Makubwa: Anna Mghwira adai yeye bado ni mwenyekiti wa ACT Wazalendo na hajajiuzulu

Seif ilikuwa sharti la kikatiba na ni wananchi waliotaka serikali ya umoja wa kitaifa sio CUF wala CCM!!! na ilikuwa kwa misingi ya kutafuta suluhu zenji kma ambavyo chadema ilikubali kuunda halmashauri na ccm pale arusha mjini mwaka 2014 ila huyu mama ni lini magufuli alikubali kuleta suluhu na wapinzani hasa wanapodai haki ya mikutano ili wajenge chama??? Ni lini magufuli kakubali rasimu ya warioba irudi??? Mama kasaliti umma wa wapinzani waliotoka naye povu kupinga udikteta
Bila kujali kuwa lilikuwa ni sharti la Kikatiba au la (Sababu yalikuwa ni makubaliano ya muda si ya kudumu ndiyo maana yalipingwa na vyama vingine vya upinzani sababu havikushirikishwa) Muhimu kujua ni Maalim alikuwa anatekeleza kazi zake kwa mujibu wa ilani gani ya Uchaguzi? Chama chake au chama kilichoshinda uchaguzi? Sikuwahi kusikia CUF na CCM visiwani wamekaa kuhuisha Ilani ya pamoja
 
Bila kujali kuwa lilikuwa ni sharti la Kikatiba au la (Sababu yalikuwa ni makubaliano ya muda si ya kudumu ndiyo maana yalipingwa na vyama vingine vya upinzani sababu havikushirikishwa) Muhimu kujua ni Maalim alikuwa anatekeleza kazi zake kwa mujibu wa ilani gani ya Uchaguzi? Chama chake au chama kilichoshinda uchaguzi? Sikuwahi kusikia CUF na CCM visiwani wamekaa kuhuisha Ilani ya pamoja
Mkuu nlishasema hata kwa CUF it was a big mistake ndio maana walikuja kujitoa baaae hta kabla serikali mpya haijaanzishwa!!! But all in all whether seif alitumia ilani ya CCM ila zenji inaeleweka kabisa walikuwa wakisaka amani baada ya vurugu za muda mrefu ssa huku bara hakuna vurugu yoyote inayolazimu kuunda serikali ya mseto ghafla wanaojiita wapinzani waliotoka povu kusema ilani ya ccm haitekelezeki leo hii wanaenda itekeleza !! Inaumiza sana
 
Saju b: Kuingia bungeni siyo lazima uwe mwanaCCM hata kama watakaokuchagua au kukuteua ni wanaCCM, lakini kuwa mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya kwa katiba ya CCM ni lazima uwe mwanaCCM. Muwe mnaielewa nchi yenu nyie watu. Ndiyo maana tunalilia katiba mpya ili wakuu wa mikoa na wilaya wawe watumishi wa umma na wasilazimike kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa.
Unachanganya mambo sana, halafu kinachokera ni kwamba ufafanuzi ulishatolewa huko nyuma. Fuatilia uzi wote, hizi ni elimu, tunaelimika hapa.

Katiba ya ccm haiwezi kuzungumzia cheo cha kiserikali, mkuu wa Mkoa ni mtumishi wa serikali si wa chama. Ufafanuzi zaidi rudi ktk post za nyuma.

Kinachosumbua hapa ni mazoea, utaratibu ambao kamwe si sheria wala kanuni za nchi.
 
View attachment 520423 Mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema yeye bado ni mwenyekiti wa ACT-Wazalendo na ataendelea kushika wadhfa huo kama kawaida. Mghwira aliyeapishwa Jumanne kuanza kazi, ametoa maelezo hayo katika mahojiano mahsusi na mwandishi Jamal Hashim wa Azam TV.

Amedai mbona Lipumba aliwai kuwa mshauri wa Museni Uganda yeye kuwa RC Kilimanjaro ndo iwe nongwa?

Anauwezo wa kuwa RC na kuwa mwenyekiti wa ACT
ATC wameamua kumsaidia ili atimize wajibu wa kazi za RC na majukumu yake mepya kwa utulivu.

Link News Alert: - Anna Mghwira avuliwa uenyekiti ACT-Wazalendo, Yeremia Maganja awa Makamu mwenyekiti
 
HUYU mama kukubali kuchukuwa nafasi ya Ukuu wa mkowa hakufanya kosa, na wala uamuzi huo sio weakness, ni moyo wa kuwatumikia Watanzania. Busara ya wanawake wanajenga na wanataka piece kwa Watanzania wote. Wanaume kwaajili mala nyingi kwa ubinafsi wenu, mnataka kushinda, hata kama ushindi wenu utakuta madhara kwenye familia zenu. Sasa kuna kosa gani hapo amefanya? Agekataa ndiyo angekuwa sio weak? Angekataa angekuwa sio mama mwenye majukumu ya kuitumikia nchi yake. Upinzani sio vita na serikali, upinzani nikutowa mawazo kwa serikali kama imekosea, na kuiunga mkono kama imefanya vizuri. Kitu ninachoona kwa wapinzani ni vita tu, tutajengaje nchi yetu kama vyama vya siasa vinazuwa vita? Obama wakati alichukuwa madaraka kawachaguwa watu watatu kwenye cabinet yake kutoka kwenye upinzani, wote wanaume na huwezi kusema wako weak kwa kuwa walikubali hizo apoointment, ni wanatumikia nchi yao na wamekomaa kidemokrasia. Lazima tukubali kutokubaliana bila ya chuki.

Robert Gates assumed the office of Secretary of Defense on December 18, 2006, under then-President George W. Bush. The retention of Gates fulfilled Obama's pledge made on the campaign trail to have a Republican in his Cabinet.


Robert Gates aliyekuwa Secretary of defence tarehe 18/12/2006 kwenye utawala chini ya George Bush , Obama alimuacha aendelee na kazi yake. Obama aliahidi kuwaweka Republican kati ya mawaziri wake.
 
TAARIFA KWA UMMA
MAAMUZI YA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI JUU YA UENYEKITI WA CHAMA CHA ACT Wazalendo
Tarehe 3 Juni, 2017 Mwenyekiti wa chama chetu cha ACT Wazalendo, Mama Anna Elisha Mghwira aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kufuatia uteuzi huu, Kamati ya Uongozi wa Chama ilikutana leo tarehe 7, Juni 2017 kutafakari juu ya matokeo ya uteuzi huu katika utekelezaji wa majukumu yake ya Uenyekiti na mustakabali wa siasa za Chama chetu na mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi nchini kwetu. Katika tafakari yake, Kamati ya Uongozi imezingatia yafuatayo:
Kama Chama hatuna kipingamizi kwa Mama Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa, wala kumzuia ndugu Rais kumteua mtanzania yoyote na haswa mwana ACT Wazalendo kutumikia Taifa letu. ACT Wazalendo ni chama cha siasa na azma yake ni kutumikia Taifa.
Kamati ya Uongozi inampongeza Rais kwa kuvunja miiko ya siasa za Tanzania kwa kuanza kuteua wapinzani katika utumishi wa umma. Uteuzi wa mara ya pili wa ndugu Rais kwa wanachama na viongozi wa ACT Wazalendo ni kielelezo kuwa chama chetu kinao watu makini na wanaofaa kuongoza. Ni uthibitisho kuwa ACT inapaswa kupewa nafasi ya kuongoza nchi katika uchaguzi ujao. Tunapenda kumhakikishia ndugu Rais kuwa tunao watu waadilifu na wazalendo wengine wengi ndani ya ACT kama jina la chama chetu linavyojipambanua yaani ACT- Wazalendo. Asichoke na asisite kuja kuvuna na wengine maana tumeonyesha uwezo wa kutengeneza wengi wa aina hiyo. Muhimu zaidi, Chama chake cha CCM kijifunze kutoka kwetu namna ya kuchagua na kuvutia viongozi waadilifu na wazalendo katika chama chao.
Kamati ya Uongozi inashauri Rais au mamlaka yoyote ile ya uteuzi kuweka mfumo bora wa kuazima watu kutoka vyama vingine kumsaidia kazi za Maendeleo ya Nchi Kwa kufanya Mashauriano na Vyama husika ili kuepuka migongano isiyo ya lazima ndani ya vyama na katika jamii. Pamoja na kwamba Rais kama Mkuu wa Nchi anayo mamlaka ya kuteua yeyote amtakaye, lakini ni Afya na hekima teuzi hizo kufanywa kwa kushauriana na Viongozi wa Vyama husika ambavyo anachukua wanachama wake. Hii haitakuwa kuingilia mamlaka yake ya Kikatiba bali kuimarisha Umoja wa Kitaifa na hata Mfumo wa Vyama Vyama vingi nchini. Kuteua bila ya mashauriano kunaleta wasiwasi wa dhamira mbaya na kuathiri taswira ya vyama vya upinzani ambavyo Rais anachukua wanachama wake.
Kwa hiyo basi;
a. Kamati ya Uongozi imempongeza Mama Anna Elisha Mghwira Kwa kutambuliwa na hatimaye kuteuliwa na Rais kushika nafasi muhimu ya Mkuu wa Mkoa.
b. Kufuatia uteuzi wake kuwa Mkuu wa Mkoa, Kamati ya Uongozi imezingatia kuwa kutakuwa na mgongano wa moja kwa moja wa kiutendaji na kitaswira kati ya majukumu ya Uenyekiti wa chama na majukumu yake mapya, jambo linaloweza kuathiri Ufanisi wa moja wa nafasi hizi mbili.
c. Kwa mujibu wa Ibara ya 17(1)(iii) ya Katiba ya ACT Wazalendo na kutokana na mashauriano kati ya Mama Anna Mghwira na viongozi wenzake wakuu wa Chama, Mama Anna Mghwira amekoma kuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo. Ibara ya 17(1)(iii) ya Katiba ya ACT inamfanya Kiongozi wa Chama kukoma kushika nafasi yake iwapo atashindwa kutekeleza majukumu yake. Ni dhahiri kuwa kwa kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa, Mama Anna Mghwira hawezi tena kutekeleza kwa ufanisi wajibu huu.
d. ACT Wazalendo, inamshukuru Mama Mghwira kwa muda, mchango, nguvu, busara na hekima zake alizozitumia katika muda wote wa Uenyekiti wake, na tunamtakia kila la kheri katika kutumikia nafasi yake mpya.
e. Mwisho, Kamati ya Uongozi (Kwa mujibu wa Ibara za 29(24) ya Katiba ya ACT Wazalendo imemteua Ndugu Yeremia Kulwa Maganja kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama Taifa hadi uchaguzi Mkuu utapoitishwa Mwezi Machi 2018.
Ahsanteni Sana.
Samson Maingu Mwigamba
Kaimu Kiongozi wa Chama
Juni 7, 2017
Dar es salaam
 
View attachment 520423 Mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema yeye bado ni mwenyekiti wa ACT-Wazalendo na ataendelea kushika wadhfa huo kama kawaida. Mghwira aliyeapishwa Jumanne kuanza kazi, ametoa maelezo hayo katika mahojiano mahsusi na mwandishi Jamal Hashim wa Azam TV.

Amedai mbona Lipumba aliwai kuwa mshauri wa Museni Uganda yeye kuwa RC Kilimanjaro ndo iwe nongwa?

Anauwezo wa kuwa RC na kuwa mwenyekiti wa ACT
Huyu mama naye karogwa itakuwa.
 
Huyu mama ameinajisi ACT na Upinzani kwa Ujumla ...... Anapaswa kuomba radhi mara moja.
 
Mwenyekiti wa CCM ni Raisi wa nchi

Mwenyekiti wa ACT ni mkuu wa mkoa.....



Mama Anna karibu sana Kilimanjaro. ....
 
Back
Top Bottom