KERO Malalamiko Kuhusu Makosa katika Transcript ya Mhitimu wa Chuo cha Afya

KERO Malalamiko Kuhusu Makosa katika Transcript ya Mhitimu wa Chuo cha Afya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Johnedwiga

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
5
Reaction score
6
Mimi ni mmoja wa wahitimu wa chuo cha afya chini ya NACTE mwaka 2019. Kero yangu inahusu transcript yangu ambayo niliipata baada ya kupitia usumbufu mkubwa.

Nilipoipokea, sikuikagua kwa makini, lakini baadaye nilipogundua makosa, nilibaini kuwa somo ambalo nilipata alama ya A lilikuwa limeandikwa C kwenye transcript yangu.

Nilirudi kufuatilia suala hilo na nikaelekezwa chuoni. Nilipofika chuoni, nilikuta matokeo yangu yanaonesha alama ya A kama nilivyopata awali. Niliambiwa kuwa tatizo halikutokana na chuo, hivyo nililazimika kurudi tena kwa mamlaka husika.

Nilipoeleza changamoto yangu kwa mtumishi mmoja, nilipata jibu lililoniumiza zaidi. Aliniuliza kwa namna ya kejeli kama nilikuwa na GPA ya 4 na bado nilitaka iongezwe. Kauli hiyo ilinifanya nijisikie vibaya sana, kwa sababu sikuwa naomba kuongezewa alama, bali nilitaka kosa lililokuwepo kwenye transcript yangu lirekebishwe ili liendane na matokeo yangu halisi.

Hadi leo, jambo hili bado linaniumiza. Nilikuwa nalipenda sana somo hilo, na kila ninapolikumbuka pamoja na kilichotokea, ninajikuta nikilia. Kwa kweli, sijawahi kurudi tena kufuatilia suala hilo tangu siku hiyo.

Naomba mamlaka husika zilifuatilie suala hili kwa haki na kutoa utaratibu wa kurekebisha makosa ya matokeo kwenye transcript. Mhitimu anapaswa kupata nyaraka zinazoakisi matokeo yake halisi, na malalamiko yake yanapaswa kusikilizwa kwa heshima bila kudhaniwa kuwa anataka kuongezewa alama zisizomstahili.
 
Back
Top Bottom