwa wasiotaka ushauri, hainipelekei kuwanyanyapaa. Kwa mfano, unaye rafiki wa miaka mingi, siku moja unagundua kuwa ni cameroon au malaya/kicheche (kwanza hizi sifa sipendi kuzitumia katika mazungumzo yangu kwa kumwonesha kidole mtu), unamtenga ili asije kukuambukiza tabia zake?

Zaidi ya yote, kwa nini tunakuwa na "prejudices" hizi zaidi kwa wanawake? Hata katika malezi yetu, msichana anawekewa mipaka kadhaa kuliko mvulana. Mvulana akiwa na tabia za ucheche, huyo tunamwita kidume, msichana akizungumza tu na mvulana, huyo anaelekea kubaya.
 
hii kitu huwa inakuwa kweli kama anayeambiwa kuamua kufanya vitu ambavyo alikuwa amejizuia kutokuvifanya..
 
"Sitaki kabisa kukuona na wale wanawake. Utakuwaje na urafiki na Malaya wale. Sasa hivi watakuuza kirahisi kabisa. Ukitaka kuifanya ndoa yetu ianze vurugu, endelea kuwa na urafiki nao. Wanawake kibao hapa mjini wamekuwa Malaya na kuvunja ndoa zao kwa sababu ya kuwa na marafiki wasio na mpango."

Je wewe unakubaliana na dhana hii, kuwa mwanamke aliyeolewa kuwa na urafiki na wanawake wasio waaminifu au wanaoitwa Malaya, basi naye atashawishiwa hadi awe Malaya?
Mzingira ndo huwa yanasababisha yote lakini aslimia 99 wengi wanababuliwa kwa dhana ya mazingira kwani kama nikwenye kilevi wengi wao ukuta tayari wameingi kwenye mtego na kubabuliwa!!
 
Back
Top Bottom