Malaika wa Kifo: Hadithi ya Kutisha ya Muuguzi Genene Jones

Malaika wa Kifo: Hadithi ya Kutisha ya Muuguzi Genene Jones

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Katika wodi ya watoto wachanga kwenye hospitali ya Texas, muuguzi mmoja alionekana mwenye tabasamu pana, uchangamfu kubwa, huruma na kujali isivyo kawaida. Alikuwa karibu na kila mtoto aliyelia, alihakikisha kila kitu kipo sawa, na mara nyingi alionekana kumfariji mzazi kwa tabasamu la matumaini huku akimpatia pole na hongera za kujifungua.
images (52).jpeg

Huyu ni Genene Jones, lakini nyuma ya pazia la tabasamu la Genene, kulikuwa na kiza na siri nzito ambayo ni nzito kuibeba.
images (53).jpeg

Usiku mmoja, muuguzi mmoja ambaye alikuwa peke yake na mtoto mchanga, alichukua sindano na kumchoma makusudi kemikali hatari kwenye mishipa ya kichanga huyo, ni kemikali ya Succinycholine. Sekunde chache baadaye, mapigo ya moyo ya mtoto yakaanza kudorora, kufifia hadi hatimaye kichanga huyo kupoteza maisha.
images (59).jpeg

Hakukuwa na alama ya majeraha wala kilio cha msaada — kifo kilikuwa ni kimya kimya kama wimbo wa Juma Mohamed Mchopanga, kichanga ambacho hakikuweza kuongea wala kuomba msaada kikafumba macho yake milele.
images (57).jpeg

Katika historia ya watu makatili duniani unaweza kuwataja, Adolf Hitler, Pol Pot, Hideki Tojo, Idi Amin Dada, ama Slobodan Milosevic ila nikiacha kutaja jina la Genene Jones sidhani kama itakuwa busara.
images (60).jpeg

Ni jina ambalo linachukua nafasi ya kipekee – si kwa ukumbusho wa matendo ya huruma wala tabasamu lake la Mamba. Bali kwa mauaji ya kikatili aliyoyafanya akiwa chini ya vazi jeupe takatifu la uuguzi. Muuguzi huyu kutoka Texas, Marekani, anajulikana kama mmoja wa wauaji wa kutisha zaidi waliowahi kuhudumu ndani ya sekta ya afya, Genene alikuwa na tabia zote sawa na “malaika wa kifo”.
images (61).jpeg

Genene Anne Jones alizaliwa mwaka 1950 katika jimbo la Texas. Baada ya maisha ya utotoni yenye changamoto kadhaa, aliamua kujiunga na taaluma ya uuguzi, akiwa na matarajio makubwa ya kusaidia wagonjwa kuokoa maisha yao.
images (62).jpeg

Mnamo miaka ya 1970 na mapema miaka ya 1980, alifanya kazi katika hospitali ya Bexar County Medical Center (ambayo kwa sasa inaitwa University Hospital) na katika kliniki binafsi.
images (63).jpeg

Lakini badala ya kuvaa vazi jeupe na kuwa msatari wa mbele kama mlinzi wa maisha ya wanadamu, bibiye Jones alianza kujulikana kwa matukio ya kushangaza ya vifo vya watoto waliokuwa chini ya uangalizi wake.
images (64).jpeg

Watoto walikuwa wakioteza maisha ghafla, au kupatwa na matatizo ya kiafya yasiyoeleweka mara tu baada ya kuwa mikononi mwake. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mamlaka za Afya, Genene alikuwa akiwachoma watoto sindano zilizokuwa na kemikali hatari ya heparin na wakati mwingine huwachoma kemikali ya digoxin (dawa za moyo ambayo huweza kuwa sumu endapo ikizidi kipimo).
images (56).jpeg

Alikuwa akifanya hivyo ili kuwaleta watoto karibu zaidi na kifo, ili baadaye aonekane kama shujaa kwa kujaribu kutoa msaada wa kuwaokoa — kwa mantiki ya “kujenga mazingira ya kuhitajika zaidi”.
images (55).jpeg

Kati ya kesi maarufu ni ile ya Chelsea McClellan, mtoto wa miezi saba aliyefariki mnamo 1982 baada ya kuchomwa sindano na Genene.
images (65).jpeg

Kesi hii ilichangia kumtia hatiani, na hatimaye mnamo mwaka 1984 alihukumiwa kifungo cha miaka 99 jela, sio kifo bali miaka 99 jela. Kila ukitazama picha ya mtoto McClellan sidhani kama kuna mzazi anaweza kukubali kuwa tabasamu la mtoto Chelsea McClellan ndio limeondolewa duniani na mtu ambaye ni muuguzi.
images (66).jpeg

Katika hali ya kushangaza, sheria za jimbo la Texas wakati huo ilimpa uwezekano wa kuachiliwa kwa msamaha baada ya kutumikia sehemu ya kifungo chake. Hii ilisababisha vuguvugu kutoka kwa umma na familia za wahanga.
images (54).jpeg

Ili kuhakikisha hatoki, mamlaka zilifungua mashtaka mapya mwaka 2017 dhidi yake kuhusu mauaji mengine manne ya watoto. Mnamo 2020, alikiri kosa moja la mauaji na akahukumiwa kifungo cha maisha, sio kifo bali kifungo cha maisha.
images (60).jpeg

Wachambuzi wa tabia za wahalifu wamejaribu kueleza nini kilichomsukuma muuguzi Genene kufanya unyama huo. Dr. Katherine Ramsland, mtaalamu wa saikolojia ya uhalifu, anasema Genene alionyesha tabia za wazi za ugonjwa wa “Munchausen syndrome by proxy” hali ambapo mtu hujenga au kusababisha ugonjwa kwa mwingine ili kupata huruma au kutambulika kama shujaa.
images (67).jpeg

Kwa mujibu wa The Death Shift, kitabu kilichoandikwa na Peter Elkind, mauaji haya yalikuwa ya kimfumo na kwa makusudi, yakifichwa na udhaifu wa mifumo ya hospitali. Elkind anaeleza jinsi utawala wa hospitali ulivyoshindwa kuchukua hatua mapema licha ya ishara za wazi, muuguzi kuonekana akiwa na hali ya vichanga kufariki mikono mwake, inatia shaka kubwa.
images (68).jpeg

Wakati huo kitabu cha, Blind Eye cha James B. Stewart, kinalinganisha kesi ya Genene Jones na matukio mengine ya wauguzi wauaji, kikibainisha kuwa udhaifu wa uwajibikaji katika sekta ya afya hutoa nafasi kwa wahalifu kama hawa kupoteza maisha ya watu kwa makusudi.
images (64).jpeg

Blind Eye imeelezea wazi wazi kuwa wauguzi kama Kristen Hearther Gilbert, Charles Cullen wana mioyo migumu sawa na Genene Jones huku tabia zao zikioana na kurandana na Robert Diaz, Brian Rosefed, pamoja na mwamba Kimberly Saenz.
images (61).jpeg

Vyombo vya habari kama CNN, ABC News na Texas Monthly viliripoti kwa kina kuhusu kesi hii ya kinyama. CNN iliandika: “Jones si tu muuaji, bali ni mfano wa hatari inayoweza kufichwa nyuma ya unyenyekevu wa uuguzi.”
images (54).jpeg

Wapo watu ambao hupata nafuu wakiona lile vazi, ila kwa Genene ilikuwa ni kama aliingia mkataba na Malaika wa Kifo. Alichokifanya hakina tofauti na Lucy Letby, pamoja na Niel Hogel.
images (53).jpeg

Makala ya Texas Monthly mwaka 1983 yenye kichwa “The Killer Nurse” ilifichua kwa kina namna vifo vya watoto vilivyofumbiwa macho na mamlaka za hospitali, hadi pale familia moja ilipoamua kuchukua hatua binafsi za upelelezi. Vifo vya mwanzo vilionekana ni vifo vya kawaida tu ingawa namba ya vifo vya vichanga hivyo ilikuwa juu.
images (55).jpeg

Sitaki kusema wala kuonesha kuwa wauguzi wote ni wauaji bali kisa hiki cha Genene Jones ni taa nyekundu kwa taasisi za afya kuhusu kutokuwa na mifumo dhabiti ya usimamizi. Kesi hii ilichochea mageuzi ya sheria za uhalifu wa kiafya nchini Marekani na kuwapa nguvu zaidi wazazi na waangalizi kuuliza maswali wanapoona hali isiyo ya kawaida hospitalini.
images (56).jpeg

Wapo wazazi hupenda kuwaachia mamlaka yote wauguzi, kiasi kwamba hata kumgusa mtoto wako unaona ni kama haramu, ama kinyaa, wakati umebeba mimba miezi tisa ila ukishajifungua tu ndio unaona kama umetua mzigo, ukikutana na wauguzi sampuli ya Genene Jones, Irene Becker, ama Robert Diaz, watakufundisha kazi na sio siri utaimba Halelujah kwa sauti ya kwanza.
images (59).jpeg

Zaidi ya watoto 60 wanadaiwa kusindikizwa mbinguni mikononi mwa Genene, ingawa wengi wanaweza kuona ni watoto wachache ila kumbuka muuguzi mmoja amehusika kuondoka roho za binadamu 60, hii idadi ni kubwa sana. Ukishindwa kumuangalia mtoto wako wapo watu watamuangalia na kumsafirisha kwenda peponi.
 
Ila waafrica utumwa wa kifikra hauwezi Isha, huyo muugizi ni wa kumuweka kundi moja na Hitler kweli, au sababu kauwa wazingu, Netanyahu Kila siku anauwa wangapi.
 
Back
Top Bottom