Makubaliano yamefanywa Muungano umevunjwa rasmi bila maandishi wala tangazo na Zanzibar inaruhusiwa kujifanyia kila kitu isipokuwa kuwa na jeshi

Nashangaa sana kwamba Watanzania wengi, hasa watu wa bara, hawajagundua kwamba awamu ya sita imevunja muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar bila maandishi au matangazo. Hadi sasa kuna makubaliano kwamba Zanzibar watajifanyia kila kitu ambacho nchi rasmi inafanya isipokuwa hawatakuwa na jeshi la ulinzi.

Na kuna makubaliano kwamba serikali ya muungano haitaingilia jambo lolote au kutoa maelekezo yeyote upande wa Zanzibar kwa sababu sasa wamekuwa kama serikali kamili. Hata ziara za viongozi wa serikali ya muungano kule Zanzibar zimedhibitiwa. Na pia mabalozi wa nje wanapewa nafasi zao, na nadhani raisi wa Zanzibar ndie anateua watu wake na raisi wa Tanzania kutangaza rasmi.

Haya yote yamefanyika kimya kimya, na naweza kudiriki kusema yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika mazingira ya kuwa na raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar. Hiyo imeonekana ni zile nafasi zinaitwa "it is now or never".

Ila jambo la kusikitisha ni kwamba katika hali hii Zanzibar ni kama imepewa fursa kubwa ya kujiendeleza haraka hasa katika miundo mbinu kwa sababu yajayo hayajulikani. Kama umeangalia vizuri, kuna miradi mikubwa ya miundo mbinu inayoendelea huko visiwani, pamoja na kubadilisha majengo ya shule karibu yote. Umewahi kujiuliza Zanzibar wanapata wapi fedha za kufanya haya mambo makubwa?

Ni kwamba, mbinu iliyotumika ni Tanzania kuchukua mikopo ya nje, ambapo sehemu kubwa sana ilienda Zanzibar kama gawio lao. Ile mikopo haikuwa kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania bara, mlengwa alikuwa Zanzibar. Ndio maana baadhi ya wanasiasa wa bara, walipogundua hilo walikasirika sana. Na tukumbuke kuwa daraka kubwa la kulipa hii mikopo liko Tanzania bara.

Ni kweli kwamba kuna fedha zinabaki Tanzania bara lakini faida kubwa ya ile mikopo ilikuwa ni kwa ajili ya Zanzibar. Tukichukua mkopo wa tuseme Trilioni 10, ukawapa Zanzibar gawio lao la trilioni mbili, zile trilioni mbili zinazoenda Zanzibar ni fedha nyingi sana kufanyia mambo mengi sana, wakati trilioni nane zinazobaki bara impact yake kuona zimefanya nini ni kidogo sana kwa sababu ya ukubwa wa nchi. Na ukweli ni kwamba mfumo wa gawio ulitengenezwa kwa kupendelea upande wa Zanzibar.

Sasa jambo ambalo limeanza kuwaamsha watu wa bara ni hili la meli za nje kusajiliwa Zanzibar. Kwa kiburi kabisa, pamoja na skendo zilizolikumba jina la Tanzania, Zanzibar wanadai tulishakubaliana tunajiendesha kama nchi kamili, na tuna haki ya kusajili meli. Wanadai kama hatutaki watumie jina la Tanzania basi mabadiliko yafanywe wazisajiri kwa jina la Zanzibar.

Na pia kuna baadhi ya wanasiasa wanahoji, kama Zanzibar wanaruhusiwa kujifanyia kila kitu kama nchi na kutoingiliwa, kwa nini bado wanateuliwa kwenye nafasi zinazohusu muungano au hata mambo ya bara peke yake? Baadhi ya majibu wanayopewa ni kwamba raisi ana uhuru wa kuteua timu yake ambayo itaona itamsaidia, na anaweza kuchukua watu bara au visiwani katika nafasi yeyote.

Kwa hiyo kila mtu akae akijua muungano haupo tena, makubaliano yamefanywa Zanzibar wajifanyie kila kitu isipokwa kuwaja jeshi, lakini makubaliano haya hayatatangazwa rasmi.
Uongo hauna manufaa yoyote yale
 
zanzibar ni mali ya english monarchy, tanganyika ilitumiwa na inatumiwa tu ktk indirect rule ya zanzibar, hawataki (english monarchy) kudili na hao muslims ( ~98% ya zanzibar ni muslim) moja kwa moja hivyo wanatusukumizia sisi lkn zanzibar inabakia english monarch’y property sisi (tanganyika) ni gatekeeper tu.

imposing Anglikan Church - Zanzibar …

View attachment 3549496
Watanganyika wanajidanganya eti wanataka kuidhibiti Zanzibar kwa visingizio vya kiini macho. Hakuna kuwa ni mali ya english monarchy. Akiwa kiongozi anatoka Bara haya huyasikii lkn akikaa Mzanzibari unasikia ufukunyuku tele. Ni undumila kuwili. Zanzibar iliyostawi itendelea kuwepo wacha watu wajidanganye na kujitekenya. Kama kweli Zanzibar inawakera wavunje muungano kila mtu abaki kwao, ila hawafanyi kwasababu ni wanafiki.
 
Mkuu swala la kuvunja muungano lilishafanywa tokea awamu ya kwanza na ikaendelea awamu zilizotangulia. Mfano:
1. Kuvunja makubaliano ya muungano
2. Kuongeza idadi ya orodha ya mambo ya muungano
3. Kuondoa nafasi ya Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa JMT
4. Kutokuitisha bunge la katiba ndani ya miezi 6 baada ya kusaini makubaliano ya muungano.

Nimeonesha haya ambayo yamefanywa na awamu zilizopita. Sasa kama ni kuvunjwa muungano katika awamu hii, swala hili lilipaswa lisemwe katika awamu zilizotangulia kwani kimsingi na kisheria huu muungano ulishauliwa zaidi ya miaka 60 iliyopita.

Ni kweli huu muungano haupo na lililopo ni Tanganyika
kujaribu kuidhibiti Zanzibar kimabavu
, ila kwa bahati Zanzibar ipo na itaendelea kuwepo iwe ndani ya muungano au nje ya muungano.

Na haya makubaliano yalifanywa Zanzibar? Tuliungana nchi mbili kwa hiari ya viongozi wa nchi hizi huru zenye mamlaka. Awamu ya sita imeyakuta.

Ni kweli kwa mfano uliotoa fedha zinafanya mambo mengi lkn jee zinapelekwa kama unavyodai? Jawabu ni hapana. Jee ulitaka zisifanye mambo mengi? Ubinafsi.

Mkuu huu muungano, kwa mujibu wa Karume senior, ni kama koti; ukiona linakubana unalivua. Fanyeni hivyo ili tupumue. Mukiendelea na fikra za kuidhibiti Zanzibar, hii nchi itakushindeni kwani ilishawashinda wengi.
Maelezo yako yanaeleweka. Binafsi nimekuwa na mashaka sana na makusudio ya Nyerere kuhusu Zanzibar na Muungano wa serikali mbili. It's always been suspicious.

Lakini unakosea kwenye muktadha uliopo (current context of the union). Hicho unachoita Tanganyika kutaka kuidhibiti Zanzibar kimabavu huenda ni wazo lililokuwepo hapo awali enzi za muasisi Nyerere. Haiko hivyo leo hii.

Kilicho dhahiri ni Kundi la wanasiasa wa CCM huko Zanzibar (wenye misingi ya ASP) ndio wenye maslahi makubwa na huu muungano. Bila hivyo, hawawezi kuwa madarakani. Hivyo wameshikamana na wenzao wa Tanganyika kuendeleza udikteta wa chama dola huko Zanzibar kwa maslahi yao binafsi.

