Malawi: Kiongozi wa upinzani, Lazarus Chakwera ashinda Uchaguzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,017
9,885
Kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera akiwahutubia wafuasi wake (picha ya maktaba)
Maelezo ya picha
Mwanga wa siasa ya Lazarus Chakwera ulifufuliwa baada ya mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka jana

Kiongozi wa upinzani nchini Malawi Lazarus Chakwera ameshinda duru ya pili ya uchguzi wa urais, maafisa wanasema.

Alimshinda rain aliyekuwa rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kwa sailimia 58.57 ya kura Katina uchaguzi wa Jumanne, tume ya uchaguzi ilitangaza usiku wa Jumamosi.

Mwezi Februari, Mahakama ya katiba nchini Malawi ilifutilia mbali ushindi wa Mutharika' katika uchaguzi wa Mei 2019, kutokana na dosari zilizokumba uchaguzi huo.

Nchi iligawanyika vikaliwiki kadhaa kuelekea uchaguzi wa marudio. Malawi ni nchi ya pili kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais kutokana na hitilafu katika mchakato wa uchaguzi, baada ya Kenya kufanya hivyo maka 2017.

Baada ya matokeo ramsi kutangazwa usiku wa Jumamosi Juma, Bw. Chakwera alisema ushindi wake ni " ushindi kwa demokrasia na haki" na kuongeze kusema: "Roho yangu imejaa furaha."

Wafuasi wake walimiminika katika barabara za mji mkuu wa Malawi, Lilongwe, kushangilia ushindi wao baadhi wakipiga honi za gari na wengine kufyatua fataki. Bw. Chakwera anatarajiwa kuapishwa leo Jumapili.

Ushindi huu unamaanisha nini?
Tukio hili lina umuhimu mkubwa katika historia ya siasa nchini Malawi, na linaonesha wadi kwamba mahatma na time ya uchaguzi hazikuwa tayari kushinikiza kufanya maamuzi kwa kwa maslahi ya ofisi ya rais.

Rais Peter Mutharika
Maelezo ya picha: Rais anayeondoka madarakani Peter Mutharika ameutaja uchaguzi wa Jumanne kuwa mbaya zaidi uliowahi kushuhudiwa nchini Malawi

Sio mara ya kwanza mahakama ya katiba katika taifa la Afrika kufuta uchaguzi wa urais - Tukio sawia na Malawi lilifanyika nchini Kenya miaka michache iliyopita - lakini mgombea wa upinzani aliiondoa katika duru ya pili ya uchaguzi katika hatua ambayo ilimpatia ushindi bila jasho Rais Kenyatta.

Ushindi wa Peter Mutharika mwaka jana ulifutwa na mahakama ya katiba baada ya ushahidi kuonesha kuwa uchaguzi wa mwaka jana yalichakachuliwa.

Chanzo: BBC Swahili
 
Hatimaye tume ya taifa ya uchaguzi ya Malawi imemtangaza rasmi mgombea wa upinzani mr Chakwera kuwa mshindi wa kiti cha urais kwa asilimia 58% ,upepo mzuri Afrika kwa wapinzani mwaka huu.

IMG_20200628_175900.jpg
 
Wapinzani wenye hawako prepared kuendesha nchi, Kwa sasa CCM chini ya magufuli inatutosha sana kwa hii miaka mitano iliyobaki, 2025 Upinzani mkiwa serious tunaweza kuwafikiria ila sio sasa yani uwape nchi watu kama nyalandu, lissu au Mbowe huo ni uwende wàzimu kabisa
 
Kweli majina huumba. Naona jamaa kafufuka kutoka kifo cha kisiasa kama alivyofufuka yule Lazaro wa Bibliia! Tuwe makini tuchaguapo majina ya wana wetu!
 
Demokrasia acheni iitwe demokrasia Rais mstaaf wa malawi P.Mutharika alijenga sana mabarabara ya lami na kusambaza umeme vijijini,pamoja na kusambaza mabomba ya maji safi.Lakini leo kakubali kuachia bila ya vurugu wala tatizo ila huku tz mtu utamkuta anang`ang`ana aendelee kua madarakani kisa amefamnya vitu kama hivo hapo juu as if alitoa fedha mfukoni mwake...kuna vingi vya kujifunza uchaguzi wa Malawi.
 
Back
Top Bottom