Makumira University kumekucha!

Makumira University kumekucha!

msnajo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
3,066
Reaction score
1,142
Lile jinamizi la migomo vyuo vikuu limetua kwa kasi ya ajabu pale Makumira university. Ni pale wanachuo wa mwaka wa kwanza walipozira kuzama class kutokana na ugumu wa maisha wanaokumbana nao uliosababishwa na kutokupewa hela na bodi ya mkopo.

Wadau nauliza hivi kweli kila kitu cku hizi kinakwenda kimigomo? Serikali yetu iko wapi iliyounda bodi ya mikopo inayoshindwa kutekeleza majukumu yake ipaswavyo? Wanachuo pale wanashindia maji na maembe ili wanatakiwa pia kuhudhuria lecture dararan kama kawaida..

Kweli elimu na njaa vanaenda pamoja? Mwenzao jana kazimia kwa mshtuko alioupata baada ya kudhibitisha kuwa jina lake halipo kwenye batch ya mwisho ya majina, amelazwa pale selian hospital na wenzake wako katika harakati za kuchanga hela kwa ajili ya kumpatia matibabu.

God help then
 
Hii serikali ishauzwa kilichobaki kugawana 2.. Wenye uwezo wa kujilipia wanapewa mkopo wasio na uwezo hawapewi.
Ha2na serikali hapa,bora wagome 2 hop mambo yao yatata2liwa
 
kuna haja ya serikali yetu kuwa na masikio ya kusikia hii bodi ya mikopo iangaliwe upya ina tatizo gani??????
 
Hela inaenda kulipa Dowan. Fungeni mikanda
 
Nashangaa watu wanaijadili bodi ya mikopo, wamesahau kwamba fedha zinatoka serikali. Je kama bodi ya mikopo haijapewa hela ya kutosha kugawa/kukopesha wanafunzi wote nani wakulaumiwa bodi au serikali?
 
St joseph college dsm pia unanukia, kitengo cha wahandisi wa mawasiliano hawajapewa hela za nauli ya field tangu february mwaka jana.
 
Nashangaa watu wanaijadili bodi ya mikopo, wamesahau kwamba fedha zinatoka serikali. Je kama bodi ya mikopo haijapewa hela ya kutosha kugawa/kukopesha wanafunzi wote nani wakulaumiwa bodi au serikali?

Tatizo ni serikali ya CCM haina uchungu na wananchi wake. Tuitoe madarakani kama Tunisia.
 
nashangaa watu wanaijadili bodi ya mikopo, wamesahau kwamba fedha zinatoka serikali. Je kama bodi ya mikopo haijapewa hela ya kutosha kugawa/kukopesha wanafunzi wote nani wakulaumiwa bodi au serikali?

nikweli ulisemalo mkwele,so we uonavyo solution ni nn?

Mi binafsi kwa serikali ya sasa sina la kuwapongeza........kunamatatizo chunguzima mengine hata hilo la wanafunzi ni dogo............
So chamsingi nimaandamano ya kitaifa kuiondoa serekali iliyopo madarakani........(this is my opinion)
 
Kuna habari kuwa wanafunzi wa Makumira university wako kwenye mgomo na kwa sasa wamefunga barabara ya mosh-arusha.kisa cha mgomo ni ucheleweshaji wa mikopo. waliopo hapo chuoni tunaomba habari zaidi.
 
Lile jinamizi la migomo vyuo vikuu limetua kwa kasi ya ajabu pale Makumira university. Ni pale wanachuo wa mwaka wa kwanza walipozira kuzama class kutokana na ugumu wa maisha wanaokumbana nao uliosababishwa na kutokupewa hela na bodi ya mkopo. Wadau nauliza hivi kweli kila kitu cku hizi kinakwenda kimigomo? Serikali yetu iko wapi iliyounda bodi ya mikopo inayoshindwa kutekeleza majukumu yake ipaswavyo? Wanachuo pale wanashindia maji na maembe ili wanatakiwa pia kuhudhuria lecture dararan kama kawaida.. Kweli elimu na njaa vanaenda pamoja? Mwenzao jana kazimia kwa mshtuko alioupata baada ya kudhibitisha kuwa jina lake halipo kwenye batch ya mwisho ya majina, amelazwa pale selian hospital na wenzake wako katika harakati za kuchanga hela kwa ajili ya kumpatia matibabu. God help then

poleni sana, basi yote tunayoyashuhudia ni matunda ya sisi waTZ kukalia kimya matatizo kwa kuogopa kuudhi watu

Serikali hii imetuangusha sana
 
Hela inaenda kulipa Dowan. Fungeni mikanda

Hahahaha,umenifurahisha kweli!
Kwa kifupi Tanzania ya sasa hupati kitu kwa ustaarabu au kwa utaratibu mwingine tofauti na mgomo,....wagome sana tu ikibidi wafanye fujo hapo maskio yataelekezwa kwao na matatizo yataisha otherwise wasubiri hadi kidonda cha dowans kiishe
 
tunisia soon

Jitolee uende maeneo ya kariakoo au sehemu yenye watu wengi then sema yote yanayo kuudhi ukimaliza jilipue na petroli ili tupate hasira tuanze maandamano hadi jk atimue,....

Imekaaaje hiyo?
 
Taarifa nilzopata mda huu zinasema polisi wamefika na kuwatawanya wanachuo kwa ku2mia mabom.
 
Ivi wakuu kwanii nchi hii kama imetushinda tusiiuze halafu kila mtu alambe mgao wake ajikatae akaishi anapojua?
 
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema hali ime2lia na wanachuo wamejikusanya uwanjan kujipanga kwenda kuwatoa wenzao walokamatwa na police.
 
Wana jf nimepita hapa chuo kikuu Makumira wanafunziwa megoma,wamefunga barabara kuu ya Moshi Arusha kwa mawe,matofali na makorokoro mengine. Polisi wamefika wamewatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto na wanafunzi wengi wamekamatwa. Kisa cha mgomo ni mikopo hawajapata.
 
poleni sana ndugu zetu,
inamaana chuo kinachogoma mapema ndiyo kinasaidiwa mapema?. kwasababu kama udom waligoma matatizo yametatuliwa kama yaleyale yapo na sehemu nyingine kwanini wasitatue kote?
 
Back
Top Bottom