"Malaya hao"..!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
“Sitaki kabisa kukuona na wale wanawake. Utakuwaje na urafiki na Malaya wale. Sasa hivi watakuuza kirahisi kabisa. Ukitaka kuifanya ndoa yetu ianze vurugu, endelea kuwa na urafiki nao. Wanawake kibao hapa mjini wamekuwa Malaya na kuvunja ndoa zao kwa sababu ya kuwa na marafiki wasio na mpango.”

Je wewe unakubaliana na dhana hii, kuwa mwanamke aliyeolewa kuwa na urafiki na wanawake wasio waaminifu au wanaoitwa Malaya, basi naye atashawishiwa hadi awe Malaya?
 
Kiongozi si unajua tena ndege warukao pamoja huwa na mbawa zinazolingana...............

Kama kuna watu sio waaminifu kwa kweli haina haja kuwa na urafiki na mkeo, hata kama atajitetea kuwa ana akili zake timamu lakini kuna nini cha interest anachokipata kwa watu wa aina hiyo? Na je jamii inapomuona nao inapata picha gani?

Sioni sababu hata kidogo!
 
Yaah. Uwezekano huo upo ingawaje sio wote. Kuna binti enzi zile tukiwa chuo. Alipangiwa room moja na wadada wenye tabia hizo. Baada ya muda akawa mfuasi wao na kuwazidi malaya wenyewe.
 
Baba, hii sijaisoma. Shkamoo! Mwl wa Sunday Skul anakusalimia

Nilisahau kuweka onyo kwenye heading kuwa usije ukafungua hii maneno, hata my Daughter Lizzy na mwanangu mwingine MJ1, sitaki kabisa wasome hapa, kwani watajifunza tabia mbaya...................LOL
 
Mh. Hapo ni kama unauliza msuli pemba! Na haitakua umetenda haki kuisifu filimbi ukaacha kumsifu "mpiga filimbi" nna maana haina mantiki uwalaumu wanaom'buruza kunako ujinga yeye akaonekana innocent! HAKUNAGA kama MNAPENDANAGA aidha ht na mie na nna tatizo linaloelekea kufanana na lako
 
inawezekana kuna kijiukweli lakini mumeo akikwambia maneno haya fanya uchunguzi. Ujue keshaharibu huko anataka akutenganishe nao ili ukweli usitoke.
 
:A S 465:Msimamo na akili vina ukomo mwishowe anawezashawishika akaingia kundini the best option is to stop the relation otherwise Majuto mjukuu

Hivi kweli mtu mzima ambaye ameolewa na anajua majukumu yake kama mke, ile kuwa na urafiki na wanawake wenye tabia hizo zinazoitwa za umalaya akubali tu kuuzwa na kuwa malaya! hivi hili linawezekana kweli?
 
nakubaliana na hilo.... na utakuaje na urafiki na malaya kama wewe si malaya
 
ukiona mwanamke anashawishiwa na mashoga zake kusaliti ndoa, huyo anaitwa kichwa panzi.

Uaminifu katika ndoa ni value unayofundishwa na wazazi, hasa mie huamini nafasi ya mama ni kubwa sana hapa, kama mama alikuwa anagawa hata watoto hawatakuwa na hiyo value ya uaminifu lakini kama mama alikuwa mwaminifu hata mabinti zake huwa waaminifu.
Chunguza umeoa kwenye familia ya aina gani, kama ni vichwa panzi jenga na uzio kabisa.
 
wanawake wasio waaminifu > ushasema wasio waaminifu sasa urafiki nao maana unataka ajifunze kutokuwa mwaminifu.Tena hasa kwenye visaloon ivi kuna washenzi wanafanya sana iyo kazi ya ukuhadi wa wake za watu
 
wanawake wasio waaminifu > ushasema wasio waaminifu sasa urafiki nao maana unataka ajifunze kutokuwa mwaminifu.Tena hasa kwenye visaloon ivi kuna washenzi wanafanya sana iyo kazi ya ukuhadi wa wake za watu

Kweli eh! Kwa hiyo akili Mukichwa........................!!!!
 
nakubaliana na hilo.... na utakuaje na urafiki na malaya kama wewe si malaya

Sisi tunaoishi nyumba sa kupanga huku uswahilini basi tuna kazi, maana waweza kuta unaishi nyumba moja wauza Bar kadhaa, na wale wanajiuza wamo humo humo, na mkeo ni mama wa nyumbani. kama ujuavyo, kuna kuazimana vibao vya nazi, kuombana chumvi, na usisahau habari ya kusukana Mabutu, na kuchapa umbea............................. Kama ni hivyo, ndoa zetu zitasalimika kweli?
 
Nilisahau kuweka onyo kwenye heading kuwa usije ukafungua hii maneno, hata my Daughter Lizzy na mwanangu mwingine MJ1, sitaki kabisa wasome hapa, kwani watajifunza tabia mbaya...................LOL

Baba shkamoo!
Mada inasemaje tena Baba yangu?! Mimi nasema kuwa inategemea na ukaribu au frequency ya kukutana na hao marafiki!!! Ila baba huyo anayegombezwa hivyo ni mke au mtoto? Mke hagombezwi unaongea nae
 
Back
Top Bottom