Malalamiko ya Tozo za miamala na kodi za majengo kupitia Luku yamepungua, safi sana

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,804
1,871
Watanzania sasa wamemuelewa Mama na kukubali kulipa Tozo na kodi kwa moyo mmoja. Katika mitandao malalamiko hayo yamepungua, na leo kulikuwa na Thread moja tu ya kulalamikia kuchelewa kwa muamala kwa ajili ya Tozo na si lalamiko la tozo. Ni suala la utendaji tu

Hii imetokana na watanzania kuelezwa matumizi ya pesa hizo za mwezi mmoja tu kujenga madarasa 560 watayosomea watoto wetu na kujengwa kwa zahanati zaidi ya 90 tutazotumia sisi wenyewe.

Ni mwendawazimu tu anaweza kuendelea kulalamika katika faida hizo kwa mwezi mmoja. Fikiria kwa mwaka mmoja tutakuwa wapi. Mama endelea watanzania tupo nyuma yako, na yataposimama madarasa na zahanati vicheko vitazidi.

Mama, Rais SSH endelea kuzungumza na watanzania kwa lugha wanayoielewa, na wao watakuelewa tu.
 
Ni mwendawazimu tu anaweza kuendelea kulalamika katika faida hizo kwa mwezi mmoja. Fikiria kwa mwaka mmoja tutakuwa wapi. Mama endelea watanzania tupo nyuma yako, na yataposimama madarasa na zahanati vicheko
Hatujamuelewa kabisa na miamala tumepunguza sana. Kuna mingine haiepukiki hivyo michache tunalazimika kuifanya.

Serikali haikuhitaji kutuwekea mzigo wa tozo ili wafanye hicho wanchodai kufanya. Tunalipa kodi nyingi sana wanastarehe tu na magari ya kifahari, safari zisizokuwa za azima na entouarge kubwa halafu wanatubambikia mzigo wa tozo.

Wao mbona hawalipi kodi kwenye mishahara yao?
 
kwa hiyo???
MI-5 tena. Yaani mtu kanisaidia shida yangu, watoto wangu walikuwa wanasomea chini ya miti, kajenga madara. Hivi kibinaadamu hapo unasema nini. Mi wazazi wangu walinifundisha nisema:

Asante sana na ubarikiwe, Shukran, M Mungu aendelee kukujaza hayo maarifa na akili katika kutuongoza, Wewe ni chaguo la M Mungu akuongezee umri mrefu na uendelee kuiongoza TZ.

Hayo ndio baadhi ya maneno niliyofundishwa kuyasema nikifanyiwa mazuri, sio kukashifu.
 
Hatujamuelewa kabisa na miamala tumepunguza sana. Kuna mingine haiepukiki hivyo michache tunalazimika kuifanya. Serikali haikuhitaji kutuwekea mzigo wa tozo ili wafanye hicho wanchodai kufanya. Tunalipa kodi nyingi sana wanastarehe tu na magari ya kifahari, safari zisizokuwa za azima na entouarge kubwa halafu wanatubambikia mzigo wa tozo. Wao mbona hawalipi kodi kwenye mishahara yao?
Tumia pesa upate pesa.
 
Ya sasa mbona ndogo sana?

Waongeze kodi n tozo maradufu, ingependeza zaidi.
 
Halafu Sasa hivi wanaofungua na kufufua akaunti zao kwenye mabenki wengi sana.

Mimi nimefungua akaunti mbili mpya kwa ajili ya kukwepa miamala ya simu.
Tozo safiiiii.
 
Halafu Sasa hivi wanaofungua na kufufua akaunti zao kwenye mabenki wengi sana.

Mimi nimefungua akaunti mbili mpya kwa ajili ya kukwepa miamala ya simu.
Tozo safiiiii.
Nakutakia kila la heri, lakini hatan huko utachangia tu. Na zile foleni huko mabenki na bankomati kuboom kila wakati- Mmmmm
 
Serikali inakwenda kwa mipango ya muda, kwa sasa hiyo inatosha kutatua kero za madarasa na zahanati.

Waongeze tafadhali. Hata zikiwa mara kumi itapendeza zaidi.

Wao vigogo hata wasipolipa kabisa sisi tunatosha sana.

Kwanza tulishazizowea.
 
Halafu Sasa hivi wanaofungua na kufufua akaunti zao kwenye mabenki wengi sana.

Mimi nimefungua akaunti mbili mpya kwa ajili ya kukwepa miamala ya simu.
Tozo safiiiii.
Ni jambo jema, itaenda kuinua sekta ya bank ambayo ilikuwa inaelekea kufa kutokana na hii miamala ya simu
 
tumeamua kukaa kimya 2025 sio mbali tuombe uzima tu tutatoa kishindo kikuu "kenge damu itamtoka masikioni"
Msije kalia kuwa nako tumeibiwa, kumbe zahanati na wazazi wa watoto wakaao madarasa ya Samia, wamejibu. Hapa ni utatuzi wa kero tu ndio jibu 2025.

Wanaouza maneno waendelee kuuza maneno.....
 
Hayajapungua, ni kwamba tu serikali imetia pamba masikioni na kudharau sauti za wananchi.

Hakuna mtu wa kuzungumza kitu kilekile kila siku, huo ni uchizi.

Hata Ukifiwa unalia na maisha yanaendelea hii haimaanishi kuwa uchungu wa kufiwa umeisha
 
Back
Top Bottom