Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,862
Mwanga wa siasa ya Lazarus Chakwera ulifufuliwa baada ya mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka jana
Kiongozi wa upinzani nchini Malawi Lazarus Chakwera ameshinda duru ya pili ya uchguzi wa urais, maafisa wanasema.
Alimshinda rain aliyekuwa rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kwa sailimia 58.57 ya kura Katina uchaguzi wa Jumanne, tume ya uchaguzi ilitangaza usiku wa Jumamosi.
Mwezi Februari, Mahakama ya katiba nchini Malawi ilifutilia mbali ushindi wa Mutharika' katika uchaguzi wa Mei 2019, kutokana na dosari zilizokumba uchaguzi huo.
Nchi iligawanyika vikaliwiki kadhaa kuelekea uchaguzi wa marudio. Malawi ni nchi ya pili kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais kutokana na hitilafu katika mchakato wa uchaguzi, baada ya Kenya kufanya hivyo maka 2017.
Baada ya matokeo ramsi kutangazwa usiku wa Jumamosi Juma, Bw. Chakwera alisema ushindi wake ni " ushindi kwa demokrasia na haki" na kuongeze kusema: "Roho yangu imejaa furaha."
Wafuasi wake walimiminika katika barabara za mji mkuu wa Malawi, Lilongwe, kushangilia ushindi wao baadhi wakipiga honi za gari na wengine kufyatua fataki. Bw. Chakwera anatarajiwa kuapishwa leo Jumapili.
Ushindi huu unamaanisha nini?
Tukio hili lina umuhimu mkubwa katika historia ya siasa nchini Malawi, na linaonesha wadi kwamba mahatma na time ya uchaguzi hazikuwa tayari kushinikiza kufanya maamuzi kwa kwa maslahi ya ofisi ya rais.
Sio mara ya kwanza mahakama ya katiba katika taifa la Afrika kufuta uchaguzi wa urais - Tukio sawia na Malawi lilifanyika nchini Kenya miaka michache iliyopita - lakini mgombea wa upinzani aliiondoa katika duru ya pili ya uchaguzi katika hatua ambayo ilimpatia ushindi bila jasho Rais Kenyatta.
Ushindi wa Peter Mutharika mwaka jana ulifutwa na mahakama ya katiba baada ya ushahidi kuonesha kuwa uchaguzi wa mwaka jana yalichakachuliwa.
Chanzo: BBC Swahili