Malalamiko ya Wananchi kuhusu mabadiliko na gharama za vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo mwaka 2021

Feb 3, 2019
11
15

Mtandao wa Tigo umekuwa mtandao wa ajabu sana. Yaani saizi wana-program ya ovyo sana ukinunua salio kupitia Tigo pesa, pesa iliyokuwa kwenye acc ya Tigo pesa unakatwa haijalishi hata kama umenunua kifurushi kwa salio la kawaida. Naamini watu wa Sheria mpo humu mtalizungumza suala hili kwa Lugha ya ki-Sheria.

Ni sawa sababu mnadai pesa yenu, lakini kwenye technique za kibiashara mna feli sana. Sababu

1. Mnafanya service yenu kuwa ya gharama sana kwa wateja wenu kitu kinachofanya Vodacom akutandike kila siku sokoni. Mfano mimi mlikuwa mnanidai 3500/= Nimelipa pia nikaongeza vocha ya 3000/= nyingine ili niweze kujiunga kifurushi maana yake hapo nimetumia 6,500/= mnaona Mteja wenu Mlivyo mpatia gharama kubwa.

2. Customer care wanna-midomo michafu sana halafu ukipeleka lalamiko wana kucheka punde unakatiwa simu.

3. MB’s pia mnachakachua tena sana tu. Kweli mnatuogopesha wateja wenu

Niwaambie tu nilikuwa loyal customer wenu ila enough wazee.

WADAU WENGINE WENYE MALALAMIKO HAYA

Vodacom:


pia soma > Malalamiko mbalimbali kuhusu mabadiliko ya vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo kwa mwaka 2020
 
Hamieni Airtel.

Mwanzo nilipata shida sana kuhamia mtandao mpya ila kwa sasa sijutii kwa maamuzi yangu ni mwendo wa kuperuzi. Line ya tigo imebaki kuwa ya kupokea simu na mihamala tu.

Yani kwa maoni yangu binafsi sikuhizi naona Voda ananafuu kuliko tigo. Tigo wamekua majambazi haswa.
 
Alafu Sasa hivi wamekuja na njia mpya ya kukwapua pesa eti Pata Pata sh 300 yaani mtu anakaa anawaza jinsi ya kumuibia mteja wake bila huruma badala ya kuwaza kumfurahisha kwa kukubali kumuungisha, mara Patapata na mara jibu maswali Kuna pesa wakati ni uongo hebu waache hayo mambo ya kuibia wateja wao.
 
Hakuna mtandao wa kiduanzi kama tigo nafikiri management ya tigo vichwani mwao wamejaza upuuzi mtupu, eti mteja anajiunga kifurushi wanagawanya dakika zingine utumie usiku wa manane tu zingine mchana hawa jamaa ni wa hovyo sana, mm mwezi wa 4 huu sijaweka salio kwa laini ya tigo kwa sababu ya mambo ya kijinga kama hayo
 
Tigo washenzi sana!

Walikuwa wanakuja vizuri ila sasa wamekuwa wabaya wa mwisho. Siku hizi wametegesha ukipiga simu ikifika pale pa kuongea na mhudumu inakata automatic.

Vifurushi hovyo na network hovyo 😏😏😏
Bora airtel japo wana mapungufu kiasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…