Kama unaamini nyinyi Wazanzibari mko pamoja mnataka kupumua toka udhibiti wa Tanganyika, unajidanganya sana. Tatizo haliko kwa Watanganyika. Nao ni victims tu wa mfumo wa CCM uliotengenezwa na Nyerere wa chama dola. Viongozi wenu huko Zanzibar walioko CCM/ASP hawataki Zanzibar huru: wanautaka muungano na kuenzi "mapinduzi matukufu"ya 1964" ili waendelee kufaidi fursa zote Tanganyika na Zanzibar.

You have to think bigger for a real solution to this unscrupulous union.
 
Watanganyika wanajidanganya eti wanataka kuidhibiti Zanzibar kwa visingizio vya kiini macho. Hakuna kuwa ni mali ya english monarchy. Akiwa kiongozi anatoka Bara haya huyasikii lkn akikaa Mzanzibari unasikia ufukunyuku tele. Ni undumila kuwili. Zanzibar iliyostawi itendelea kuwepo wacha watu wajidanganye na kujitekenya. Kama kweli Zanzibar inawakera wavunje muungano kila mtu abaki kwao, ila hawafanyi kwasababu ni wanafiki.

hakuna mwenye uwezo wa kuuvunja muungano kwa maana hawajauweka wao, zanzibar ni mali ya english monarchy, muungano wa tanganyika na zanzibar ni copy & paste ya muungano wa great britain (england, scottland na ireland) ni 1:1 hakuna sehemu nyingine yoyote ile duniani kuna muungano wa aina hiyo uko gb na hapa kwetu tu basi.

zanzibar haijawahi kupata uhuru ktk kwa mkoloni ulishawahi kujiuliza hilo? uingereza hakuipa zanzibar uhuru kama vile ilivyofanya makoloni yake mengine bali mwaka 1963 ilimkabidhi sultani kwa hiari kabisa na makubaliano kwamba inabakia (zanzibar) english monarchy mwaka mmoja baadaye mapinduzi yakatokea yaliongozwa na sijui okelo kutoka ug, iweje mganda (ug -english empire)?

je, kuna sherehe ya uhuru zanzibar ktk kwa english monarchy? jibu la hilo swali litakufungua macho, isitoshe jiulize kwa nini wazanzibari wote wanakimbilia uingereza kuanzia communist a.babu, sultani na wengineo, zanzibar wana ukaribu sana gb klk tanganyika unafahamu ni kwa nini? ...
 
Maelezo yako yanaeleweka. Binafsi nimekuwa na mashaka sana na makusudio ya Nyerere kuhusu Zanzibar na Muungano wa serikali mbili. It's always been suspicious.

Lakini unakosea kwenye muktadha uliopo (current context of the union). Hicho unachoita Tanganyika kutaka kuidhibiti Zanzibar kimabavu huenda ni wazo lililokuwepo hapo awali enzi za muasisi Nyerere. Haiko hivyo leo hii.

Kilicho dhahiri ni Kundi la wanasiasa wa CCM huko Zanzibar (wenye misingi ya ASP) ndio wenye maslahi makubwa na huu muungano. Bila hivyo, hawawezi kuwa madarakani. Hivyo wameshikamana na wenzao wa Tanganyika kuendeleza udikteta wa chama dola huko Zanzibar kwa maslahi yao binafsi.

Kama unaamini nyinyi Wazanzibari mko pamoja mnataka kupumua toka udhibiti wa Tanganyika, unajidanganya sana. Tatizo haliko kwa Watanganyika. Nao ni victims tu wa mfumo wa CCM uliotengenezwa na Nyerere wa chama dola. Viongozi wenu huko Zanzibar walioko CCM/ASP hawataki Zanzibar huru: wanautaka muungano na kuenzi "mapinduzi matukufu"ya 1964" ili waendelee kufaidi fursa zote Tanganyika na Zanzibar.

You have to think bigger for a real solution to this unscrupulous union.
Hii comment nitajitolea kumpigia lamination akae nayo kwake awe anasoma.
 
Nashangaa sana kwamba Watanzania wengi, hasa watu wa bara, hawajagundua kwamba awamu ya sita imevunja muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar bila maandishi au matangazo. Hadi sasa kuna makubaliano kwamba Zanzibar watajifanyia kila kitu ambacho nchi rasmi inafanya isipokuwa hawatakuwa na jeshi la ulinzi.

Na kuna makubaliano kwamba serikali ya muungano haitaingilia jambo lolote au kutoa maelekezo yeyote upande wa Zanzibar kwa sababu sasa wamekuwa kama serikali kamili. Hata ziara za viongozi wa serikali ya muungano kule Zanzibar zimedhibitiwa. Na pia mabalozi wa nje wanapewa nafasi zao, na nadhani raisi wa Zanzibar ndie anateua watu wake na raisi wa Tanzania kutangaza rasmi.

Haya yote yamefanyika kimya kimya, na naweza kudiriki kusema yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika mazingira ya kuwa na raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar. Hiyo imeonekana ni zile nafasi zinaitwa "it is now or never".

Ila jambo la kusikitisha ni kwamba katika hali hii Zanzibar ni kama imepewa fursa kubwa ya kujiendeleza haraka hasa katika miundo mbinu kwa sababu yajayo hayajulikani. Kama umeangalia vizuri, kuna miradi mikubwa ya miundo mbinu inayoendelea huko visiwani, pamoja na kubadilisha majengo ya shule karibu yote. Umewahi kujiuliza Zanzibar wanapata wapi fedha za kufanya haya mambo makubwa?

Ni kwamba, mbinu iliyotumika ni Tanzania kuchukua mikopo ya nje, ambapo sehemu kubwa sana ilienda Zanzibar kama gawio lao. Ile mikopo haikuwa kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania bara, mlengwa alikuwa Zanzibar. Ndio maana baadhi ya wanasiasa wa bara, walipogundua hilo walikasirika sana. Na tukumbuke kuwa daraka kubwa la kulipa hii mikopo liko Tanzania bara.

Ni kweli kwamba kuna fedha zinabaki Tanzania bara lakini faida kubwa ya ile mikopo ilikuwa ni kwa ajili ya Zanzibar. Tukichukua mkopo wa tuseme Trilioni 10, ukawapa Zanzibar gawio lao la trilioni mbili, zile trilioni mbili zinazoenda Zanzibar ni fedha nyingi sana kufanyia mambo mengi sana, wakati trilioni nane zinazobaki bara impact yake kuona zimefanya nini ni kidogo sana kwa sababu ya ukubwa wa nchi. Na ukweli ni kwamba mfumo wa gawio ulitengenezwa kwa kupendelea upande wa Zanzibar.

Sasa jambo ambalo limeanza kuwaamsha watu wa bara ni hili la meli za nje kusajiliwa Zanzibar. Kwa kiburi kabisa, pamoja na skendo zilizolikumba jina la Tanzania, Zanzibar wanadai tulishakubaliana tunajiendesha kama nchi kamili, na tuna haki ya kusajili meli. Wanadai kama hatutaki watumie jina la Tanzania basi mabadiliko yafanywe wazisajiri kwa jina la Zanzibar.

Na pia kuna baadhi ya wanasiasa wanahoji, kama Zanzibar wanaruhusiwa kujifanyia kila kitu kama nchi na kutoingiliwa, kwa nini bado wanateuliwa kwenye nafasi zinazohusu muungano au hata mambo ya bara peke yake? Baadhi ya majibu wanayopewa ni kwamba raisi ana uhuru wa kuteua timu yake ambayo itaona itamsaidia, na anaweza kuchukua watu bara au visiwani katika nafasi yeyote.

Kwa hiyo kila mtu akae akijua muungano haupo tena, makubaliano yamefanywa Zanzibar wajifanyie kila kitu isipokwa kuwaja jeshi, lakini makubaliano haya hayatatangazwa rasmi.
Punguzeni chuki punguzeni kuendekeza umaskini wa vichwani.

Samia kajenga madarasa ya shule mbalimbali zaidi ya 50,000 kwa miaka minne.

Kajenga shule za amali 103 nchi nzima kwa miaka minne.

Kajenga meli nne kule Ziwa Tanganyika kapeleka ambulance kwa ajili ya wagonjwa wa visiwa vya Ziwa Victoria.

Kaimalizia Dodoma hivi sasa limekuwa jiji linalotazamika ndani ya miaka minne.

DP World wameongeza ufanisi pale TPA kule Bandari ya Tanga zimetumika bilioni 600 kwa ajili ya ukarabati.
Mnataka Samia awe anatugongea milango akituletea chakula cha mchana na jioni!, stupid kabisa!!.

Huu ujinga kwamba Zanzibar inapendelewa wakati fursa zimetengenezwa nyingi sana huku bara ndani ya miaka minne unapozidi kuendekezwa unatuchoresha sisi watu wa huku Bara, tunaonekana mabogus tusiojielewa duniani tunataka kitu gani.

Kwao ni Kizimkazi Unguja, hajajali anapotoka yeye yupo kimaendeleo zaidi.
 
Licha ya kujitutumua Zanzibar Haina capacity hiyo ya kucolonjze Tanganyika, wasiwasi wangu ni kwa WaZanzibar wanaoishi bara siku Tanganyika ikifufuka watajificha wapi, maana itakuwa kilio na kusaga meno.
Kabla ya tarehe 9 desemba wazanzibari wengi walipanda meli wakaenda kwao, walijua vurugu zingetokea wasingebakia salama.

Hizi ni roho za kibaguzi roho za kutengana zinaongozwa na ushetani unaoishi ndani ya binadamu.

Awamu ya tano jukwaa hili hili lilimsimanga hayati JPM kwa kusema Chato imekuwa nchi ndani ya Tanzania!.
Wananzengo wakajitokeza na kumtetea JPM kwa kuhoji iwapo chato ipo ndani au nje ya JMT.
 
Watanganyika wanajidanganya eti wanataka kuidhibiti Zanzibar kwa visingizio vya kiini macho. Hakuna kuwa ni mali ya english monarchy. Akiwa kiongozi anatoka Bara haya huyasikii lkn akikaa Mzanzibari unasikia ufukunyuku tele. Ni undumila kuwili. Zanzibar iliyostawi itendelea kuwepo wacha watu wajidanganye na kujitekenya. Kama kweli Zanzibar inawakera wavunje muungano kila mtu abaki kwao, ila hawafanyi kwasababu ni wanafiki.
Roho za kibaguzi. Wale wabunge wa G55 ukitazama kwa undani wengi ni wakristo wenzangu walianzisha vuguvugu lile kwa sababu Rais alikuwa hayati Mwinyi. Alipoondoka hakuna mtu aliyehoji muungano.

Kuja kwa SSH warasimu ambao wengi ni wakristo wamekuja upya wakianzisha tena ujinga ule ule wa G55.
 
Haya yote yanatokea kwa makusudi, msemaji wa serikali ametamka kwa uwazi usajili umefanyika Zanzibar, kwani Zanzibar unaitenganishaje na Tanzania?
 
Nashangaa sana kwamba Watanzania wengi, hasa watu wa bara, hawajagundua kwamba awamu ya sita imevunja muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar bila maandishi au matangazo. Hadi sasa kuna makubaliano kwamba Zanzibar watajifanyia kila kitu ambacho nchi rasmi inafanya isipokuwa hawatakuwa na jeshi la ulinzi.

Na kuna makubaliano kwamba serikali ya muungano haitaingilia jambo lolote au kutoa maelekezo yeyote upande wa Zanzibar kwa sababu sasa wamekuwa kama serikali kamili. Hata ziara za viongozi wa serikali ya muungano kule Zanzibar zimedhibitiwa. Na pia mabalozi wa nje wanapewa nafasi zao, na nadhani raisi wa Zanzibar ndie anateua watu wake na raisi wa Tanzania kutangaza rasmi.

Haya yote yamefanyika kimya kimya, na naweza kudiriki kusema yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika mazingira ya kuwa na raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar. Hiyo imeonekana ni zile nafasi zinaitwa "it is now or never".

Ila jambo la kusikitisha ni kwamba katika hali hii Zanzibar ni kama imepewa fursa kubwa ya kujiendeleza haraka hasa katika miundo mbinu kwa sababu yajayo hayajulikani. Kama umeangalia vizuri, kuna miradi mikubwa ya miundo mbinu inayoendelea huko visiwani, pamoja na kubadilisha majengo ya shule karibu yote. Umewahi kujiuliza Zanzibar wanapata wapi fedha za kufanya haya mambo makubwa?

Ni kwamba, mbinu iliyotumika ni Tanzania kuchukua mikopo ya nje, ambapo sehemu kubwa sana ilienda Zanzibar kama gawio lao. Ile mikopo haikuwa kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania bara, mlengwa alikuwa Zanzibar. Ndio maana baadhi ya wanasiasa wa bara, walipogundua hilo walikasirika sana. Na tukumbuke kuwa daraka kubwa la kulipa hii mikopo liko Tanzania bara.

Ni kweli kwamba kuna fedha zinabaki Tanzania bara lakini faida kubwa ya ile mikopo ilikuwa ni kwa ajili ya Zanzibar. Tukichukua mkopo wa tuseme Trilioni 10, ukawapa Zanzibar gawio lao la trilioni mbili, zile trilioni mbili zinazoenda Zanzibar ni fedha nyingi sana kufanyia mambo mengi sana, wakati trilioni nane zinazobaki bara impact yake kuona zimefanya nini ni kidogo sana kwa sababu ya ukubwa wa nchi. Na ukweli ni kwamba mfumo wa gawio ulitengenezwa kwa kupendelea upande wa Zanzibar.

Sasa jambo ambalo limeanza kuwaamsha watu wa bara ni hili la meli za nje kusajiliwa Zanzibar. Kwa kiburi kabisa, pamoja na skendo zilizolikumba jina la Tanzania, Zanzibar wanadai tulishakubaliana tunajiendesha kama nchi kamili, na tuna haki ya kusajili meli. Wanadai kama hatutaki watumie jina la Tanzania basi mabadiliko yafanywe wazisajiri kwa jina la Zanzibar.

Na pia kuna baadhi ya wanasiasa wanahoji, kama Zanzibar wanaruhusiwa kujifanyia kila kitu kama nchi na kutoingiliwa, kwa nini bado wanateuliwa kwenye nafasi zinazohusu muungano au hata mambo ya bara peke yake? Baadhi ya majibu wanayopewa ni kwamba raisi ana uhuru wa kuteua timu yake ambayo itaona itamsaidia, na anaweza kuchukua watu bara au visiwani katika nafasi yeyote.

Kwa hiyo kila mtu akae akijua muungano haupo tena, makubaliano yamefanywa Zanzibar wajifanyie kila kitu isipokwa kuwaja jeshi, lakini makubaliano haya hayatatangazwa rasmi.
Na huu ndo ulikuwa ugomvi mkubwa wa Ndugai na Bibi Shetani Samia,nakumbuka kwenye mgao wa pesa za uviko Ndugai alimuuliza Mwigulu,"huu utaratibu wa kugawa pesa kwa kutumia mfumo wa majimbo hauko sawa",alimuuliza hili swali mbele ya Samia..maana yake ukigawa pesa za uviko kwa kuangalia jimbo na sio idadi ya watu walioko kwenye jimbo,Zanzibar walipata pesa nyingi zaidi ya Bara kwa uwiano wa watu
 
Maelezo yako yanaeleweka. Binafsi nimekuwa na mashaka sana na makusudio ya Nyerere kuhusu Zanzibar na Muungano wa serikali mbili. It's always been suspicious.
Uko sawa. Haiaminiki kwamba mtu aseme ningekuwa na uwezo ningeitupilia mbali Zanzibar halafu useme uamuzi wake "is always been suspicious". Soma between the lines".
Lakini unakosea kwenye muktadha uliopo (current context of the union). Hicho unachoita Tanganyika kutaka kuidhibiti Zanzibar kimabavu huenda ni wazo lililokuwepo hapo awali enzi za muasisi Nyerere. Haiko hivyo leo hii.
Mkuu; kuwa na kumbukumbu. Maneno haya yamesemwa na kurudiwa miaka hii ya 2020s. Jikumbushe vizuri. Sisi tunazungumza kwa uhakika. Hali hiyo bado iko vilevile na kuzidi. Hii leo kwasababu kiongozi anatoka Zanzibar ndio malalamiko yanakuja kwa mawazo yaleyale eti ya kuidhibiti Zanzibar. Hakuna mabadiliko.
Kilicho dhahiri ni Kundi la wanasiasa wa CCM huko Zanzibar (wenye misingi ya ASP) ndio wenye maslahi makubwa na huu muungano. Bila hivyo, hawawezi kuwa madarakani. Hivyo wameshikamana na wenzao wa Tanganyika kuendeleza udikteta wa chama dola huko Zanzibar kwa maslahi yao binafsi.
Hapa umesema kweli.
Kama unaamini nyinyi Wazanzibari mko pamoja mnataka kupumua toka udhibiti wa Tanganyika, unajidanganya sana. Tatizo haliko kwa Watanganyika. Nao
Nikuhakikishie kwamba sijidanganyi. Kuna siku haki itasimama.
You have to think bigger for a real solution to this unscrupulous union
Let me assure you that I think bigger for a solution to this unscrupulous union and hope that soon this demon will cease to be in its real structure or existence.
 
Kabla ya tarehe 9 desemba wazanzibari wengi walipanda meli wakaenda kwao, walijua vurugu zingetokea wasingebakia salama.

Hizi ni roho za kibaguzi roho za kutengana zinaongozwa na ushetani unaoishi ndani ya binadamu.

Awamu ya tano jukwaa hili hili lilimsimanga hayati JPM kwa kusema Chato imekuwa nchi ndani ya Tanzania!.
Wananzengo wakajitokeza na kumtetea JPM kwa kuhoji iwapo chato ipo ndani au nje ya JMT.
Mbaguzi mkubwa ni huyo muuaji na mwanaye ambao Oct 29 waliwaleta wazanzibari kuja kuwaua Waanganyika. Mauaji yale yalidhihirisha kuwa hawa si wenzetu. Kutokana na uharamia ule, Wazenji wote wanatakiwa kufukuzwa, warudi kwao kwa maana wamethibitisha pasipo shaka kuwa ni maadui wakubwa wa Watanganyika.
 
Hakuna polisi yoyote aliyetoka Zanzibar, kile kilikuwa kikosi maalum cha polisi hufanya kazi maalum.

Punguza chuki na nongwa, hakuna mzenji aliyeua mtu huko mtaani, ndugu zetu walitushughulikia.
 
hakuna mwenye uwezo wa kuuvunja muungano kwa maana hawajauweka wao, zanzibar ni mali ya english monarchy, muungano wa tanganyika na zanzibar ni copy & paste ya muungano wa great britain (england, scottland na ireland) ni 1:1 hakuna sehemu nyingine yoyote ile duniani kuna muungano wa aina hiyo uko gb na hapa kwetu tu basi
Huenda unazungumzia mambo kwa kukisia tu. Muungano huu unafanana kidogo na ule wa GB lkn sio kwa kila kitu. Nikukumbushe Scotland walishapiga kura ya maoni kujitoa lkn ni Waskochi wenyewe waliukataa. Tanzania hilo limetokea?

Scotland wana Benki Kuu yao tofauti na ile ya UK. Hapa Tanzania hilo lipo?

Scotland wana fedha yao inayoitwa Scotland pound tofauti na Britidh pound. Jee hapa Tanzania ipo? Umezungumza vitu ninavyovijua. Tuendelee.
zanzibar haijawahi kupata uhuru ktk kwa mkoloni ulishawahi kujiuliza hilo? uingereza hakuipa zanzibar uhuru kama vile ilivyofanya makoloni yake mengine bali mwaka 1963 ilimkabidhi sultani kwa hiari kabisa na makubaliano kwamba inabakia (zanzibar) english monarchy
Sio kweli. Nadhani historia imekupita kidogo. Sultani alikabidhiwa hati ya uhuru kama Mzanzibari na sio mkoloni. Rejea yaliyotokea kwa yule aliyeitwa chachandu
je, kuna sherehe ya uhuru zanzibar ktk kwa english monarchy?
Unazungumza kama huijui Zabzibar na ndo iluvyo. Hakuna sherehe za uhuru kwasababu waliopindua wanadai uhuru wa Zanzibar ulipatikana kwa mapinduzi
 
Punguzeni chuki punguzeni kuendekeza umaskini wa vichwani.

Samia kajenga madarasa ya shule mbalimbali zaidi ya 50,000 kwa miaka minne.

Kajenga shule za amali 103 nchi nzima kwa miaka minne.

Kajenga meli nne kule Ziwa Tanganyika kapeleka ambulance kwa ajili ya wagonjwa wa visiwa vya Ziwa Victoria.

Kaimalizia Dodoma hivi sasa limekuwa jiji linalotazamika ndani ya miaka minne.

DP World wameongeza ufanisi pale TPA kule Bandari ya Tanga zimetumika bilioni 600 kwa ajili ya ukarabati.
Mnataka Samia awe anatugongea milango akituletea chakula cha mchana na jioni!, stupid kabisa!!.

Huu ujinga kwamba Zanzibar inapendelewa wakati fursa zimetengenezwa nyingi sana huku bara ndani ya miaka minne unapozidi kuendekezwa unatuchoresha sisi watu wa huku Bara, tunaonekana mabogus tusiojielewa duniani tunataka kitu gani.

Kwao ni Kizimkazi Unguja, hajajali anapotoka yeye yupo kimaendeleo zaidi.
Kwenye discussions kama hizi uwe unaruhusu to some extent freedom of speech. Usilazimishe mtu mwingine ampende mtu hampendi kwa sababu zake.

JPM tulimsema sana kutokana na weakness zake na zilikua valid. Huyu naye tunatumia standard ile ile kwa weakness zake.

Kavunja katiba ya chama, baadaye akaiba kura mwishowe akaua watu. Hiyo haina ubishi. Kabla ya hapo alitetea utekaji na uuaji. Biggest mistake na hii ndiyo causation, hamna mtu anayeanza tu kukusema bila sababu. The law of cause and effect.

Pleaseee
 
Wanasheria wote serikali wasione kwamba kavunja katiba ila sisi humu ndani tuone!!. Hii hoja ya Polepole ilishatupiliwa mbali kitambo.

Hana sababu ya kuiba kura kwa mengi sana aliyoyafanya tangu 2021 March ushahidi upo kila mahali.

Kuua watu ilitokea kwa sababu maalum, hatakuwa wa mwisho kuja na maamuzi hayo magumu.

Mkapa aliua watu kule Zanzibar mwaka 2001 akaomba msamaha kupitia kitabu chake.

Muungano upo, utakuwepo utalindwa kwa nguvu zote uendelee kuwepo.
 
Huenda unazungumzia mambo kwa kukisia tu. Muungano huu unafanana kidogo na ule wa GB lkn sio kwa kila kitu. Nikukumbushe Scotland walishapiga kura ya maoni kujitoa lkn ni Waskochi wenyewe waliukataa. Tanzania hilo limetokea?

Scotland wana Benki Kuu yao tofauti na ile ya UK. Hapa Tanzania hilo lipo?

Scotland wana fedha yao inayoitwa Scotland pound tofauti na Britidh pound. Jee hapa Tanzania ipo? Umezungumza vitu ninavyovijua. Tuendelee.

Sio kweli. Nadhani historia imekupita kidogo. Sultani alikabidhiwa hati ya uhuru kama Mzanzibari na sio mkoloni. Rejea yaliyotokea kwa yule aliyeitwa chachandu

Unazungumza kama huijui Zabzibar na ndo iluvyo. Hakuna sherehe za uhuru kwasababu waliopindua wanadai uhuru wa Zanzibar ulipatikana kwa mapinduzi

nitajie tofauti moja tu kati ya muungano wa gb na huu wetu, moja tu …
 
Back
Top Bottom