Ni kweli kondoo anawachunga mpka na kuwagonowa.
hakuna vita vinavyopigana na upande mmoja ukawa unaushindi peke yake. hata vita ambayo MUNGU aliwapigania waisrael kwa waamaleki ilikuwa musa akishusha mikono waisrael wanapigwa; ukipata nafasi unaweza kuangalia kutoka 17:8-13 na hawa ndio waliokuwa wanaongea na MUNGU mojakwa moja itakuwa watumishi na wachungaji?
ikumbukwe kuwa hawa watu hawatoki toka mbinguni ni watoto wetu waliozaliwa kwenye familia zetu ambazo zingine zinaufukara wa kumcha MWENYEZI MUNGU lakini huinua mtumishi wake katika udhaifu huo.
mara nyingi nasema kabla ya kuwahukumu watu hebu tujitazame sisi tumezini na wangapi? vaa viatu vya mwalasusa na ukapewa utajiri wote ikiwa ni pamoja na wanawake wa dar(wachache wasio waaminifu) ambao muda mwingi wanawaweka kwenye mitego wachungaji wewe unge fanyaje? hivyo ni swala la udhaifu wa kibinadamu lakini naimani hufanya toba na MUNGU humsamehe wakati sisi tukiendelea kulalamika.
1samwel2:1-10
Namshangilia Mwenyezi-Mungu moyoni mwangu.
Namtukuza Mwenyezi-Mungu aliye nguvu yangu.
Nawacheka adui zangu;
maana naufurahia ushindi wangu.
2“Hakuna aliye mtakatifu kama Mwenyezi-Mungu;
hakuna yeyote aliye kama yeye;
hakuna aliye mwamba kama Mungu wetu.
3Acheni kujisifu,
acheni kusema ufidhuli.
Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu.
Yeye huyapima matendo yote.
4Pinde za wenye nguvu zimevunjika.
Lakini wadhaifu wanaendelea kupata nguvu.
5Wale ambao zamani walikuwa na chakula tele,
sasa wanaajiriwa ili wapate chakula.
Lakini waliokuwa na njaa,
sasa hawana njaa tena.
Mwanamke tasa amejifungua watoto saba.
Lakini mama mwenye watoto wengi,
sasa ameachwa bila mtoto.
6Mwenyezi-Mungu huua na hufufua;
yeye huwashusha chini kuzimu
naye huwarudisha tena.
7Mwenyezi-Mungu huwafanya baadhi wawe maskini,
na baadhi wawe matajiri.
Wengine huwashusha,
na wengine huwakweza.
8Huwainua maskini toka mavumbini;
huwanyanyua wahitaji toka majivuni,
akawaketisha pamoja na wakuu,
na kuwarithisha viti vya heshima.
Maana, minara ya dunia ni ya Mwenyezi-Mungu;
yeye ameisimika dunia juu ya minara yake.
9“Maisha ya waaminifu wake huyalinda,
lakini maisha ya waovu huyakatilia mbali gizani.
Maana, binadamu hapati ushindi kwa nguvu zake.
10Maadui wa Mwenyezi-Mungu watavunjwa vipandevipande;
atanguruma dhidi yao kama radi mbinguni.
Mwenyezi-Mungu ataihukumu dunia yote;
atampa nguvu mfalme wake
ataukuza uwezo wa mteule wake.”