Malalamiko dhidi ya China hayaisaidii Marekani kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111239345594.jpg
Wizara ya Sheria ya Marekani hivi karibuni ilitangaza kuzishtaki kampuni na raia kadhaa wa China kwa madai ya kuzalisha na kuuza malighafi za dawa za kulevya. Hii si mara ya kwanza kwa Marekani kuihusisha China na suala la dawa za kulevya nchini humo. Lakini swali ni kwamba, je, tatizo la matumizi ya dawa za kulevya nchini Marekani lina uhusiano gani na China? Ama China imechukua nafasi ya Mexico kuwa kituo kikuu cha magendo ya kuuza dawa za kulevya nchini Marekani?

Bila shaka jibu ni hapana!

Malalamiko ya Marekani dhidi ya China kuhusu suala la dawa za kulevya yote yanatokana na Fentanyl. Fentanyl ni malighafi muhimu ya kutengeneza dawa za kutuliza maumivu. Lakini kama dawa hii ikitumiwa kupita kiasi, ni rahisi kwa mtumiaji kuwa mraibu. Kwa wakati huu, dawa hiyo ya kuokoa maisha inaweza kuwa dawa ya kulevya. Wamarekani ndio watumiaji wakubwa zaidi duniani wa dawa ya Fentanyl, na hata watu wengi wanatumia dawa hiyo badala ya dawa ya kulevya. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani, kuanzia Januari 2022 hadi Januari 2023, zaidi ya Wamarekani 109,000 wamekufa kutokana na kutumia dawa kupita kiasi.

Sababu ya Marekani kuilalamikia China ni kwa sababu China ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa Fentanyl duniani. Lakini kama Marekani ikitaka kudhibiti dawa hiyo, kwa nini haipigi marufuku kampuni zake kuagiza dawa hiyo kutoka China? Ni wazi kuwa Marekani haina mamlaka ya kupiga marufuku kampuni za China kuzalisha na kuuza dawa hiyo. Licha ya hayo, madhumuni ya kampuni za China kuzalisha Fentanyl ni kutengeneza dawa ya kuokoa maisha, na sio kwa ajili ya Wamarekani kuitumia kama dawa za kulevya. Marekani haiwezi kuzuia China kuzalisha Fentanyl kwa ajili ya hitaji lake la kukabiliana na dawa za kulevya, hali ambayo inaweza kusababisha upungufu wa dawa hiyo duniani.

Ukweli ni kwamba, kama moja ya wazalishaji wakuu wa Fentanyl, China ni nchi ya kwanza duniani kudhibiti aina zote za Fentanyl, na imekuwa na jukumu muhimu katika kuzuia matumnizi haramu ya dawa hiyo. China pia imefikia makubaliano na Marekani kuchukua hatua chanya ili kuimarisha ushirikiano katika udhibiti wa dawa hiyo.

Matumizi mabaya ya Fentanyl nchini Marekani yanatokana na sababu mbalimbali, ikiwemo hatua dhaifu za kudhibiti dawa, ushawishi wa makundi ya kimaslahi, na utamaduni wa kijamii. Kama nchi iliyo na tatizo kubwa zaidi la matumizi mabaya ya dawa, hadi sasa Marekani haijaorodhesha rasmi aina zote za Fentanyl katika dawa zinazodhibitiwa. Zaidi ya hayo, makundi mengi ya kimaslahi nchini humo yanafadhili wataalam kueneza maoni kwamba “Fentanyl haina madhara”, na kuhimiza maduka ya dawa na madaktari kutoa dawa nyingi kupita kiasi.

Kuhusu changamoto ya dawa za kulevya, Marekani inapaswa kutafuta vyanzo vyake vya ndani, ili kupata njia halisi ya kuiondoa, badala ya kuitupia lawama China.
 
Back
Top Bottom