Wakati fulani...UKAWA walisema tatizo ni mfumo wa CCM ndiyo unakwamisha maendeleo ya nchi hivyo waungane wauondoe mfumo huo madarakani ili waweke nchi sawa. Na wakasisitiza wako tayari kushirikiana na yeyote kuondoa mfumo huo, maana walisema tatizo siyo watu bali ni mfumo. Ni kweli walitekeleza azma yao ingawa walikosea mahali. Bahati.....hawakuweza kuchukua madaraka.
------------------------
Na sisi watanzania tuwaige wanaukawa ila tusikosee mahali kama wao...Adui yetu mkubwa kwa sasa (mbali na maradhi, umasiki, ujinga) ni Matumizi ya madawa(sumu) za kulevya. sumu hizi zinaua kizazi chetu cha sasa na vijavyo. Kwa sasa tusichague silaha ama mtu wa kushirikiana naye ili mradi silaha ama mtu huyo ina/anafaa katika mkakati wa kushida vita hiyo. Paul Makonda ni asset kwenye vita hivi, tumtumie kushinda vita dhidi ya madawa ya kulevya.