Malaria sugu inanitesa! Dawa gani itanipa tiba ya kudumu?

Kuna mtu kaipta duka gani hapa Dar.....nimeuliza mjini wahindi kadhaa wanasema hawana
 
Wakuu naomba msaada wa tiba ya malaria sugu tangu ujana wangu hadi leo nakaribia 50yrs nimekuwa nauguwa na kutibu malaria kila mwezi, tangu wakati wa chroloquine, fansider, Halfan,Metakhafin, Amodiaquine, mseto,,,,dawa za asili mshana, mwarobaini, soku-masai, n.k kwa yeyote atakae niwezesha kukaa angalau kila baada ya mwaka mmoja naahidi kutoa zawadi nono shs 100,000 hadi shs 2,000,000.

Nimekuwa na mawazo kuwa immunity yangu kwa malaria ni very weak, sababu sijasumbuliwa na magonjwa mengine labda kdg tonslitis kwa mwaka x2, minyoo x3 kwa mwaka, Mafua ndio mara kwa mara kila dalili za malaria tu

Swali langu je pana namna yeyote ya kuongeza immunity(kinga) ya mwili hasa dhidi ya malaria ?

Kwa kukurupuka naweza sema kwa uhakika 'siamini' kuwa tatizo lako ni Malaria, hakuna mtu anaugua Malaria sugu tangu ujana, japo sijui sasa una umri gani..lakini naweza kisia ni miaka mingi umekuwa ukiugua. Lakini pia jua kuwa kwa kuishi sehemu yenye Malaria kwa wingi (Malaria endemic area), si lazima kila illness episode basi ni Malaria, unaweza kuwa ukawa unaugua magonjwa/ugonjwa mwingine pia lakini unang'ang'ania ni Malaria.

Kabla hujaita ugonjwa ni 'Malaria Sugu', kuna vigezo inabidi vitimie:

1. Umepima kwa kipimo cha 'Malaria Blood Slide' (Gold Standard for Malaria Diagnosis) kikifanywa na qualified Lab Technician, na akona wadudu wa Malaria
2. Ukatumia dawa sahihi (iwe Chloroquine kwa enzi hizo, au SP wakati wa era yake, au sasa ARTs (Mseto), kwa dozi sahihi kulingana na uzito/umri wako, na ukatumia dozi kama ulivyoshauriwa na kumaliza
3. Ukapima tena Malaria baada ya kumaliza dozi na bado wadudu wa Malaria wakaonekana

Kifupi cha hapo juu...bado hujaita ugonjwa ni 'Malaria Sugu'! Jiulize kama mara zote hizo ulizougua tangu ujana ulienda hospitali ukapimwa Malaria ikaonekana, na ukapewa dawa sahihi na ukamaliza dozi, na bado wadudu wakaonekana baada ya kumaliza dawa.

Wakati mwengine watu huwa wanachanganya 'Malaria Sugu' (old inadequately treated infection)....na 'Malaria Maambukizo Mapya' (new infection after treatment). Ukipata Malaria ikatibiwa, haina maana hutapata Malaria tena kama utarudi kwenye mazingira na tabia zako zinazokuweka katika risk ya kupata Malaria. Kinachotokea ni mtu anapata Malaria, inatibiwa, hacheck kama imetibika yoote baada ya dozi, anarudi kwenye mazingiara na tabia zake za kutojilinda na Malaria, anapata maambukizi mapya ya Malaria, akirudi hospitali kupima na kuambiwa ana malaria...anaiita 'Malaria Sugu'! Hiyo si Malaria sugu, bali ni new infection kutokana na kutojilinda na Malaria. Je wewe unajilinda na Malaria tangu huo ujana wako?

Au inawezekana pia ukawa unasumbuliwa na ugonjwa mwingine ambao si Malaria, na labda unaenda kwenye dispensary (hasa private) ambazo capacity yake ni ndogo, lakini wanataka kutengeneza hela toka kwako...wanapima hawaoni kitu lakini for the sake of selling medicines wanakuambia una Malaria, wengine wanaambiwa na daktari kabisa kuwa wana Malaria Sugu (jaribu kumdadisi, ana maana gani akikuambia una Malaria Sugu?)...ulijaribu kubadili hospitali/madaktari tangu enzi hizo za ujana wote wakakupima na kukupa majibu hayo hayo ya Malaria Sugu?

Watu tunaoishi katika maeneo yenye Malaria (Malaria Endemic areas) huwa tunapata aina fulani ya kinga (natural immunity) dhidi ya Malaria. mara nyingi hii hudevelop kwa watu wanaoishi maeneo hayo tangu utoto, na wakaugua Malaria mara kadhaa utotoni. hata hivyo, si kila mtu aishiye kwenye hayo maeneo atapata natural immunity hiyo. We umezaliwa na kuishi utoto wako hapa kwetu (Tanzania) hasa sehemu za Pwani, Morogoro, kanda ya Ziwa...mara chache unapata immunity hiyo sehemu za Nyanda za juu (kusini na kaskazini) na sehemu za baridi sana, kwa sabau huko rate ya kuugua Malaria ni ndogo.

Jiulize hayo maswali kabla hujajivika ugonjwa wako 'Malaria Sugu' ....chunguza, usije kuta una tatizo kubwa kuliko hilo la Malaria, ukalizembea kwa kuridhika kuwa ni malaria sugu tu!

NB: Namna nyingine ya kuongeza kinga dhidi ya ugonjwa (zaidi ya natural immunity) ni kwa kutumia chanjo. Chanjo ya Malaria haijathibitishwa bado, japo imeonyesha matokeo mazuri katika majaribio. Kwa sasa hamna chanjo, hivyo hamna namna ya kuongeza immunity dhidi ya Malaria, zaidi ya natural immunity.
 
Mi sijawahi umwa malaria toka 2001 na hiyo najua inachangia pia kwa vile sijaishigi africa kwa mda mrefu nahisi siku nikipata malaria naona nitalazwa hospitali
 
NILIELEKEZWA HIYI DAWA NA PROF MMOJA WA KIHINDI KTK CHUO NILICHOSOMA UNDERGRADUATE MIAKA YA TISINI,NA NIMESHAWAELEKEZAWATU WENGI SANA! NAKUELEKEZA BUREEEE!TENA DAWA INAUZWA HADI KATIKA PHARMACY ZA WAHINDI!inaitwa ZANDU!ukiinunua niambie nikuelekeze jinsi ya kuitumia ili malaria isirudirudi tena kwako.ni dawa ya asili ya wahindi na inatibu magonjwa mengi sana hata typhoid,amoeba n.k,nk

mkuu,ngoja niitafute hapa Mwanza nikiipata tu ntakutafuta unielekeze.
 
Wakuu tunawashukuru wote waliotoa michango yao ya mawazo na ushauri lakini bado tunahitaji misaada hiyo zaidi na hasa ya kitaalam, TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU

ukisema ya
kitaalam ina maana wanataaluma watahusika zaid hapa,mm si mtaalam ila nlikuwa naumwa malaria mara 2 smtimz had3 kwa mwez,nmetumia dawa zote zkashndwa,nkaacha kutumia dawa,tangu hapo mpaka leo cjawah
kutumia dawa na malaria n adim kwang,wataalam hii imekaaje?
 
Mwombe Mungu ndo daktari wa madaktari! Huyo hashindwi na lolote! Nategemea kurushiwa Hilo donge!
Nakubaliana na wewe, mimi hiyo hali ilinkumba na kuniendesha kwa muda. Ilifikia kipindi nikawa nakunywa dawa in advance. Ila nilipochoka nikamuomba MUNGU na kumuambia sitaki tena utumwa wa malaria na malaria sio ugonjwa wangu. Tangu kipindi hicho inaweza ikapita mwaka nikaugua malaria kwa mbaaali tena mara moja
Thanks to GOD
 
Wakuu naomba msaada wa tiba ya malaria sugu tangu ujana wangu hadi leo nakaribia 50yrs nimekuwa nauguwa na kutibu malaria kila mwezi, tangu wakati wa chroloquine, fansider, Halfan,Metakhafin, Amodiaquine, mseto,,,,dawa za asili mshana, mwarobaini, soku-masai, n.k kwa yeyote atakae niwezesha kukaa angalau kila baada ya mwaka mmoja naahidi kutoa zawadi nono shs 100,000 hadi shs 2,000,000.

Hupima kuhakiki ni malaria kabla matibabu, pia namshukuru mungu sijawahi kulazwa kwa malaria, naomba msaada hata wa ushauri tu.

Nimekuwa na mawazo kuwa immunity yangu kwa malaria ni very weak, sababu sijasumbuliwa na magonjwa mengine labda kdg tonslitis kwa mwaka x2, minyoo x3 kwa mwaka, Mafua ndio mara kwa mara kila dalili za malaria tu

Swali langu je pana namna yeyote ya kuongeza immunity(kinga) ya mwili hasa dhidi ya malaria ?

Pole sana mkuu naamini watakusaidia kwani tuna DRs wengi sana.
 
mkuu ni pm,kuna dawa toka kijijini ni komesha!unakunywa na chai ya rangi.malaria kwangu historia
 
mkuu ni pm,kuna dawa toka kijijini ni komesha!unakunywa na chai ya rangi.malaria kwangu historia

Mkuu upo mkoa gani? Mimi nipo mwanza, naweza kupata hiyo dawa. Wenye matatizo na malaria isiyosikia dawa tupo wengi
 
Tafiti zinaonesha 40% ya dawa africa ni feki na ili huchangia usugu wa malaria
Kuna dawa niliwai pewa na mmsai mmoja ni mzizi unatafuna ilikuwa ifakara nilidunda mwaka bila malaria sasa tatizo amefariki na mwanae iyo dozi haijui shida tupu
On a serious note malaria so kuna watu kila mwezi wagonjwa
Bongolala nimekupm jibu basi
 
Hili ni tatizo la wengi mi dawa yangu ilikuwa metakeflin nakaa miaka bila kuugua malaria lakini baadaye zikanichoka zikawazinibabua sasa natumia alu kila mwezi .tusaidien wenye dawa za uhakika
 
ASANTE SANA RIWA
Nashukuru sana mkuu kwa mchango wako wa kitaalamu na hasa ufafanuzi wa neno "sugu" kwa maana hiyo sio sugu sbb ninapoumwa mara nyingi hupima naa kuthibitisha kuwa nuina wadudu wa malaria then napewa dawa na kuitumia kama nilivyoagizwa na dr nakukamilisha dose baada ya hapo ninapima tena na kuthibitisha kuwa nimepona/wadudu hawapo kabisa kwa mara nyingi na dawa nyingi hutibu na kumaliza wadudu,,,, tatizo kama ulivyosema haichukui muda tu unajikuta una wadudu tena yawezekana hata baada ya wiki 3 au hata 2 tu, hii inatujengea fikra kuwa labda wadudu hawakuisha kabisa mwilini au kama wasemavyo kuwa wanaweza jificha kwenye maini au mifupa ndio maana ya neno sugu kutumika,,,,,,
Kuhusu maeneo ya kuzaliwa na kuishi ni kweli mm ni mzaliwa wa kanda ya ziwa penye mbu wengi na muda mrefu nimeishi huko kwa sasa niko pwani, nadhani yawezekana nikawa na kiasi tu cha kinga..
Na pia kuhusu aina nyingine za magonjwa hilo liko waazi kwa binadamu yeyote anapokuwa na tatizo na hasa la muda mrefu lazima atakwa na mawazo kama hayo nimekuwa several times nikihisi vitu vingi sana kwa muda huo wote na madaktari wakifanya uchunguzi lakini bado sijapata tatizo lingine linaloweza changia ila hofu yangu ni kuwa hali hi ndio inaweza niletea matatizo mengine naamuomba mwenyezi mungu anilinde kwa hilo..
hasa ukitambua kuwa muda wote ninaishi mjini na miji ya mkoa ambapo matibabu yanapatikana kwa urahisi kulinganisha na vijijini.
 
Basi wewe unapata recurring infections. Usikae mahali kuna mbu especially usiku (heh!!, nimemmiss Mbu jamani)
Tumia anti-mosquito repellent. Kuna nzuri tu unaweka mfukoni wakati unatoka. Zinasaidia haswaa!
 
Last edited by a moderator:
Jamani mradi wa kutokomeza malaria haona tija ? umeishia wapi ? kwa wale wenzetu walioko maeneo yaliyonyunyizia dawa za huo mradi kuna mafanikio yeyote ? tunaomba taarifa tafadhali ili tuhamie huko ! ! !
 
Na mimi ni mgeni hapa jamvini, ni kweli malaria inasumbua sio mchezo. Kila siku unajisikia kama mwili wako umevaliwa. Mnaojua dawa tafadhali mtusaidie.
 
Hata mim pia ilikua baada ya miez miwl lazma niugue bt toka ninywe dawa ya antiquen ni ant malaria hyo cjaugua na karibia mwaka sasa zipo aina mbili yenzie nimeisahau jina zinaendan bei 11000-15000 kwnye maduka ya dawa dar bt cjajua other places jaribt kuitafuta yaweza kukusaidia kama mimi
 
Tafiti zinaonesha 40% ya dawa africa ni feki na ili huchangia usugu wa malaria
Kuna dawa niliwai pewa na mmsai mmoja ni mzizi unatafuna ilikuwa ifakara nilidunda mwaka bila malaria sasa tatizo amefariki na mwanae iyo dozi haijui shida tupu
On a serious note malaria so kuna watu kila mwezi wagonjwa
Bongolala nimekupm jibu basi


Ni kweli kwamba dawa nyingi ni fake.
Kama walivyochangia wengine, cha kwanza kabisa ni kumuamini na kumuomba Mungu, pili ni kuboresha LISHE na tatu ni kutumia baadhi ya dawa zilizo bora kama alternative ya emergency kutokana na hatua utakayokuwa nayo. Chakula/mlo/ Lishe inaweza kufanya zaidi yale dawa inaweza kufanya tena bila madhara hasi makubwa. Kumbuka dawa nyingi zina madhara hasi mengi.

Kuna dawa iitwayo MALARONE ni nzuri sana na inauzwa kati ya sh Tzs 70,000-100,000 per dose. You may find it in some few medical stores. More info on Malarone can be found here Malarone for malaria
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom