Malaria sugu inanitesa! Dawa gani itanipa tiba ya kudumu?

Nguli una uhakika ulipewa dawa ya Artemisinin? Chungu? Tangu nianze shiriki katika tafiti za dawa za jamii ya Artemisinin mwaka 2002 sijaona dawa ya jamii hiyo 'chungu'. Jaribu kucheck, sidhani kabisa kama ulipewa jamii ya Artemisinin.

Nilishawahi kutumia Artemisinin, hilo la uchungu ndo kwanza nalisikia toka kwa Nguli, nawaza alipewa aina ingine ya dawa na si Artemisinin.
 
Inawezekana huumwi hata hiyo Malaria. I had the same problem. Kumbe ni aina ya kazi ninazofanya zinanichosha na ninahisi malaria na kumbe hata siyo. Nilikwenda kwa Dr mmoja akanipa ushauri wa maneno, na kuniuliza ninafanya nini. At that time, I was very busy na mambo ya makaratasi. After that ushauri, ikawa malaria ikitokea ninakwenda kupimwa sehem za kueleweka na kutumia dawa ya kueleweka, vyakula na maji kwa wingi. Sasa hivi nina muda mrefu kama miaka 5 sasa nimerelax.

nipo busy na GPA pia, sehemu za kueleweka ni zipi, na dawa ya kueleweka ni ipi? Nijulishe
 
Jamani mwenzenu ni mgeni ktk safu hii, lakini ukweli ni kwamba nahitaji msaada wa juu ya suala hili la malaria. Tangu mwezi wa saba nasumbuliwa na hii homa, kuna dawa nikitumia nakaa kama wiki moja hivi, halafu hali inarudi tena vilevile. Kila nikienda kupima nakuta nina malaria 2 au 3, tangu mwezi wa saba, haiongezeki wala kupungua zaidi ya hapo. Hivyo wadau kama kuna anayeijua tiba, tufahamishane..!
 
Nenda hospitali kubwa ukaeleze shida yako...usiende samunge wala hospitali za vichochoroni!
 
Mkuu uliwahi kutumia dawa za aina gani? Mbona maelezo yako hayajitoshelezi.
 
Jamani mwenzenu ni mgeni ktk safu hii, lakini ukweli ni kwamba nahitaji msaada wa juu ya suala hili la malaria. Tangu mwezi wa saba nasumbuliwa na hii homa, kuna dawa nikitumia nakaa kama wiki moja hivi, halafu hali inarudi tena vilevile. Kila nikienda kupima nakuta nina malaria 2 au 3, tangu mwezi wa saba, haiongezeki wala kupungua zaidi ya hapo. Hivyo wadau kama kuna anayeijua tiba, tufahamishane..!

Hili swali la muhimu sana. Bila shaka MziziMkavu atatupatia jibu. Tufanye subira
 
Mkuu uliwahi kutumia dawa za aina gani? Mbona maelezo yako hayajitoshelezi.

nimetumia zaidi dawa za hospitalini, nilianza na Alu, nikaja quinin, nilipata nafuu wiki mbili tu hali ikarudi tena, nikaja metacaphline na mwisho nikatumia antiquine.
 
Jamani mwenzenu ni mgeni ktk safu hii, lakini ukweli ni kwamba nahitaji msaada wa juu ya suala hili la malaria. Tangu mwezi wa saba nasumbuliwa na hii homa, kuna dawa nikitumia nakaa kama wiki moja hivi, halafu hali inarudi tena vilevile. Kila nikienda kupima nakuta nina malaria 2 au 3, tangu mwezi wa saba, haiongezeki wala kupungua zaidi ya hapo. Hivyo wadau kama kuna anayeijua tiba, tufahamishane..!
Jaribu kutumia dawa yangu hii Pata kijiko kimoja cha Asali Safi mbichi ya nyuki uchanganye na kijiko kimoja cha Siki ya Apple(Applle Vinegar) au Siki ya Zabibu uwe unakunywa asubuhi kila siku kabla kula kitu Tumia hii Dawa kwa muda wa mwezi Mmoja itakusaidia kuondosha hiyo Malaria yako Sugu.

Au Tumia Dawa hii Pata ndimu30 uzikamuwe uzitie kwenye chupa moja kisha hiyo chupa uiweke kwenye jua siku 3 baada ya siku 3 uanze kutumia kila siku unywe kipimo cha kikombe cha kahawa Asubuhi kabla ya kula kitu mpaka umalize hiyo chupa utakuwa umeshapona, kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu inshallah. Jaribu kutumia moja kati ya hizi dawa.
 
Jamani mwenzenu ni mgeni ktk safu hii, lakini ukweli ni kwamba nahitaji msaada wa juu ya suala hili la malaria. Tangu mwezi wa saba nasumbuliwa na hii homa, kuna dawa nikitumia nakaa kama wiki moja hivi, halafu hali inarudi tena vilevile. Kila nikienda kupima nakuta nina malaria 2 au 3, tangu mwezi wa saba, haiongezeki wala kupungua zaidi ya hapo. Hivyo wadau kama kuna anayeijua tiba, tufahamishane..!

Pole Dogo Lao....Hii issue ya Malaria sugu inachanganya sana watu na madaktari, hasa kutokana na mgonjwa anavyojieleza. Ni vyema kama mgonjwa yuko ana kwa ana na daktari akamuuliza maswali ili kubaini kama kweli ni Malaria sugu au la.

Kuna vitu watu wanachanganya...kuna Malaria Sugu (sio yule wa jukwaa la siasa), maana yake Malaria imethibitika kwa vipimo (hasa hadubini/microscopy) na kutibiwa kwa dawa sahihi (Mseto au Quinine) na kumaliza dose lakini kipimo cha hadubini kikaonyesha bado wadudu wa Malaria wapo kwenye damu.

Au kuna Malaria new infection (maambukizo mapya) umepata muda si mrefu baada ya kutumia na kumaliza dozi sahihi ya dawa sahihi ya Malaria kwa kurudia maisha yako ya kutojilinda na Malaria.

Au ni tatizo jingine ambalo dalili zake zinafanana na za Malaria lakini si Malaria na hospitali wanashindwa kuthibitsha hilo wanabaki kusingizia Malaria (ili wauze dawa, hii ni common sana kwenye hospitali binafsi, ukipima Malaria mara nyingi utakuwa nayo hata kama ni homa ya mafua!).

Sasa basi....kabla hujasema ni Malaria Sugu (ambayo siamini kama una Malaria Sugu, tangu mwezi wa saba ungekuta tushakuzika (samahani lakini ndio ukweli)), ni vyema ucheck mlolongo mzima wa kuugua kwako tangu huo mwezi wa saba mpaka sasa...una dalili gani, ukaenda hospitali zipi, ukafanyiwa kipimo kipi cha Malaria, ukapewa dawa zipi, ukabadilishiwa na kupewa dawa zipi, ulitumia dozi na kumaliza kama ulivyoshauriwa, ulijisikia afadhali kwa siku kadhaa kabla ya dalili kurudi tena, unajikinga na Malaria? Majibu ya maswali hayo yatathibitisha ni Malaria sugu, au new infection, au ni tatizo jingine na sio Malaria kabisa!

Dawa ya kutibu Malaria (uncomplicated) kwa sasa zenye ufanisi bora kuliko zote duniani ni mseto (Artemisinin Combined Therapy ACT), hapa kwetu kuna ALu (Coartem), DuoCotexcin na brand nyingine kadhaa. Je ulitumia mseto na kumaliza dozi kama ulivyoshauriwa? Bado Tabia ya watu kwenda hospitali na kupewa SP hasa Metakelfin ipo sana, hii dawa ilishashindwa kutibu Malaria kwa kiwango kikubwa sana mpaka kutolewa kwenye muongozo except kwa kina mama wajawazito tu.

Dawa ya kutibu Malaria Kali (complicated) na Malaria Sugu ni aidha dawa za Artemisinin za kuchoma sindano mfano Artemether au Artesunate, au dawa ya kuchoma sindani au dripu ya Quinine. Ambazo unatumia kwa siku chache au kadhaa, kisha unamalizia na dozi nzima ya mseto. Je, ulishawahi kutibiwa hivyo?

Kama majibu ya maswali yangu hayo mawili ni ndio, na bado maabara (yenye technician wa kuaminika) zilionyesha una wadudu wa Malaria kwenye damu...basi una Malaria Sugu, na unapaswa kupelekwa India kwa matibabu badala ya Zitto.
 
Dawa yake piga BAN mfululizo,
Piga mpaka IP-Ban kwenye Simu au PC anayotumia hata kama ni ya Internet Cafe, ukishtukia ID zake zingine nazo piga BAN zote pia,
Anaemtetea nae piga BAN.
Hapo hutokaa usikie Malaria Sugu wala wale jamaa zake wengine kina nani Sijui!!!
 
Wakuu naomba msaada wa tiba ya malaria sugu tangu ujana wangu hadi leo nakaribia 50yrs nimekuwa nauguwa na kutibu malaria kila mwezi, tangu wakati wa chroloquine, fansider, Halfan,Metakhafin, Amodiaquine, mseto,,,,dawa za asili mshana, mwarobaini, soku-masai, n.k kwa yeyote atakae niwezesha kukaa angalau kila baada ya mwaka mmoja naahidi kutoa zawadi nono shs 100,000 hadi shs 2,000,000.

Nimekuwa na mawazo kuwa immunity yangu kwa malaria ni very weak, sababu sijasumbuliwa na magonjwa mengine labda kdg tonslitis kwa mwaka x2, minyoo x3 kwa mwaka, Mafua ndio mara kwa mara kila dalili za malaria tu

Swali langu je pana namna yeyote ya kuongeza immunity(kinga) ya mwili hasa dhidi ya malaria ?
 
Mzizimkavu, tunahitaji msaada wako kwa hili kwani tatizo hili hata mie ninalo. Haiwezi pita miezi 6 bila Malaria!!

Jamani hata mimi huwa haipiti miezi miwili lazima nimeze dawa,nilimuuliza doctor mmoja niepukana vipi na hali hii akanipa jibu kuwa so long as the mosquitoes are there you can not escape the disease,labda kama nitaamua kwenda kuishi ulaya.
 
NILIELEKEZWA HIYI DAWA NA PROF MMOJA WA KIHINDI KTK CHUO NILICHOSOMA UNDERGRADUATE MIAKA YA TISINI,NA NIMESHAWAELEKEZAWATU WENGI SANA! NAKUELEKEZA BUREEEE!TENA DAWA INAUZWA HADI KATIKA PHARMACY ZA WAHINDI!inaitwa ZANDU!ukiinunua niambie nikuelekeze jinsi ya kuitumia ili malaria isirudirudi tena kwako.ni dawa ya asili ya wahindi na inatibu magonjwa mengi sana hata typhoid,amoeba n.k,nk
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom