Ziara na Mikutano ya hadhara ya viongozi wa ACT Wazalendo na mabadiliko ya sheria ya TISS

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Katika ziara za viongozi wa chama Mh.Zitto Zuberi Kabwe , Mwenyekiti Babu Duni na Makamu Mwenyekiti Dorothy Semu moja ya jambo ambalo limeelezewa kwa unyeti ni suala la mabadiliko ya sheria ya usalama wa Taifa.

Suala hili ACT wazalendo tumekuwa tukilipigia kelele sana kwamba kuna haja kubwa idara ya usalama wa Taifa kufanyiwa mabadiliko ili kuendana na mabadiliko ya sasa ya kidunia ,kiuchumi,kibiashara na ushindani kati ya nchi na nchi au mashirika ili kulinda Maslahi ya Taifa.

Kiongozi wa chama Ndg.Zitto akiwa katika ziara Katavi ,Makambako ,Songea na maeneo mengine anasema muswada wa sheria huu wa sheria ya usalama wa Taifa 60% ina mambo mazuri sana ila 40% ina mapungufu hivyo tusiuharakishe kuupitisha Bungeni ila upewe muda wa kutosha kujadiliwa sababu kuna mambo ya haki za watu kama kumuwekea Afisa usalama Kinga ya jinai "Criminal Immunity" kwamba asishtakiwi ikiwa atafanya kosa katika utendaji wake.Hili ni jambo ambalo sote kwa pamoja tunapaswa kuiambia serikali na wabunge kwamba vifungu vya namna hii viondolewe,tusichoke kusema na kukosoa .ACT wazalendo tunaona hatari kubwa dhidi ya haki za watu ikiwa vifungu vya namna hiyo vitapitishwa.

Jambo lingine ambalo nimependa kusikia kiongozi ndug.Zitto akilizungumzia ni suala la kuifanyia mabadiliko makubwa idara yetu ya usalama wa Taifa ili iendane na wakati katika kulinda Maslahi ya Taifa kiuchumi dhidi ya nchi zingine hivyo akisema ni vyema tuwe na kitengo cha External Intelligence/Foreign Intelligence/ Economic Intelligence kitengo ambacho kutakuwa na uwezo wa kukusanya taarifa kuhusu masuala ya kiuchumi, kibiashara,uwekezaji na ushindani kati ya nchi yetu na nchi zingine ili kulinda Maslahi ya nchi yetu dhidi ya nchi zingine.

Nchi nyingi sana sasa hivi zina vitengo namna hii ,kwa sasa nchi nyingi duniani zimeingia katika ushindani na kulinda maslahi yao kiuchumi na kibiashara kwa maslahi ya nchi zao na mataifa yao dhidi ya nchi zingine ,hata sisi Tanzania bado hatujachelewa kufanya hivyo.Katika Thesis ya Valentyn Levytaskyi itwayo "Economic Intelligence of the Modern State ya 2001 " ameelezea vizuri sana kuhusu umuhimu wa nchi kuwa na kitengo cha ujasusi wa kiuchumi (Economic Intelligence/External intelligence/Foreign Intelligence).

Marekani walifanya hivyo 1949 walirekebisha sheria yao ya ujasusi ya 1947 na kuweka kitengo cha "Office of economic Research Report".Bado hatujachelewa nchini kwetu pia nchi nyingi za Afrika wana vitengo hivi ,tutangulize Maslahi ya Taifa letu mbele katika mabadiliko ya sheria hii.

Kuna makosa kadhaa ya wazi wazi na ya aibu yaliwahi kutokea nchini ,sababu kubwa ni nchi yetu kukosa kitengo hiki .

Mnakumbuka Desemba 2021 Mh. Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kuzungumza kwa uchungu kuhusu serikali kuingia mkataba na kampuni ya Kituruki (Yutek Gemi San Ltd ) ya ujenzi wa meli 5 ,takribani Tsh. Bil.400 .

Rais Samia alisema mkataba huo uliingiwa tar 15 Juni 2021 huko Mwanza kati ya Serikali kupitia kampuni ya huduma za Meli Tanzania (MSCL) na kampuni hiyo ya Kituruki itwayo YUTEK GEMI SAN LTD.

Katika kufuatilia utekelezaji wa ujenzi wa meli hizo baada ya kuunda timu ya ufuatiliaji ,Rais Samia anasema mambo kadhaa waliyabaini yenye kutia wasiwasi.

1.Timu iligundua Mkandarasi huyo wa kampuni ya Yutek haina eneo lake la ujenzi wa meli yaani Ship-yard isipokuwa ni madalali tuu.

2.Timu iligundua uwezo wa kifedha wa kampuni hiyo ya Yutek ni mdogo mno na Timu hadi inaondoka haijapewa taarifa zozote za kifedha.Na kampuni hiyo haikufanya chochote kuhusu ujenzi wa Meli.

Makosa mengine yamekuwa yakijitokeza na ya aibu sana ,itakumbukwa tar 30 , Januari 2019.Serikali iliingia mkataba huko Arusha na kampuni ya Indo-Power Solutions Ltd ya nchini kenya chini ya Mkurugenzi wake Brian Mutembei ili kununua korosho tani laki moja zenye thamani ya Tsh.Bil.418 .Ila mwezi wa 5 ,2019 serikali ikavunja mkataba na kampuni hiyo baada ya kugundulika kampuni hiyo ni ya kijanja kijanja na ni madalali ,hii ni aibu kwa Taifa na ni hali ya kuhatarisha Maslahi ya kiuchumi ya nchi yetu.

Ila tukiwa na kitengo cha external intelligence/Foreign Intelligence au Economic Intelligence kama ambavyo ACT-Wazalendo tunapendekeza ni rahisi sana "Due Diligence" yaani uchunguzi na ukaguzi kabla ( Complete review and Audit) kufanyika kabla ili kujua hali ya kampuni au nchi tunayoingia nayo makubaliano au mkataba huo kabla ya kuingia mkataba wenyewe ili kujua uwezo wa kifedha wa kampuni hiyo (Financial Due Diligence),uhalali wa kampuni hiyo kisheria (Legal due Diligence),uwezo wake katika kufanya kazi (Operational Due Diligence) na mambo mengine, hii ni hatua ya awali kabisa kabla ya kuingia mkataba na hii ndiyo njia itayosaidia kulinda Maslahi yetu .

ACT wazalendo tunashauri tusiharakishe mabadiliko ya sheria yetu ya usalama wa Taifa , tufanye marekebisho ya sheria yetu huku tukitanguliza Maslahi ya nchi yetu mbele,ni muda sasa kupitia marekebisho ya sheria hii tuweke na kitengo kitakachojikita na masuala ya ujasusi wa kiuchumi na mambo ya nje External intelligence/Foreign Intelligence /Economic Intelligence ndio itakuwa na kazi ya kukusanya taarifa za kiuchumi,ushindani , uwekezaji kati ya nchi yetu na nchi zingine au mashirika mengine na kuishauri serikali ili kulinda Maslahi ya Taifa letu.

Abdul Nondo .

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa-ACT Wazalendo.

01/Juni/2023.
 
Ukitaka kumficha mtu kitu tanzania, weka kwenye maandishi. Au kieke kwenye story ya ngono, hapo atajaribu kusoma
Inategemea maandishi ya aina gani. Maana kuna chama ambacho ni ngumu kueleweka kina mlengo gani, kuanza kujaza free bites za brain, kulinda maslahi yao binafsi
 
Nondo umeandika vema kabisa. ILA: Haki haibembelezwi, lugha yako yako ni ya kuomba hisani. Samia hawezi maana kukupa hisani ya unachokitafuta. She is still, as of now consolidating power. She is becoming agressive supreme of power.
sasa wewe mtaalamu suggest tunamshinikizaje Samia? hillo ndilo la msingi ambalo ungelimaliza nalo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom