Makumira University kumekucha!

Makumira University kumekucha!

Hivi pale bodi ya mikopo kuna tatizo gani? Mbona wakurugenzi wa pale wanaota tu vitambi na kujenga magorofa huku waki drive magari luxury, hizi pesa za kufanyia haya matanuzi si ndo zingeenda kuwalipa wanafunzi posho za chakula na malazi?

Nyatega, Lubambula, Kisare na Bangu wako pale Bodi ya Mikopo kwa maslahi ya nani? Hii management ya bodi ya mikopo inahitaji kuondolewa yote na kuajiri management team nyingine itakayoweza kuendana na changamoto zilizopo.

Kwa nini migogoro ya vyuo vikuu kuhusu mikopo ya wanafunzi imekuwa mingi baada tu ya kuanzishwa kwa Loan Board mwaka 2005? Wakati ilitarajiwa kuanzishwa kwa taasisi maalumu kama hii ya kushughulikia mikopo ya wanafunzi kungeleta ufanisi na tija zaidi na hivyo kuondokana na migogoro ya mara kwa mara.

Management ya Loan Board ni sifuri kabisa, sijui hata Mh. Rais anawalea kwa nini!!!!
 
Migomo haijaanza leo; ni toka enzi zileeee..!! Kwa waliosoma Mlimani mtakumbuka aina mbali mbali za migomo ya pale ambayo ilikuwa imelenga kueleza matatizo ya wanafunzi. Wakati mwingine, ilikuwa inalenga kupinga mikataba ya kijinga kama ya kuwalazimisha au kuwawekea wanafunzi vikwazo vya au masharti magumu ya udhamini.

Kilichokuwa kinanikera ni baadhi wa wazazi and wananchi kibao waliokuwa wanaponda na kudai kuwa wanafunzi mnapewa hela za kujikimu, then mnaenda kustarehe and mkiishiwa tu mnagoma. Hii migomo ya chuo kama Mlimani si ya kukurupuka, huwa inapangiliwa vizuri (I mean miaka hiyo sijui kwa sasa); by then tulikuwa na Rev/Square. Na mingine inalenga kukisaidia kizazi kijacho and not hiki cha sasa (mfano hii biashara ya udhamini unaowatesa wanafunzi hii leo).

Nakumbuka Prof. Chachage (RIP) aliwahi kusema kuwa, "intellectual au mtu mwenye akili timamu na elimu kamilifu hawezi kugoma au kuandamana bila sababu ya msingi". Na aliitaka serikali kukaa chini na kuangalia tatizo sio kuwalaumu wanafunzi, akimaanisha mtu aliyegoma ni kwamba mambo yamemfika shingoni.

Hivyo basi, nchi hii na serikali yake ikaamua kuzoea "migomo" badala ya kushangaa migomo. Hili limepelekea migomo kuwa ni "business as usual" instead kuwa ishara mbaya kwa serikali kuwa kuna mapungufu mahali. Imagine hadi malecturer wa vyuo vikuu kugoma...!!! Hii ni hali mbaya sana, at least Pinda kwa swala hili la malecturer na wanafunzi wa UDOM alichukua hatua but I hope si maneno ya jukwaani bali yatakuwa vitendo (kwani tumesikia mengi majukwaani toka miaka hiyo).
 
Kazi kweli inamaana hawapati hela mpaka DOWANS walipwe?
 
Tanzania hatuna serikali ni uozo mtupu
mawaziri wameshupalia dowans
wameacha kufanyia kazi ajenda za
za muhimu Kama mikopo ya wanafunzi
tumewachoka sasa tunatoka nchi nzima
kudai haki yetu .
 
Kama alivyosema Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu Dowans ni lazima iwe ilipwe. Hivyo, that is the first priority! Wakigoma vija wa Saidi Mwema hawachoki kusambaza na kuwapa mkung'uto kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya (wa) Tanzania.
 
Wana JF habari za uhakika kabisa ni kuwa wanachuo cha Makumira kilichopo Arusha wamegoma na kufunga njia ya magari ya Moshi - Arusha na kusababisha polisi kutinga eneo hilo na kuwatanyawanya kwa nguvu. Kisa cha mgomo huo ni bodi ya mkopo kuwacheleweshea kupata fedha zao a.k.a boom
Polisi wamefanikiwa kuwatuliza ghasia na hali ya magari kupita barabari imerejea tena.
Duuuuuh kweli Tz saizi ni noma!
 
Katika kile kinachooneka kuwa si jambo la kawaida, FFU wametua campus ya Makumira wakiwatawanya wanachuo kila walipokusanyika. Mtoa news anasema uongoz wa chuo haujasema lolote na FFU bado katika kuhakikisha kuwa utulivu unarudi mahali pake. . Habari zaidi zitaendelea kumiminika kadri zitakavyotufikia.
 
mtakula hata majani si tuko bize huku kuilipa Dowans,si ndivyo waliopora madaraka wanavyotufanyia,waziri wa elimu mwenyewe anajua madudu yanayoendelea HESLB na alikiri mwenyewe sasa amefanya nini tangu alipogundua hilo
 
Duuu, hivi hii mikopo ina shida gani siku hizi :suspicious:
Bodi ya mikopo inasubiri maelekezo rasmi ya maandishi toka CC sisiemu,- Kwa mjibu wa Chiligati hii ilikuwa agenda mojawapo ya kikao kilichomalizika.
 
Nimepata habari na ruco wamefanya kamgomo kadogo dogo. Vandalism ya bustani ndio imefanyika sana. OCD allitwa kujaribu kutuliza.
 
kwa asiyejua bodi ni washenzi kweli,utadhani sio watz wenzetu...halafu nimeckia kila afsa pale bodi anakuaga na majina kama kumi hewa ,hv ni kweli au ?
 
nyie wanafunzi tulieni kwanza tunakabiliwa na deni la kimataifa, Dowans. tukimaliza tutawafikiria. hamuoni jinsi nchi yetu ilivyo masikini? nyie ni watoto wa wakulima maskini, mkifukuzwa wazazi wenu watakasirika sana.

au mmetumwa na chadema?

tafadhali rudini madarasani, msiwasikilize hao wapinzani tunashuhulikia tatizo. watawasababisha mtakosa masomo wakati wao walikwishasoma ndiyo maana wanataka madaraka ya kisiasa.
 
Polisi wameingilia maandamano ya wanafunzi, makumIra, wawapiga hovyo na kuwajeruhi baadhi yao, mabomu yatumika na wengine wawekwa ndani. Hajabu nikuwa hata wapitanjia wapewa mkongoto ilihali hawahusiki!

Hivi hawa polisi ni lini watafanyaq kazi kwa kuzingatia sheria? Hii ni dalili ya uoga na upumbavu na umbumbumbu.
TUSIKATE TAMAA UKOMBOZI UNAKARIBIA!

FREEDOM IS COMING TODAY!

Poleni ndugu zangu Makumira ALUTACONTINUA!
 
nyie wanafunzi tulieni kwanza tunakabiliwa na deni la kimataifa, Dowans. tukimaliza tutawafikiria. hamuoni jinsi nchi yetu ilivyo masikini? nyie ni watoto wa wakulima maskini, mkifukuzwa wazazi wenu watakasirika sana.

au mmetumwa na chadema?

tafadhali rudini madarasani, msiwasikilize hao wapinzani tunashuhulikia tatizo. watawasababisha mtakosa masomo wakati wao walikwishasoma ndiyo maana wanataka madaraka ya kisiasa.


Are you serious?
 
Mkuu wa chuo makumira hatimaye baada ya mgomo wa wanachuo leo asubuhi ametoka mafichoni alikokuwa amejificha yeye pamoja na viongozi wenzie tangia asubuhi na. Ameomba kukutana na wanachuo leo saa 7mchana. Viongozi wa kibongo bwana! mpaka afe mtu ndo mazungumzo yaanze? Mtajifunza lini?
 
Baada ya kila kitu kuparanganyika,migomo,hujuma,migawanyiko na kutokuaminiana kuongezeka watakimbia tu wenyewe...
 
baba lao wewe hujui mikopo ilenda kufanya uchkachuaji kwenye uchaguzi mkuu???? TUNATAKIWA KUTIBU SABABU NA SI DALILI WANDUGU
Duuu, hivi hii mikopo ina shida gani siku hizi :suspicious:
 
Hapa kila mtu ana fungu lake la makosa.
  • Wanafunzi baadhi yao hawajazi fomu zao kikamilifu halafu pesa zikichelewa au wasipopata kabisa wanasema bodi ina matatizo.
  • Serikali nayo ilichemka kuanzisha hii bodi kisiasa bila uhalisia na kufanya utafiti wa kutosha kwani ni wazi sasa kumaintain utoaji wa mikopo imekuwa ngumu na nadhani wanapeleka fedha kwa mafungu
  • Utendaji kwenye bodi umekuwa ni tatizo, nadhani tatizo la kuajiri akina mjomba na mtoto wa baba mkubwa ndio matokeo yake haya kwani wanafanya makosa mengi sana na inavyoonekana hawawezi kabisa proper record keeping.
  • Kumekuwa na tuhuma kwa muda mrefu za rushwa ndani ya bodi(sina hakika kama ni kweli) kwamba baadhi ya watendaji ndani ya bodi wana mawakala wao vyuoni, unakata kitu kidogo unapewa mkopo hata kama una division four! mradi una admission.
Suluhisho:
  • Bodi ivunjwe iundwe upya kulingana na uhalisia wa uwezo wa serikali kutoa pesa sio kwa ajili ya kushinda uchaguzi. Hii ni pamoja na mchanganuo mzuri wa nani apate kiasi gani na pia utaratibu wa vyuo kupandisha ada.
  • Wafanyakazi wa bodi wachunguzwe upya ajira yao ili wawepo wale wenye uwezo wa kufanya kazi hii (competent people)
  • Bodi ifungue matawi mikoani na pia iwe na kitengo cha elimu kwa umma
 
Back
Top Bottom