Malaria sugu inanitesa! Dawa gani itanipa tiba ya kudumu?

Kama unakunywa doze na kumaliza kuna haja ya kucheki izo dawa zisije zikawa zimexpire bure as juzi tuu mtu kapewa dawa experied kaumuka mwili mzima.
Nami ilishanitokea kutopona malalia nikaenda pima typhoid ikaonekana ninayo so nikaanza dose ya typhoid kwanza bse nasikia otherwise huponi.
Za kienyeji kuna mtu alinambia SHUBILI ni dawa nzuri waweza jaribu
 
Jaribu kutengeneza chai ya rangi bila sukari then kamulia limao zima kisha kuywa halafu utupe matoke
 
Kama unakunywa doze na kumaliza kuna haja ya kucheki izo dawa zisije zikawa zimexpire bure as juzi tuu mtu kapewa dawa experied kaumuka mwili mzima.
Nami ilishanitokea kutopona malalia nikaenda pima typhoid ikaonekana ninayo so nikaanza dose ya typhoid kwanza bse nasikia otherwise huponi.
Za kienyeji kuna mtu alinambia SHUBILI ni dawa nzuri waweza jaribu

nitajaribu mkuu, nadhani dawa za 'kisasa' hazitaki kunitendea haki, ila sijajua inatumikaje
 
Afadhali wewe ndugu umepona kwa ALU. mimi nimeshatumia mara tatu. imedunda kabisa. mara ya pili kutumia nilikaa mwaka bila kutumia dawa ya malaria ila ilinipata tena na nilipotumia ALU ikawa bila bila. Kuna dawa inaitwa MUSHANA inapatikana hapo ubungo plaza nataka nianze kuitumia hiyo

Yawezekana licha ya kutumia ALu, lakini huchukui tahadhali dhidi ya malaria. Tumia chandalua chenye matundu madogo sana kisha kifue kwa kutumia Ngao. Hili lifanyike kila ufuapo, weka ngao. Usidanganyike na maelezo kuwa kuna Ngao ya muda mrefu.

Pia hakikisha kuwa mazingira yanayozunguka makazi yako hayana miti na kama yanayo basi hakikisha kuwa unafanya Fumigation japo mara 1 kila baada ya miezi 6.

Naamini kuwa kwa kufanya hivyo hata hizo dawa unazotumia zitafanya kazi.
 
yani ungejua mkuu nilivyo care na hawa parasites. Usiku niko makini sana pia mchana. Ni immune tu nadhani iko compatible na hawa plasmodiam
 
HESHIMA kwenu Wakubwa.
Naomba munisaidie kuhusu hili tatizo.Mie nimekuwa ninasumbuliwa na Malaria Kila baada ya mwezi mmoja au miwili lazima niugue Malaria Nimetumia dawa za kutibu Malaria za Aina tofauti pia Sindano lkn wapi.Napona kwa mda tu kisha naumwa tena.Nb Chandarua ninatumia chenye ngao.Pai khs HIV nimeshapima mara kibao, niko safi tu.je hii ni malaria ya kawaida au kuna tatizo?.
Na imani mtanishauri kwa Hekima na Upendo Mkubwa asanteni.
 
Dah, hii madaktari wa hapa jamvini nadhani watakuwa msaada mkubwa kwako. Uwe mpole unaweza usipate jibu zuri kwa sasa kwa kuwa wengi washapumzika. Wasipojibu kesho mapema asubuhi isogeze kwenye NEW POSTS watakujibu tu!
 
Ingawa sio na daktari naweza kukupa kaushauri tu kulingana na uzoefu. Kafanye full blood test, uangalie levels za cells zinazohusiana na kinga za mwili. Pia jaribu kupima magonjwa mengine kama typhoid yana dalili zinazofanana na malaria, kama hujawahi kupima.
 
HESHIMA kwenu Wakubwa.
Naomba munisaidie kuhusu hili tatizo.Mie nimekuwa ninasumbuliwa na Malaria Kila baada ya mwezi mmoja au miwili lazima niugue Malaria Nimetumia dawa za kutibu Malaria za Aina tofauti pia Sindano lkn wapi.Napona kwa mda tu kisha naumwa tena.Nb Chandarua ninatumia chenye ngao.Pai khs HIV nimeshapima mara kibao, niko safi tu.je hii ni malaria ya kawaida au kuna tatizo?.
Na imani mtanishauri kwa Hekima na Upendo Mkubwa asanteni.
Mimi siyo daktari. Maoni yangu ni kwamba kama wewe ni mtu wa viwanja, hasa baa za wazi (grosari kwa Kibongo) au mienendo kama hiyo, uwezekano wako wa kupata malaria mara kwa mara ni mkubwa kwa sababu ya kuumwa na mbu katika mkusanyiko wa watu wengi. Badili tabia inaweza kusaidia.
 
na mwili wa mtu pia una uhusiano? manake mie hukaa miaka sijapata malaria, na ninaoishi nao kila mwezi wanayo malaria
 
teh teh teh

Jamani mimi sina msaada mkubwa kwa kukosa utaalam.. lakini na mimi nina tatizo hilo pia. Nimeshatumia madawa ya kila aina na kila bei toka nchi mbalimbali. Hospitali zote kubwa nimeenda kutibiwa malaria hii lakini inarudi kila baada ya mwezi mmoja. Labda na mimi ni sababu ya kukaa sana nje usiku (viwanja). Lakini je, hii malaria itufanye tuingie ndani mapema jamani? Nahisi pia madawa yamepoteza nguvu. Sina jibu la moja kwa moja lakini nahofia kabisa.

Pole ndugu yangu. Ukipata tiba na mimi nisaidie.
 
Punguza mapenzi na mbu mara kwa mara!
Masanie...punguza makali ya maneno kidogo leo tupo kisala zaidi...Nenda kaonane na dr. wanaotumia dawa za matuna mmoja yupo magomeni mwingine hapo shekilango karibu na Rombo Green View...
 
Kuna possibilities mbili:
1-Unapopata malaria, matibabu unayopata hayamalizi kabisa vijidudu vilivyomo mwilini. Yaweza kuwa humalizi dozi, au hupati dozi sahihi. Note kwamba vijidudu vya malaria vina mzunguko tofauti mwilini.
2 - Unapata maambukizi mapya kila wakati (huko grocery hehehe, hamia kempiski, japo happy hours tuu), au hutumii chandarua chenye dawa??
Pole. tafuta suluhisho, malaria sio mchezo ndugu,tutakusahau sasa hivi!
 
HESHIMA kwenu Wakubwa.
Naomba munisaidie kuhusu hili tatizo.Mie nimekuwa ninasumbuliwa na Malaria Kila baada ya mwezi mmoja au miwili lazima niugue Malaria Nimetumia dawa za kutibu Malaria za Aina tofauti pia Sindano lkn wapi.Napona kwa mda tu kisha naumwa tena.Nb Chandarua ninatumia chenye ngao.Pai khs HIV nimeshapima mara kibao, niko safi tu.je hii ni malaria ya kawaida au kuna tatizo?.
Na imani mtanishauri kwa Hekima na Upendo Mkubwa asanteni.

una uhakika ni malaria? isije ikawa waswahili washalembea kipapai? malaria kila mwezi duh! marazi ya kila mwezi ni yale ya kinamama tu kwa mujibu wa sayansi.
 
Wana JF naomba msaada wenu, ni takribani mwaka sasa sijawahi kupata nafuu kutokana na huu ugonjwa. Je tatizo hili lipo au ni mimi tu? Nimetumia dawa nyingi, za hospital mpaka mitishamba, huwa napata nafuu ya muda mfupi na ugonjwa unarudi tena. Kwa yeyote mwenye kuijua tiba ya uhakika anijulishe.Nipo DSM, asanteni
 
Hata mama yangu aliugua malaria miaka 3 lakini pona yake alikuwa anakunywa maji, mazoezi na kula vyakula vya asili vyenye uchunguucungu. Baada ya mwezi 1 tu kwa mwendo huu akapona kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom