Orodha Rasmi ya watu wanaopitia Maisha magumu nchini Tanzania

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,904
Wakuu Kwema!

Ifuatavyo ni orodha Rasmi ya Watu wanaopitia Maisha Magumu katika nchi yetu ya Tanzania.

1. Single Mother.
Moja ya kundi linalopitia maisha magumu hapa nchini Tanzania ni Dada zetu waliopata watoto kabla ya kuolewa.
Ugumu wa maisha yao unatokana na mtazamo wa jamii dhidi Yao, pia unatokana na Dhana potofu iliyojengeka kwao.

Asilimia 90% ya single mothers wanaopitia kipindi kigumu hali inayowafanya wapate Msongo wa mawazo.
Kwa ambao tunadada zetu tunalijua hili.

Dalili ya ugumu waupitiao unajitokeza katika tabia zao za hasira, chuki iliyopitiliza, kiburi kilichotokana na kuchanganyikiwa.

Wito Kwa Vijana, waache zinaaa ili Kupunguza ongezeko la Single mother, pia wasichana nanyi muache tamaa na akili za kitoto kuwafikiria wanaume ni watu wakuthamini ujinga na tamaa zenu.

2. WASOMI WALIOHITIMU DEGREE NA DIPLOMA AMBAO HAWANA AJIRA.

Hili ni kundi linalopitia maisha magumu hapa nchini. Kundi hili hupata ugumu baada ya miaka mitatu au minne Kuisha tangu wamalize Shule.
Baada ya hapo Hujikuta katika taabu, uchungu, na huzuni kukubaliana na mazingira.

Vijana wenye degree na Diploma huishi Kwa taabu Sana.
Na hata Wale waliopata vibarua ambavyo wanalipwa chini ya laki tatu(300,000/=) huishi Kwa huzuni nyingi.

3. WATU WAFUPI
Kundi hili tangu Dunia kuumbwa linapitia maisha magumu sana. Maneno ya dhihaka, kejeli, Dharau na kutothaminiwa kwao imekuwa sehemu ya maisha yao.
Ufupi unaozungumziwa hapa ni ule wa chini ya futi tano Kwa wanaume na Kwa wanawake ni chini ya futi nne. Hao ni wafupi wote.

Kundi hili hujikuta katika hasira, chuki, na pengine Uchawi.
Ni ngumu kumkuta mtu mfupi asiye na hasira au chuki, au ubishi, au kutokujiamini.
Wengi huwa na maruweruwe yanayosababishwa na magumu wayapitiayo.

Watu wafupi hupata shida Sana nyakati za kutafuta wachumba, ili mtu mfupi Aoe au aolewe basi itampasa atafute mfupi mwenzake au waliopishana nukta chache, tofauti na hivyo basi awe na sifa maalumu Kama vile pesa, au awe mchawi Amloge mwenza aliyemrefu.

Au mwenza mrefu atakubali kuolewa au kuoa na mtu mfupi endapo warefu wenzake wamemtenga, na umri wake umesonga.

4. WANAWAKE WALIOFIKISHA UMRI WA MIAKA 30+ ALAFU HAWAJAOLEWA.
Kundi hili huishi maisha magumu wala sina haja ya Kueleza.
Asilimia kubwa hujikuta katika vita ya kinafsia wakijilaumu na baadaye kulaumu wengine.

5. VIJANA MASIKINI
Kundi linateseka mno.
Kundi hili linadhalilika Kwa mengi.
Umasikini husababisha Afya kudhorota, kukosa nguvu za kiume kutokana na Mlo kuwa duni, mwili kufubaa,
Kukosa hamu ya kuishi.
Kunyanyaswa na wanawake wanaotaka Vijana wenye pesa walau za Kuwatunza. N.k.

6. WAALIMU
Hapana Shaka kuwa Kada hii ni punch bag ya kila mtu, hata vijiweni wapuuzi na wendawazimu wakitaka kutokea mfano watu wenye Hali ngumu za maisha basi waalimu watatajwa.
Wasanii na wanasiasa nao kila uchwao ni hivyo hivyo.

Ni waalimu wachache Sana wanaojivunia kazi ya ualimu.

Wakati nasoma Pale Udsm mwaka wa tatu, nilimtongoza mrembo mmoja anayesomea mambo ya Bank na Finance kutoka ndaki ya UDBS. Yule manzi akaniuliza unasoma kozi gani, nikamwambia ninasomea ualimu, majibu nitayaanzishia Uzi maana yalinikera japo Mimi ni mtu jasiri nijayejiamini.

Waalimu wengi ni dhalili
Waalimu wengi hawajiamini
Waalimu wengi wanahasira Kali na chuki za kijinga kutokana na ugumu wa maisha.

7. WAFANYAKAZI WA NDANI.

Hii Kada nipo muda mrefu. Hakika kundi hili ni moja ya makundi yanayopitia maisha Magumu. Kama hujui maisha magumu basi mtafute mfanyakazi wa ndani.
Wengi wamekata tamaa za maisha.
Hukosa kujiamini na kushindwa kutetewa kutokana na umasikini wao.

Hata hivyo wapo Wafanyakazi WA Ndani washenzi ambao huwaonea waajiri wao hasa Wale waajiri wenye utu na wanaowajali.

ATHARI MAKUNDI HAYA KUPTIA HALI NGUMU NI KAMA IFUATAVYO;

1. Vijana kuwa na chuki Kwa waliofanikiwa.
2. Vijana kutukana hovyohovyo hata sehemu isiyohitaji matusi.
Mfano mitandaoni hata hapa JF sio ajabu ukashangaa mtu anatukana ukicheki hujamfanya lolote, usimlaumu anapitia magumu.

3. Ongezeko la waganga WA kienyeji na Makanisa ya kinabii.

4. Ongezeko la watu wanaobeti na kucheza michezo ya kamari.

5. Ongezeko la udangaji Kwa wanawake hasa single mother ambao wanahitaji Kulea watoto waliotelekezewa.

6. Ongezeko la biashara ya kuongeza nguvu za kiume kutokana kundi kubwa la Vijana hawali mlo kamili hivyo automatically nguvu lazima wakose.

7. Ongezeko la watu kujiua au kuua aidha Kwa sababu ya Mapenzi au utafutaji wa Mali Kama Urithi au wizi.
Umasikini Kwa sehemu kubwa huchangia mauaji na kujiua.

8. Ongezeko la vioja Mtandaoni na memes za kujifurahisha au kudhihaki kuliko kufundisha au kufariji.

9. Ongezeko la mario na ushoga kwani wanaume wakishakosa pesa na wasipokuwa na nguvu za kiume kinachobaki ni aidha achague Umario au kuwa shoga.

NINI KIFANYIKE.

1. Vijana wasomi wapunguze matarajio na Watu warudi vijijini wakaishi maisha ya kawaida ya kufuga kuku na kulika vinusu heka.

2. Wasichana wapewe elimu ya mahusiano wangali wadogo ili kuondoa kujichanganya Kwa kushindwa kuelewa mwanaume mwenye upendo na mwenye tamaa.
Wasidhani kujaliwa na kuhudumiwa ndio upendo kwani wanaume wahuni hufanya hivyo kuziteka nyoyo zao.

3. Umasikini Kwa Vijana upunguzwe Kwa kubadilisha fikra zao kuhusu Dhana ya kazi. Wasichague kazi.

4. Kasumba ya kuishi mjini iondolewe ili Kupunguza competition, ambayo huwafanya Vijana kushindwa mapambano kwani competition ni fursa Kwa wenye mitaji na akili nyingi.

5. Wanawake wafundishwe kujipatia waume zao kabla ya miaka 25 ili kuwasaidia wasiwe under pressure.

Tuishie hapa
 
Kwenye wanawake wafupi sio kweli.
Mimi ni mrefu sana na huniambii kitu kwenye wanawake wafupi, I mean they're flexible na wanajaa mikononi easily.
Sijui wengine ila mimi napenda mwanamke akiwa mfupi zaidi yangu it makes you feel in control and more superior unakuwa unamuangalia kwa chini hivi.

Niikuja kwa hilo tu.
 
Wakuu Kwema!

Ifuatavyo ni orodha Rasmi ya Watu wanaopitia Maisha Magumu katika nchi yetu ya Tanzania.

1. Single Mother.
Moja ya kundi linalopitia maisha magumu hapa nchini Tanzania ni Dada zetu waliopata watoto kabla ya kuolewa.
Ugumu wa maisha yao unatokana na mtazamo wa jamii dhidi Yao, pia unatokana na Dhana potofu iliyojengeka kwao.

Asilimia 90% ya single mothers wanaopitia kipindi kigumu hali inayowafanya wapate Msongo wa mawazo.
Kwa ambao tunadada zetu tunalijua hili.

Dalili ya ugumu waupitiao unajitokeza katika tabia zao za hasira, chuki iliyopitiliza, kiburi kilichotokana na kuchanganyikiwa.

Wito Kwa Vijana, waache zinaaa ili Kupunguza ongezeko la Single mother, pia wasichana nanyi muache tamaa na akili za kitoto kuwafikiria wanaume ni watu wakuthamini ujinga na tamaa zenu.

2. WASOMI WALIOHITIMU DEGREE NA DIPLOMA AMBAO HAWANA AJIRA.

Hili ni kundi linalopitia maisha magumu hapa nchini. Kundi hili hupata ugumu baada ya miaka mitatu au minne Kuisha tangu wamalize Shule.
Baada ya hapo Hujikuta katika taabu, uchungu, na huzuni kukubaliana na mazingira.

Vijana wenye degree na Diploma huishi Kwa taabu Sana.
Na hata Wale waliopata vibarua ambavyo wanalipwa chini ya laki tatu(300,000/=) huishi Kwa huzuni nyingi.

3. WATU WAFUPI
Kundi hili tangu Dunia kuumbwa linapitia maisha magumu sana. Maneno ya dhihaka, kejeli, Dharau na kutothaminiwa kwao imekuwa sehemu ya maisha yao.
Ufupi unaozungumziwa hapa ni ule wa chini ya futi tano Kwa wanaume na Kwa wanawake ni chini ya futi nne. Hao ni wafupi wote.

Kundi hili hujikuta katika hasira, chuki, na pengine Uchawi.
Ni ngumu kumkuta mtu mfupi asiye na hasira au chuki, au ubishi, au kutokujiamini.
Wengi huwa na maruweruwe yanayosababishwa na magumu wayapitiayo.

Watu wafupi hupata shida Sana nyakati za kutafuta wachumba, ili mtu mfupi Aoe au aolewe basi itampasa atafute mfupi mwenzake au waliopishana nukta chache, tofauti na hivyo basi awe na sifa maalumu Kama vile pesa, au awe mchawi Amloge mwenza aliyemrefu.

Au mwenza mrefu atakubali kuolewa au kuoa na mtu mfupi endapo warefu wenzake wamemtenga, na umri wake umesonga.

4. WANAWAKE WALIOFIKISHA UMRI WA MIAKA 30+ ALAFU HAWAJAOLEWA.
Kundi hili huishi maisha magumu wala sina haja ya Kueleza.
Asilimia kubwa hujikuta katika vita ya kinafsia wakijilaumu na baadaye kulaumu wengine.

5. VIJANA MASIKINI
Kundi linateseka mno.
Kundi hili linadhalilika Kwa mengi.
Umasikini husababisha Afya kudhorota, kukosa nguvu za kiume kutokana na Mlo kuwa duni, mwili kufubaa,
Kukosa hamu ya kuishi.
Kunyanyaswa na wanawake wanaotaka Vijana wenye pesa walau za Kuwatunza. N.k.

ATHARI MAKUNDI HAYA KUPTIA HALI NGUMU NI KAMA IFUATAVYO;

1. Vijana kuwa na chuki Kwa waliofanikiwa.
2. Vijana kutukana hovyohovyo hata sehemu isiyohitaji matusi.
Mfano mitandaoni hata hapa JF sio ajabu ukashangaa mtu anatukana ukicheki hujamfanya lolote, usimlaumu anapitia magumu.

3. Ongezeko la waganga WA kienyeji na Makanisa ya kinabii.

4. Ongezeko la watu wanaobeti na kucheza michezo ya kamari.

5. Ongezeko la udangaji Kwa wanawake hasa single mother ambao wanahitaji Kulea watoto waliotelekezewa.

6. Ongezeko la biashara ya kuongeza nguvu za kiume kutokana kundi kubwa la Vijana hawali mlo kamili hivyo automatically nguvu lazima wakose.

7. Ongezeko la watu kujiua au kuua aidha Kwa sababu ya Mapenzi au utafutaji wa Mali Kama Urithi au wizi.
Umasikini Kwa sehemu kubwa huchangia mauaji na kujiua.

8. Ongezeko la vioja Mtandaoni na memes za kujifurahisha au kudhihaki kuliko kufundisha au kufariji.

9. Ongezeko la mario na ushoga kwani wanaume wakishakosa pesa na wasipokuwa na nguvu za kiume kinachobaki ni aidha achague Umario au kuwa shoga.

NINI KIFANYIKE.

1. Vijana wasomi wapunguze matarajio na Watu warudi vijijini wakaishi maisha ya kawaida ya kufuga kuku na kulika vinusu heka.

2. Wasichana wapewe elimu ya mahusiano wangali wadogo ili kuondoa kujichanganya Kwa kushindwa kuelewa mwanaume mwenye upendo na mwenye tamaa.
Wasidhani kujaliwa na kuhudumiwa ndio upendo kwani wanaume wahuni hufanya hivyo kuziteka nyoyo zao.

3. Umasikini Kwa Vijana upunguzwe Kwa kubadilisha fikra zao kuhusu Dhana ya kazi. Wasichague kazi.

4. Kasumba ya kuishi mjini iondolewe ili Kupunguza competition, ambayo huwafanya Vijana kushindwa mapambano kwani competition ni fursa Kwa wenye mitaji na akili nyingi.

5. Wanawake wafundishwe kujipatia waume zao kabla ya miaka 25 ili kuwasaidia wasiwe under pressure.

Tuishie hapa
Watu wafupi mbona wanaonewa sana jamani

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom