Makubaliano yamefanywa Muungano umevunjwa rasmi bila maandishi wala tangazo na Zanzibar inaruhusiwa kujifanyia kila kitu isipokuwa kuwa na jeshi

Wenye akili tunajua kuwa huu muunganao wa mchongo umeshavunjika kitambo sasa hivi kuna utumwa wa Tanganyika ndani ya Ukoloni wa Zanzibar.
 
Mkuu umetoa mfano wa mgawanyo wa fedha kwamba kama kukikopwa trl 10 basi 2 zaenda Zanzibar na miradi Zanzibar inaonekana kuliko bara hiyo inaweza ikawa ni kweli kutokana na kwamba huko zenj kiwango Cha ufisadi ni kidogo kuliko bara watu ni mafisadi sana hawana uchungu na Kodi za watz,hivyo huku bara kama tukipewa mgao wa 80% basi ujue itakayo enda kwenye malengo husika ni 30%, huku 50% ikiibwa
Bara kuna ufisadi ndio, na hizo zinazofisidiwa zingesaidia kutatua baadhi ya mambo, lakini haiondoi ukweli kwamba mikopo hii inapochukuliwa lengo ni kuipatia Zanzibar fedha za maendeleo kupitia mgongo wa Tanzania.

Na kama kuna ufisadi, kwani anaesimima nchi ni nani? Si huyo huyo anaechukua mikopo kwa ajili ya Zanzibar? Kwa nini hadhibiti huo ufisadi? Au ndio tuseme ana maslahi katika ufisadi unaofanywa bara ndio maana anauachia bila kuchukua hatua?

Unasema bara kuna ufisdi sana, nje nje, sasa tuambie, tangu huyu raisi achukue madaraka, wangapi umesikia wamekamatwa kwa ajili ya ufisadi? Huo ufisadi ambao hadi wewe unauona yeye hauoni kwa sababu anajiita chura kiziwi?
 
hasa kuimarisha KMKM na JKU, Zanzibar tayari ni free state, kombo akiamua kufanya kama diria huko nje kwa kiburi tu cha zanzibar kujiona ni nchi kamili kuna wa kukataa zanzibar isivunje katiba ya JMT?
Labda wafanye hivyo sasa wakati Samia wa Zanzibar ndio raisi. Kwa sababu wakifanya hivyo inakuwa ni uasi wa kama vile tu Kilimanjaro au Mtwara kujitangazia jeshi na uhuru wake. Amiri jeshi atachukua hatua ya kupeleka JWTZ kwenda kuzima uasi.

Sasa wakiasi sasa wakati Samia ndio raisi, yeye kama amiri jeshi mkuu anaweza kukataa kupeleka JWTZ Kuzima uasi wa Zanzibar. Lakini hiyo haitazuia baada ya kipindi cha Samia raisi ajae toka bara kuwaambia JWTZ nendeni mkarudishe madaraka kamili ya Tanzania kule Zanzibar - shoot to kill kama walivyofanya KMKM huku bara 29 October 2025. Sasa KMKM na JKU wataweza kupambana na JWTZ? Kwanza kuwapiga huhitaji hata kuweka boots on the ground in Zanzibar. Unawatwanga ukuwa huku huku bara - Bagamoyo hapo.

Unaona basi palivyo pagumu? Na ole wa Zanzibar hilolitokee na raisi ajae awe mtu asiempenda Samia. Mbona watakoma!
 
wakifanya uasi ndani ya utawala wa samia rais ajaye ataweza vipi kuirudisha kwenye muungano?
 
Kwa sababu unaweza ukafanya uasi, na uasi ukaendelea kwa kipindi fulani lakini haitahalalisha uasi wako kwa sababu umetawala nchi chini ya uasi kwa kipindi hicho. Kwa mfano. Urusi imeteka maeneo ya Ukraine na inayakalia kwa sasa. Anaweza kuja raisi miaka kadhaa baada ya Zelensky na kuyarudisha.

Na uasi wowote unaofanywa na nchi isitambuliwe kama nchi halali na Umoja wa Mataifa, basi bado inakuwa sio nchi. Jiulize, Zanzibar wakifanya uasi, UN watawatambua kama nchi kamili? Oman wanaweza kuwatambua, lakini bila UN kuwatambua bado wanakuwa si nchi halali, ni waasi.

Kwa hiyo ukifanya uasi, kupita kwa muda ukiwa katika nchi ya uasi hakuhalalishi uasi wako. Nchi uliyoifanyia uasi itakupa kibano kwa wakati na kiongozi muafaka

Nigeria, jimbo la Biafra lilijitenga, na hata Tanzania tukawaunga mkono. Lakini baadae Nigeria ilikuja kulirudisha chini ya himaya yake.
 
Wakuuu karibu Sana ugari dagaa nyasa na maji baridiiiiiii Sana! Hizi mbio sio za kushiba ukipata nafasi tembea hata peku inapunguza magojwa ya kisukal. Afya ni bora!
 
Nashangaa sana kwamba Watanzania wengi, hasa watu wa bara, hawajagundua kwamba awamu ya sita imevunja muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar bila maandishi au matangazo. Hadi sasa kuna makubaliano kwamba Zanzibar watajifanyia kila kitu ambacho nchi rasmi inafanya isipokuwa hawatakuwa na jeshi la ulinzi.

Na kuna makubaliano kwamba serikali ya muungano haitaingilia jambo lolote au kutoa maelekezo yeyote upande wa Zanzibar kwa sababu sasa wamekuwa kama serikali kamili. Hata ziara za viongozi wa serikali ya muungano kule Zanzibar zimedhibitiwa. Na pia mabalozi wa nje wanapewa nafasi zao, na nadhani raisi wa Zanzibar ndie anateua watu wake na raisi wa Tanzania kutangaza rasmi.

Haya yote yamefanyika kimya kimya, na naweza kudiriki kusema yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika mazingira ya kuwa na raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar. Hiyo imeonekana ni zile nafasi zinaitwa "it is now or never".

Ila jambo la kusikitisha ni kwamba katika hali hii Zanzibar ni kama imepewa fursa kubwa ya kujiendeleza haraka hasa katika miundo mbinu kwa sababu yajayo hayajulikani. Kama umeangalia vizuri, kuna miradi mikubwa ya miundo mbinu inayoendelea huko visiwani, pamoja na kubadilisha majengo ya shule karibu yote. Umewahi kujiuliza Zanzibar wanapata wapi fedha za kufanya haya mambo makubwa?

Ni kwamba, mbinu iliyotumika ni Tanzania kuchukua mikopo ya nje, ambapo sehemu kubwa sana ilienda Zanzibar kama gawio lao. Ile mikopo haikuwa kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania bara, mlengwa alikuwa Zanzibar. Ndio maana baadhi ya wanasiasa wa bara, walipogundua hilo walikasirika sana. Baadhi walijiondoakatika uongozi, baadhi waliondolewa, na inasemekana baadhi waliuwawa. Na tukumbuke kuwa daraka kubwa la kulipa hii mikopo liko Tanzania bara.

Ni kweli kwamba kuna fedha zinabaki Tanzania bara lakini faida kubwa ya ile mikopo ilikuwa ni kwa ajili ya Zanzibar. Tukichukua mkopo wa tuseme Trilioni 10, ukawapa Zanzibar gawio lao la trilioni mbili, zile trilioni mbili zinazoenda Zanzibar ni fedha nyingi sana kufanyia mambo mengi sana, wakati trilioni nane zinazobaki bara impact yake kuona zimefanya nini ni kidogo sana kwa sababu ya ukubwa wa nchi. Na ukweli ni kwamba mfumo wa gawio ulitengenezwa kwa kupendelea upande wa Zanzibar.

Sasa jambo ambalo limeanza kuwaamsha watu wa bara ni hili la meli za nje kusajiliwa Zanzibar. Kwa kiburi kabisa, pamoja na skendo zilizolikumba jina la Tanzania, Zanzibar wanadai tulishakubaliana tunajiendesha kama nchi kamili, na tuna haki ya kusajili meli. Wanadai kama hatutaki watumie jina la Tanzania basi mabadiliko yafanywe wazisajiri kwa jina la Zanzibar.

Na pia kuna baadhi ya wanasiasa wanahoji, kama Zanzibar wanaruhusiwa kujifanyia kila kitu kama nchi na kutoingiliwa, kwa nini bado wanateuliwa kwenye nafasi zinazohusu muungano au hata mambo ya bara peke yake? Baadhi ya majibu wanayopewa ni kwamba raisi ana uhuru wa kuteua timu yake ambayo ataona itamsaidia, na anaweza kuchukua watu bara au visiwani katika nafasi yeyote.

Kwa hiyo kila mtu akae akijua muungano haupo tena, makubaliano yamefanywa Zanzibar wajifanyie kila kitu isipokwa kuwaja jeshi, lakini makubaliano haya hayatatangazwa rasmi.
Inasikitisha sana
 
Mkuu; unaelekea una jazba na ujinga kidogo
Huenda huelewi unalolizungumza!

Lukuvi ni mmoja wa watu waliosema hayo, tena akiwa kanisani. Ukiniuliza ni katika mazingira gani, jawabu ni katika mazingira ya kuidhibiti Zanzibar. Huyo ni Lukuvi. Wengine waliosema hayo ni Samuel Sitta katika mazingira ya kuitawala Zanzibar. Hawa, naamini pamoja na utoto wako, unawakumbuka.

Mkuu, huenda waliosema hivyo ni Wakenya - akina Nyerere, Sitta na Lukuvi. Hivi ni nani alisema Watanganyika wamesema hivyo? Hivi kwa akili yako Watanganyika milioni 60 wote watasema hivyo? Watasema kupitia jukwaa gani?

Sasa iweje? Kwani si nimeshawahi kukuambia Wazanzobari walioupinga na nini kiliwakuta? Hapa hoja ni nini?

Swala la muungano wa mkataba mara zote linazungumziwa na Wazanzibari. Fuatilia hotuba za Jussa. Hakuna Mtanganyika aliyezungumzia muungano wa mkataba.

Huenda hata Kiswahili hukirlewi!! Nimesema: "Maneno haya yamesemwa na kurudiwa miaka ya 2020". Jee hapo nimesema yameanza miaka ya karibuni?

1. Kwanza sio kweli kwamba Watanganyika wanataka kujitenga. Nia ni ileile ya kuidhibiti Zanzibar. Hata haya ya sasa yanayoendelea ni kwa kuona kipindi hiki udhibiti umepungua kwani kiongozi ni Mzanzibari.
2. Ni viongozi wa CCM ndio wanaozuia hilo unamaanisha sio Watanzania (Watanganyika na Wazanzibari?)

Jifunze angalau kukumbuka. Nyerere, Sitta na Lukuvi waliyasema hadharani. Wacha kubabaika.

Kama hayana uzito nawe endelea kusema humu mtandaoni. Zanzibar ipo kwenye muungano muda wa kwamba JMT ipo. Vinginevyo itakuwepo kama Zanzibar huru bila kujali kwamba kuna mtu anachukia hilo.
Sawa.
 
Nashangaa sana kwamba Watanzania wengi, hasa watu wa bara, hawajagundua kwamba awamu ya sita imevunja muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar bila maandishi au matangazo. Hadi sasa kuna makubaliano kwamba Zanzibar watajifanyia kila kitu ambacho nchi rasmi inafanya isipokuwa hawatakuwa na jeshi la ulinzi.

Na kuna makubaliano kwamba serikali ya muungano haitaingilia jambo lolote au kutoa maelekezo yeyote upande wa Zanzibar kwa sababu sasa wamekuwa kama serikali kamili. Hata ziara za viongozi wa serikali ya muungano kule Zanzibar zimedhibitiwa. Na pia mabalozi wa nje wanapewa nafasi zao, na nadhani raisi wa Zanzibar ndie anateua watu wake na raisi wa Tanzania kutangaza rasmi.

Haya yote yamefanyika kimya kimya, na naweza kudiriki kusema yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika mazingira ya kuwa na raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar. Hiyo imeonekana ni zile nafasi zinaitwa "it is now or never".

Ila jambo la kusikitisha ni kwamba katika hali hii Zanzibar ni kama imepewa fursa kubwa ya kujiendeleza haraka hasa katika miundo mbinu kwa sababu yajayo hayajulikani. Kama umeangalia vizuri, kuna miradi mikubwa ya miundo mbinu inayoendelea huko visiwani, pamoja na kubadilisha majengo ya shule karibu yote. Umewahi kujiuliza Zanzibar wanapata wapi fedha za kufanya haya mambo makubwa?

Ni kwamba, mbinu iliyotumika ni Tanzania kuchukua mikopo ya nje, ambapo sehemu kubwa sana ilienda Zanzibar kama gawio lao. Ile mikopo haikuwa kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania bara, mlengwa alikuwa Zanzibar. Ndio maana baadhi ya wanasiasa wa bara, walipogundua hilo walikasirika sana. Baadhi walijiondoakatika uongozi, baadhi waliondolewa, na inasemekana baadhi waliuwawa. Na tukumbuke kuwa daraka kubwa la kulipa hii mikopo liko Tanzania bara.

Ni kweli kwamba kuna fedha zinabaki Tanzania bara lakini faida kubwa ya ile mikopo ilikuwa ni kwa ajili ya Zanzibar. Tukichukua mkopo wa tuseme Trilioni 10, ukawapa Zanzibar gawio lao la trilioni mbili, zile trilioni mbili zinazoenda Zanzibar ni fedha nyingi sana kufanyia mambo mengi sana, wakati trilioni nane zinazobaki bara impact yake kuona zimefanya nini ni kidogo sana kwa sababu ya ukubwa wa nchi. Na ukweli ni kwamba mfumo wa gawio ulitengenezwa kwa kupendelea upande wa Zanzibar.

Sasa jambo ambalo limeanza kuwaamsha watu wa bara ni hili la meli za nje kusajiliwa Zanzibar. Kwa kiburi kabisa, pamoja na skendo zilizolikumba jina la Tanzania, Zanzibar wanadai tulishakubaliana tunajiendesha kama nchi kamili, na tuna haki ya kusajili meli. Wanadai kama hatutaki watumie jina la Tanzania basi mabadiliko yafanywe wazisajiri kwa jina la Zanzibar.

Na pia kuna baadhi ya wanasiasa wanahoji, kama Zanzibar wanaruhusiwa kujifanyia kila kitu kama nchi na kutoingiliwa, kwa nini bado wanateuliwa kwenye nafasi zinazohusu muungano au hata mambo ya bara peke yake? Baadhi ya majibu wanayopewa ni kwamba raisi ana uhuru wa kuteua timu yake ambayo ataona itamsaidia, na anaweza kuchukua watu bara au visiwani katika nafasi yeyote.

Kwa hiyo kila mtu akae akijua muungano haupo tena, makubaliano yamefanywa Zanzibar wajifanyiho e kila kitu isipokwa kuwaja jeshi, lakini makubaliano haya hayatatangazwa rasmi.
@Whocares!!? Who fkn caress.!??
 
Ndipo mnapojifichia, kuuita ukweli unaosemwa kuwa ni chuki na ubaguzi. Mnataka siku moja watu wa Pemba na Zazibar wachinjwe kama kuku huku bara ndio mtajua tulikuwa tunawaambia kuna tatizo nyie mnsingisia chuki na ubaguzi
Wachinjwe kwa kosa lipi?. Hizi akili ndizo Nyerere alituonya mwaka ule wa 1995 pale Kilimanjaro Hotel.

Unaweza ukawaondoa kwa vurugu wapemba na waunguja halafu ukishamaliza utatafuta kabila jingine la kunyooshea vidole.
 
Huyo muungwana alitakiwa ajue kwamba huku bara kuna miradi mikubwa zaidi ya hiyo ya huko visiwani.

Uwanja wa ndege wa Tabora mradi mkubwa.

Daraja la Pangani na lile la Magomeni miradi mikubwa.

Ujenzi wa meli nne kule Karemi Ziwa Tanganyika miradi mikubwa sana.

Ndege nne zinakwenda kununuliwa mwaka huu zikiwa nyongeza ya zile 16 zilizopo, miradi mikubwa sana.

Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo mradi mkubwa sana.

Zanzibar inajengwa lakini Bara inajengwa zaidi na zaidi.
 
Bara kuna ufisadi ndio, na hizo zinazofisidiwa zingesaidia kutatua baadhi ya mambo, lakini haiondoi ukweli kwamba mikopo hii inapochukuliwa lengo ni kuipatia Zanzibar fedha za maendeleo kupitia mgongo wa Tanzania.

Na kama kuna ufisadi, kwani anaesimima nchi ni nani? Si huyo huyo anaechukua mikopo kwa ajili ya Zanzibar? Kwa nini hadhibiti huo ufisadi? Au ndio tuseme ana maslahi katika ufisadi unaofanywa bara ndio maana anauachia bila kuchukua hatua?

Unasema bara kuna ufisdi sana, nje nje, sasa tuambie, tangu huyu raisi achukue madaraka, wangapi umesikia wamekamatwa kwa ajili ya ufisadi? Huo ufisadi ambao hadi wewe unauona yeye hauoni kwa sababu anajiita chura kiziwi?
Ni sawa lakini toka lini ukasikia Zanzibar wananyosheana vidole juu ya ufisadi,kule watu kidogo Wana hofu ya mungu kwa pesa ya walipa Kodi ndio maana miradi inaonekana ikifanyika sio bara,huku watu wanawaza upigaji tu ko hata tukipewa trl 100 zitakazo enda kwenye lengo husika ni trl 20 tu.
Kuhusu yeye kuchukua hatua ni kwanini yeye ndo achukue hatua?labuda ungesema anatakiwa asikilize sauti za wachache wanaodai katiba mpya ambayo italeta taasisi imara hapo ndo kila mmoja atawajibishwa na mifumo bila kumtegemea mtu mmoja.
 
Back
Top Bottom