Nakubaliana nawe ktk mambo yote isipokuwa hapo uliposema kuna mkono/mikono ya watu. Huu mgogoro huu ulikuwepo toka wakati wa uhuru kwa hiyo hatuwezi kusingizia mikono ya watu isipokuwa viongozi walizembea sana maana nao hawakuona umuhimu wa kulinda mpaka wetu ndani ya ziwa waliwaacha wamalawi wavue samaki upande wa Tz bila hata kuulizwa halafu leo wanajifanya wanaujua mpaka. Tunagharamia majeshi halafu tunakwepa kuyatumia mpaka pale tu maslahi ya wachache wanaoingia mikataba kwa niaba ya watz. Kama wangekuwa na uchungu na raslimali zinazowanufaisha wengi wangekuwa wamedhibiti wizi wa samaki uliofanywa na wamalawi kwa miaka mingi. Malawi wameona kuna udhaifu wa uongozi ktk Tz ndo maana wanataka wapandishe presha ili TZ itetereke maana wanajua CCM kwa sasa haina uhakika kama ikiamua vita baadae wataweza kukusanya silaha kutoka kwa wapiganaji, wanahofia isije ikawa baada ya kuipiga malawi kitakachofuata ni kuiangusha ccm.Katika vitu ambavyo tunatakiwa kushikamana ni wakati wa chokochoko ya vita. Sidhani kama una uzalendo kwa haya unayoandika, leo hii TZ ikipigana na Malawi waumiao ni ndugu zetu walioko kule mpakan na wapiganaji wetu, wengine nao tutaumia manake itabidi mambo mengi yasimame kwa ajili ya vita.
Lile ziwa tunahitaji strategy kubwa mno kumaliza huo mgogoro ambao haujaanza leo. SADC na AU wameshaelezwa, UN pia. Mazungumzo wamalawi wamejitoa, sababu mojawapo ni kutolewa ramani mpya ikionesha mpaka unapita kati ya Ziwa. Hii ni sababu ya kitoto mno, manake ramani zote za TZ zilikuwa zikionesha huo mpaka, sasa kwa nini tutoe ramani mpya mpaka tusiuoneshe?. Tumewapiga bao la kwanza wao kujitoa katika mazungumzo, bao la pili wanaanza wao kumfukuza Balozi wetu. Kama wanajianzaa kwa vita, sisi kwa itifaki tutawaacha mbali mno hivyo kuweza kutumia nchi nyingine kuwadunda.
Hivyo nakusihi, kwa hili hata kama unamchukia JK, unahitaji kuonesha uzalendo kwa nchi yako. Kumbuka chokochoko hizi ni kwa mafuta ya Ziwa Nyasa tu yanayotafutwa, zitakuja nyingi sana utakaposikia kuwa na Baharini kuna mafuta. Usidhani Malawi wanayofanya wameamua tu, kuna mkono/mikono ya watu. TAFAKARI.
Automatically we will have to expel Malawi's ambassador as well in retaliation!
Ati ndio mnataka kuunda AFRIKA MOJA na viongozi wenyewe ndio kama hawa..
Balozi si yule aliyekuwa anashindana na Dr.Slaa Karatu Patrick Tsele kama sikosei...