shakurrakesh
New Member
- Oct 1, 2026
- 1
- 0
Ninaandika haya ili kueleza uzoefu wangu kama mfanyakazi na changamoto nilizokutana nazo katika mchakato wa ajira na kusitishwa kwa mkataba wangu na Talents Solution Company Limited.
Nilikuwa nimeajiriwa kwa mkataba wa mwaka mmoja, ambao kwa mujibu wa mkataba wangu ulipaswa kuendelea hadi 03/11/2026. Hata hivyo, nilisitishiwa ajira kabla ya tarehe hiyo.
Katika kipindi cha ajira yangu, kulikuwa na masuala kadhaa ninayoyaona yanahitaji maelezo na ufafanuzi kutoka kwa mwajiri, ikiwa ni pamoja na:
Ninaomba pia wafanyakazi wengine ambao wamewahi kupitia changamoto zinazofanana na hizi washirikishe uzoefu wao kwa heshima na bila matusi.
Talents Solution Company Limited, kama ina maelezo au ushahidi unaopingana na maelezo yangu, niko tayari kuupokea na kuuweka wazi hapa ili mjadala uwe wa pande zote.
Ninaamini haki ya mfanyakazi kusikilizwa, kupata maelezo ya wazi kuhusu ajira yake na kufuata utaratibu unaotakiwa ni jambo muhimu.
Naweza kuambatanisha nyaraka husika kama mkataba, barua za PIP, extension letter, termination letter na salary slip ili watu waweze kuona ushahidi na kujenga uelewa wao wenyewe.

- Majukumu yangu kubadilishwa kutoka HBB Direct Sales Executive kwenda EBB Direct Sales Executive bila mimi kupewa mabadiliko hayo kwa maandishi.
- PIP ya kwanza ilikuwa ya kipindi cha Januari–Machi 2026. Baada ya kipindi hicho kumalizika, kwa upande wangu sikupokea confirmation letter, warning letter wala performance review iliyoonyesha rasmi matokeo ya PIP hiyo.
- Baadaye nilipewa PIP nyingine ya miezi mitatu, huku barua ya extension ikiwa imeandikwa tarehe 11/03/2026, lakini mimi niliipokea na kusaini tarehe 17/03/2026, wakati barua hiyo ilionesha kipindi cha extension kuwa kuanzia 01/02/2026 hadi 30/04/2026. Naomba suala hili lifafanuliwe kwa uwazi.
- Baada ya PIP ya pili kumalizika, mkataba wangu ulisitishwa kabla ya tarehe yake ya mwisho.
- Pia nimekuwa na hoja kuhusu utaratibu wa kusitisha ajira, notice, malipo ya mwisho na clearance. Nimetumiwa salary slip inayoonesha malipo fulani, ikiwemo leave na commission, wakati mimi nilikuwa bado sijafanya clearance wala kusaini makubaliano ya mwisho ya malipo.
- Nimejaribu kufuatilia suala hili kupitia kampuni na nimewasilisha malalamiko yangu kwa maandishi, lakini kwa kuwa bado nina maswali ambayo hayajajibiwa kwa namna ninayoona inaridhisha, nimeamua kutumia njia rasmi za kisheria.