Malasusa ajitetea Halmashauri Kuu KKKT, akataliwa

Malasusa ajitetea Halmashauri Kuu KKKT, akataliwa

Hebu niambieni huo uchaguzi dayosisi ya mashariki na pwani unaendaje
 
Ukiona watu ndani ya dini wanagombana ...basi ujue hali ni mbaya sana...kuliko tunavyofikiri.....maana wao wanaishi....kiroho...zaidi kuliko kimwili
 
Malasusa ni jipu ambalo mlilea wenyewe muda mrefu

Taarifa kamili ipo kwenye link hii hapa chini.

Kwa ufupi ni kwamba Ask Malasusa alijitahidi kujitetea ndani ya Halmashauri ya KKKT kwa kusema:

1. eti "aliona tayari waraka huo umesambaa vya kutosha kwenye mitandao ya kijamii."

2. eti siyo yeye aliyetoa katazo kwa wachungaji wa dayosisi yake kutousoma waraka huo, bali aulizwe aliyetoa katazo hilo.

Hata hivyo, utetezi huo wa Ask Malasusa haukuliridhisha Baraza la Maaskofu na hivyo likatangaza kumtenga na masuala yote yanayohusu baraza hilo.

=========

UAMUZI wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kumwadhibu kwa kumtenga Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa kwa tuhuma za usaliti, huenda ukamweka katika wakati mgumu zaidi ikiwa hata kuupoteza uaskofu, iwapo hatatimiza sharti la kuomba msamaha.

Jana gazeti dada la hili la MTANZANIA Jumamosi, liliripoti habari za ndani, likieleza kiini cha tuhuma hizo za usaliti dhidi ya Askofu Malasusa, kinaelezwa ni uamuzi wake wa kuzuia waraka wa Pasaka ulioandaliwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo, usisomwe katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani anayoiongoza.

Inaelezwa taarifa za uamuzi huo, ulitangazwa pia kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya KKKT cha siku mbili, ambacho nacho kilikuwa kikifanyika mkoani Arusha sanjari na kile cha Baraza la Maaskofu na kuhudhuriwa na wajumbe wake, ambao ni maaskofu, makatibu wakuu wa dayosisi zote 25 na wakuu wa vitengo.

Jana kwa mara nyingine tena, MTANZANIA Jumapili lilimtafuta Askofu Malasusa ili kufahamu iwapo ataliomba kanisa msamaha kama alivyoelekezwa na kikao hicho cha Baraza la Maaskofu baada ya kupewa muda wa kujitafakari, hadi ifikapo Septemba, lakini hakupatikana.
 
Back
Top Bottom