Malalamiko yangu juu ya CRDB bank

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,451
6,325
Siku ya Leo imekuwa mbaya Sana kwangu,

Nilikuwa natuma pesa Kwa bimkubwa wangu huko kijijini kwetu kwa ajili ya matibabu yake

Nimetuma pesa asubuh kwa SIM banking kwenda mpesa, tangu hiyo asubuh mpaka muda huu hiyo pesa haijafika,

Nimepiga simu Sana huduma Kwa wateja wanasema shida sio crdb ni mpesa, nikipiga simu Vodacom naambiwa shida ni CRDB sio wao

Usiku huu nimepiga tena simu CRDB wananiambia Leo kulikuwa na maboresho ya mfumo wao so pesa yangu itarudi kesho saa 12 jioni

Yan kesho sio Leo usiku hapana kesho tena saa 12 jioni

Sasa hoja yangu, kama wanajua wanafanya maboresho ya mfumo why hawatangazi Kwa sie wateja wao?

Na kama wanaboresha mfumo why wanaruhusu mtu akituma pesa ziende wakati wanajua hazitofika Kwa mlengwa?

Dah imeniumiza sana
 
Ndugu Mteja, kutakua na maboresho ya huduma za Tigo Pesa leo kuanzia saa 7 usiku mpaka saa 9 usiku. Tafadhali fanya miamala yako kabla na baada ya muda huo.
 
Mimi mpaka sasa nimeshatumia zaidi ya Tsh 10,000 ili ninunue kifurushi cha sms cha sh 2000 na imeshindikana.
 
Ndugu Mteja, kutakua na maboresho ya huduma za Tigo Pesa leo kuanzia saa 7 usiku mpaka saa 9 usiku. Tafadhali fanya miamala yako kabla na baada ya muda huo.

Yes walipaswa kutoa taarifa kama hiyo
 
Hata mimi nimecheki hadi mida ya jioni sikupata huduma ya simu banking CRDB, nimeenda kuwauliza wanasema kuna tatizo vodacom maana wenye laini za mitandao mingine wanapata.
 
Halafu wahudimu wa CRDB wana lugha ya ajabu! Mara zote nilizohudumiwa nao lazima wanishurutishe na kuniletea nyodo as if I'm a beggar
 
Pole sana. Ndiyo maana US raia wanasue kila kitu. Ingekuwa mbele ungewapeleka mahakamani kisha unadaka fidia unagawana na lawyer.
 
Alafu wahudimu wa crdb wana lugha ya ajabu! Mara zote nilizohudumiwa nao lazima wanishurutishe na kuniletea nyodo as if I'm a beggar
CRBD Kwa kweli imegeuka Benki ya hovyo sana siku hizi, haya matatizo ya Network ni almost kila siku.. Huduma Kwa Wateja ni ubabe ubabe tu, polite language kwao Hamna kabisa..
 
CRBD Kwa kweli imegeuka Benki ya hovyo sana siku hizi, haya matatizo ya Network ni almost kila siku.. Huduma Kwa Wateja ni ubabe ubabe tu, polite language kwao Hamna kabisa..
Nina mpango wa kutafiti benki yenye unafuu katika hili eneo Kisha nihamishie vijisenti vyangu.
 
Mimi walijaribu kunifanyia hivyo na Tigo, niliwaaambia tuandikishiane mkataba kwamba hiyo pesa wakae nayo lakini kwa riba, ilikuwa ji milioni 1, nikawaambia kwakuwa mmesema mtarudisha baada ya masaa 72 basi haina shida.

Ila nataka 10% intrest kwa kila saa moja mtakayokaa na pesa yangu, kama mnaona hiyo riba ni kubwa basi rudisheni oesanyangu immediately.

kale kadada kusikia hivyo kakapanda juu ghorofani kuongea eti na watu wa systems, kabala hajarudi chini nikapata meseji kwamba pesa yangu imerudishwa, nikicheka sana, Tigo wajinga sana, 😂😂😂, niliondoka kama mbabe flani hivi , 😂😂😂😂
 
CRBD Kwa kweli imegeuka Benki ya hovyo sana siku hizi, haya matatizo ya Network ni almost kila siku.. Huduma Kwa Wateja ni ubabe ubabe tu, polite language kwao Hamna kabisa..

Huduma Kwa wateja ni mbovu mbovu mbovu
 
Maumivu yangu na hiyo bank siyasemi.. Salio nililoacha mara ya mwisho limefyekwa karibia nusu nzima

Hii bank ni magumashi Sana siku hizi Yan sio bank ya kuiamini wakati
Mimi walijaribu kunifanyia hivyo na Tigo, niliwaaambia tuandikishiane mkataba kwamba hiyo pesa wakae nayo lakini kwa riba, ilikuwa ji milioni 1, nikawaambia kwakuwa mmesema mtarudisha baada ya masaa 72 basi haina shida, ila nataka 10% intrest kwa kila saa moja mtakayokaa na pesa yangu, kama mnaona hiyo riba ni kubwa basi rudisheni oesanyangu immediately, kale kadada kusikia hivyo kakapanda juu ghorofani kuongea eti na watu wa systems, kabala hajarudi chini nikapata meseji kwamba pesa yangu imerudishwa, nikicheka sana, Tigo wajinga sana, 😂😂😂, niliondoka kama mbabe flani hivi , 😂😂😂😂

Na mm kesho nataka kwenda crdb nikawasumbue
 
Back
Top Bottom