Makundi ndani ya CHADEMA

armanisankara,

Tuseme kuna ukweli mkubwa katika utafiti wa mwandishi wa gazeti hilo la sauti huru. Tuseme kweli yapo makundi matatu ambayo yanajiandaa ktk kuchukua kiti cha IKULU mwaka 2015, vigogo hao watatu wakifanya maandalizi ya kukiongoza chama ktk uchaguzi wa mwaka 2015 - Kuna ubaya gani?. Labda pengine niongezee kwamba kujipanga kwao ndani ya chama kwa ukanda kutawawezesha vipi kupata Ushindi wa uchaguzi wa mwaka 2015.

Maana umeeleza mengi sana ya Ukanda na kadhalika hata umefikia kutoa hukumu kwamba Mbowe ndiye mwenye nafasi kubwa ya kusimama kama mgombea wa Chadema kiti cha Urais. Na umevutka mipaka ya ukanda kuonyesha support nje ya Kilimanjaro sasa sijui unaweza kutuambia huyo Mbowe ataweza vipi kushndwa uchaguzi mwaka 2015 tofauti na alivyoshindwa mwaka 2005 au kutosimama mwaka 2010. Ukaskazini wa Mbowe au Dr.Slaa utawasaidia vipi kungia Ikulu hapo ndio ningependa sana kuelewa maana bado haijazama akilini au basi huyo Mbowe, Dr.Slaa na Zitto ni wajinga walopindukia maana umaarufu ndani ya chama hauwezi kutoa ushindi uchaguzi wa Taifa.

Na mwisho ningependa sana ia kujua makundi ndani ya CCM wamejiandaa vipi? hii mada ingependeza zaidi kuona jinsi vyama vyote vilivyojipanga iwe kwa Ukanda, Udini, Makabila, Kujuana, Mtandao na kadhalika. Je, CCM, CUF TLP na vyama vinginevyo kuna makundi gani na mangapi wakitumia mitego gani kujenga umaarufu wao ndani ya chama na nje ili kupata ushindi mwaka 2015.
 
CCM must think watanzania ni majuha! Mtu mzima anaaga mkewe/mumuwe kwamba anaenda kazini, kumbe anaenda kuandika huo upuuzi?
 
Haya jmushi,dallai lama,nanyaro na wengine wote, hebu tuambieni na nyie mko kundi gani? Molemo yeye anajulikana yuko upande wenye posho kubwa,kwa DJ.
 
Kuna makundi Chadema so what ?Sisi hapa JF si hao Chadema hili ni jamvi la kuanika ujinga kujadili maendeleo na kuelemishana .
 
Kuna makundi Chadema so what ?Sisi hapa JF si hao Chadema hili ni jamvi la kuanika ujinga kujadili maendeleo na kuelemishana .
Hivi na kujadili makundi ndani ya ccm pia ni maendeleo, mbona mnakuwa wakali members wakiamua kujadili mvurugano wenu?
 
Mbona ni fake analysis ambayo mtu yeyote anaweza kuandika?
Eliah G Kamwela says sorry for this very kilazaful post.
 
Haya jmushi,dallai lama,nanyaro na wengine wote, hebu tuambieni na nyie mko kundi gani? Molemo yeye anajulikana yuko upande wenye posho kubwa,kwa DJ.

Niko upande wa Zitto.Wewe najuwa ni magamba lakini upo upande sawa na wangu.
 
Hata mimi nina kundi ndani ya Chadema mbona wamesahau kunitaja? Wanaoniunga mkono ni wale wanaotoka kanda ya Mashariki na upande wa Visiwani hasa mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Dar es Salaam (Temeke zaidi), Unguja na Pemba, Mtwara na Lindi pamoja na Ruvuma (Tunduru). Wanaoniunga mkono ni Ritz, zomba, Tume ya Katiba, malaria Sugu, @Mafilifili, TUNTEMEKE, @Inoncensia na Faiza foxy. Mwaka 2015 lazima tuchukue Urais kupitia Chadema la sivyo tutajiunga na CUF au ADC
 
Last edited by a moderator:
Nina wasiwasi na hii makala kama imeandikwa na Mwandishi wa Habari? Kweli kuna watu wananunua Gazeti lenye waandishi namna hii? Upo uwezekano makala hii imeandikwa na Dr.Nchimbi au Nape ambao elimu zao ni za kunua
 
Mkuu si haya ndiyo magazeti ya SSM na kina Rz1 na waislam eti wanataka kuharibu CDM? Wanapoteza muda, linaingia sikio moja linatokea lingine!!! Nguvu ya wananchi sasa, saa ya ukombozi ni sasa!!

ukishakuwa Chadema huna haja ya kuutaja Uislam kama ulivyofanya kwani tayari huwa tunajua msimamo wenu kwa Uislam!
 
Thread kama hizi zinazidi kupotray ni jinsi gani gongo inazidi kuathiri ubongo wa watu na kuwafanya wawe vilaza na dhaifu kimawazo tena wenye akili za ujuha.
 
hizi ndo ndoto za walio wengi wasio itakia mema chadema
 
Back
Top Bottom