Makubwa: Anna Mghwira adai yeye bado ni mwenyekiti wa ACT Wazalendo na hajajiuzulu

Kwani shida hapo nini!!
tapatalk_1496747238390.jpeg
 
Ina maana ACT kama chama hawakuliongelea hilo suala la uteuzi wake na kufikia makubaliano?
Kesho ni kikao cha kamati kuu kujadili hili swala la RC.ila mambo yanaonekana sio shwari ndani ya ACT maana Zito amesafiri leo means kikao cha kesho hatakuwepo badala yake anakaimu Mwigamba
 
Mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema yeye bado ni mwenyekiti wa ACT-Wazalendo na ataendelea kushika wadhfa huo kama kawaida. Mghwira aliyeapishwa Jumanne kuanza kazi, ametoa maelezo hayo katika mahojiano mahsusi na mwandishi Jamal Hashim wa Azam TV. Fuatilia taarifa ya habari ya Azam TV leo saa mbili usiku, ili kupata undani zaidi.


Hata Rais Mwenyewe amesema wapo watu watakao kuonea wivu kwenye Chama Chako-- sasa Chama Chake hicho ni ACT- Zitto Party
 
Mama anataka kuleta mgogoro wa "kikatiba" ndani ya ACT. Usikute hata Katiba ya ACT haikuoversee kitu kama hiki kutokea, na ipo kimya!
 
Kuna Mchezo wa Kisiasa unachezwa hapa!

Zitto alianza kumaliza Tofauti zake na Chadema sasa inatumika Mbinu ya Kisiasa kuhakikisha Chadema wanarejea kwny hofu Yao ya awali kutowaamini ACT

Zitto yupo Njia kakimbia Nje ya Nchi kwa Muda kutafakari
 
Kwa hiyo mkutano wa Act wazalendo kesho atahudhuria? Kuna nafasi za utumishi wa umma ukiteuliwa unatakiwa kujiuzulu vyeo vya kichama
Nasikilizia tu huo mkutano wa kesho kama mwenyekiti atahudhuria, maana agenda inamuhusu yeye
 
Akihojiwa na Hashim wa Azam Tv, Mh. Anna Mghwira amehoji kuwa kwenda kufanya kazi za serikali siyo kigezo cha kutokitumikia chama cha ACT.

Akasema Mbona Lipumba alikwenda nje ya nchi na akaendelea kuwa mwenyekiti wa CUF, sembuse hapa Kilimanjaro.

---
She is quite shallow! analinganisha kwenda kwa Museveni na kwenda Kilimanjaro.

CUF hakikuwa chama cha upinzani dhidi ya Museveni, lakini ACT ni wapinzani wa Magufuli katika siasa za Tanzania.

Anakwenda kutekeleza sera za kufungia wapinzani, kuwasweka mahabusu, kuzuia mikutano, kuwapiga mabomu etc!
 
Akihojiwa na Hashim wa Azam Tv, Mh. Anna Mgwilah amehoji kuwa kwenda kufanya kazi za serikali siyo kigezo cha kutokitumikia chama cha ACT. Akasema Mbona Lipumba alikwenda nje ya nchi na akaendelea kuwa mwenyekiti wa CUF, sembuse hapa Kilimanjaro.
She is quite shallow! analinganisha kwenda kwa Museveni na kwenda Kilimanjaro. CUF hakikuwa chama cha upinzani dhidi ya Museveni, lakini ACT ni wapinzani wa Magufuli katika siasa za TZ. Anakwenda kutekeleza sera za kufungia wapinzani, kuwasweka mahabusu, kuzuia mikutano, kuwapiga mabomu etc!
Hapa hakuna kitu ni bora uhame chama mama.hii inaonyesha ACT ni CCM B
 
... "Mbona Lipumba alikwenda nje ya nchi na akaendelea kuwa mwenyekiti wa CUF, sembuse hapa Kilimanjaro."
Ina maana kufanya consultation nje ya nchi kwa Lipumba ni sawa na kushika madaraka ndani ya nchi kwenye chama kingine? Angekaa kimya, atasababisha watu waanze kuhoji uwezo wake wa kuchambua mambo
 
Back
Top Bottom